Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Nyerere ndiye kaweka misingi ya madudu yote yaliyofuatia.Ukimpatia Lissu saa moja atatumia dk 45 kumdiss Mwalimu Nyerere kwa maneno makali kadri atakavyoweza.
Alipoulizwa na Chief Odemba kwa maoni yake kuwa ipi ilikuwa awamu iliyoongoza kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, bila kumumunya maneno alidai ni awamu ya kwanza.
Kwa mtazamo wa Lissu, Nyerere alikuwa katili kuliko Mwinyi, Mkapa, Kikwete na JPM wote kwa pamoja.
View attachment 3073523
Kikatiba na kisheria.
Soma katiba ya Tanzania, mapungufu yote ni kazi ya Nyerere.
Soma ripoti ya Nyalali na sheria 40 kandamizi.
Mapungufu yote hayo ni ya kutoka uongozi wa Nyerere.
Ukimlaumu Magufuli kukataza mikutano ya hadhara, utakuja kuambiwa Nyerere alivipiga marufuku kabisa vyama vya upinzani miaka ya 1960s, kwa karibu miaka 30. Akawafunga wapinzani wake kina Joseph Kasela Bantu na Christopher Kassanga Tumbo
Sasa, mtu anayeangalia mambo kwa kina na kisheria kama Lissu, akiangalia mzizi wa matatizo yote, lazima aanze na Nyerere kama tatizo.
Kama hujasoma, soma kitabu cha Profesa Paul Bjerk "Building a Peaceful Nation: Julius Nyerere And The Establishment Of Sovereignty In Tanzania 1960- 1964" utajifunza mengi sana.