Shida ya Lissu na Nyerere ni nini hasa?

Shida ya Lissu na Nyerere ni nini hasa?

..serikali ya Muingereza ilikuwa inakusanya wanafunzi toka maeneo mbalimbali ya Tanganyika na kuwapeleka Government School Tabora.

..alichofanya Mwalimu Nyerere na kuongeza wigo wa jambo ambalo tayari lilikuwa linafanywa ama na serikali au makanisa.

..pia sio sahihi kusema alifanya Mwalimu Nyerere. Kauli sahihi ni SERIKALI ya Tanganyika au Tanzania ilifanya.

Point ni kuwa hata bila Nyerere shule zingejengwa na watu wangesoma. Tofauti ni kuwa mambo yangefanywa tofauti.

Kwa system ya Nyerere, Tanzania ilikuwa nyuma kielimu kwa Wastani kwa muda mrefu kumlinganisha na nchi nyingi za kusini na East Africa.
 
Yapo mambo mengi hayati JKN aliyakisea kwa makusudi au kwa utashi wa kibinadamu . Ikiweo kutuachia katiba ya mwaka 77.
Hakujitahidi sana kuendeleza au alififisha maendeleo kwa waislamu japo ndio waliochangia sana yeye kuleta uhuru. Katuachia " Imperial presidency" kwenye katiba
 
..hakukuwa na udini, wala ukabila.

..makabila na dini zote waliungana kudai kujitawala.

..Tanganyika hatukuwa koloni la Uingereza.
Kwa mujibu wa mwanahistoria Mzee Mohamed Said Udini ulijitokeza waziwazi ndani ya Tanu kuanzia uchaguzi wa kura tatu ambapo waislamu Wana Tanu ilibidi wawekwe kando Ili Wakristo wasomi wachukue nafasi zao.....
 
Nyerere ndiyo chanzo Cha mambo ya hovyo yote yanayotokea Kwa sasa.yeye Aliya asisi.mfano Mali za Tanganyika kuwa za wote na Zanzibar wakati huo Mali ya Zanzibar ni ya Zanzibar peke yake.Kingine katiba ilitungwa Kwa kujipendelea yeye.yaani kujipa madaraka makubwa na kuweza kuingilia popote atakapo kama mahakama na bunge.Makongoro Nyerere anatakiwa atuombe radhi watanzania wazalendo tunaojielewa kuhusu makosa makubwa ya baba yake
 
Kitabu hicho: Remembering Nyerere in Tanzania kimechapishwa na Mkuki na Nyota Publishers na kinapatikana online pia. Kina mkusanyiko wa maandiko kadhaa ya wadau mbalimbali kumhusu Nyerere tangu enzi za mkoloni hadi mwisho wake.
Kitabu nimekwisha kiona mkuu, nitakisoma.

Hayo mengine ya huko juu kwenye bandiko lako umemwagika kweli kweli kwa hisia nyingi.
Hakuna mtu mwenye akili inayofanya kazi vizuri anaye weza kuwa na sifa hizo ulizo ainisha wewe. Independence of mind is what matters in all this; and I am confident of having that asset.
 
Sawa kabisa na jina lako. hao ulio kuwa unasikiliza simulizi toka kwao hawakukuambia kuhusu lawama hiyo kubwa ya Nyerere kutoleta internet?
Hakukua na internet, lakini TV zilikuwrpo lakini hakuruhusu kwa kisingizio Cha Ujamaa. Eti watu watakaomudu kumiliki TV sets ni wachache.
 
Hakukua na internet, lakini TV zilikuwrpo lakini hakuruhusu kwa kisingizio Cha Ujamaa. Eti watu watakaomudu kumiliki TV sets ni wachache.
Nilijua hili litakuja hapa.
Wakati huo nyumbani kwenu mlihitaji sana TV kuliko kuweka donna juu ya meza? Hivi watu mbona mnajitoa uelewa kiasi hiki?
Watu wafe njaa, lakini wenye vihela, tena si zaidi ya asili mia moja waangalie TV? Hili nalo ni la kutolea lawama?

Huo ujamaa ndio uliosababisha pawe na ukosefu wa chakula? Najuwa kwa ujinga wako utasema ndiyo..., hapo jirani walikuwa na ujamaa, mbona kila baada ya kila miaka michache njaa zinawakumba.
 
Yule mzee alikuwa mroho wa madaraka, miaka yote ile hakukuwa na mtu mwingine wa kuwa rais?
Wapigania uhuru wengi wa africa walikuwa hawana maono ya mbali walijiona wao ndio wasomi na hakuna mwingine anaweza kutawala
 
Ndg.Lissu ni mropokaji sana...

Mropokaji haswa......

Ingekuwa si Nyerere yeye angesomea wapi?!!!

Nyerere ndiye aliyeikomboa mikoa ya kanda ya kati.....

Lissu aache mambo yake ya ajabu....

#JMT for ever[emoji7]
Upo sahihi,alikuja na kitu kinaitwa kota system...ili kuketa usawa wa elimu. Tundu wakati mwingine ni mbinafsi sana.
 
Ndg.Lissu ni mropokaji sana...

Mropokaji haswa......

Ingekuwa si Nyerere yeye angesomea wapi?!!!

Nyerere ndiye aliyeikomboa mikoa ya kanda ya kati.....

Lissu aache mambo yake ya ajabu....

#JMT for ever[emoji7]
Zamani mtu akinikosoa nilikuwa nachukia. Siku moja nilikuwa naongea na counsellor wangu kuhusiana na watu kunikosoa na huyu kiongozi ananiambia hivi: "mtu akikusoa anachosema ni kwamba katika eneo fulani hufanyi vizuri. Lakini hasemi kwamba kila eneo wewe ni hopeless hata unavyojisaidia chooni." Baada ya kutafakari vizuri niliona alinipa ushauri mzuri. Kwa hiyo, hata kwa Nyerere, Tundu Lissu hakusema kwamba Nyerere alikuwa mbaya katika kila kitu, isipokuwa katika ku'deal' na wakosoaji wake. Kwa upande wa Tundu Lissu, katika eneo hili Nyerere hakufanya vizuri. Lakini ni wazi katika maeneo mengine alifanya vizuri.
 
Sijasoma hata Uzi wenyewe,ila Huyu "mnyampaa" sio "conformist".
Mwalimu Nyerere amepatia Vingi,lakini Pia amekosea Vingi!
Huwa nashangaa kwamba huyu "MZEE" anatakiwa kusifiwa tu!
Tumeifanya Mila Kumuenzi "Mtu MMOJA"..yeye nani?
MUNGU?
 
Sawa....

Utafiti bora ni kuja na majibu yanayoeleza kuwa UBAGUZI WA KIKABILA ,DINI NA KANDA una "sequela" mbaya zaidi.....

Ingekuwa si baba wa taifa Julius K.Nyerere sidhani leo hii ndg.Tundu Lissu kutoka kanda ya kati angepata hata shahada yake ya kwanza ya LLB....

Ndg.Tundu Lissu aache mambo ya kitoto......

#Nyerere ni baraka kubwa kwa taifa hili[emoji7][emoji7]
Unamaanisha dunia nzima Nyerere ndiye alisaidia watu kupata shahada za LLB?
 
Back
Top Bottom