Shigongo adai Diamond anaelekea shimoni, awataja mameneja wake kama chanzo

Vipi huyu msukuma wa Bamaga bado ajaweka part 2?
 
Na ishu yoyote ukiona shigongo anazungumzia negative kaa ukijua interests zake zimeingiliwa.
[emoji115][emoji115]
Mwenye kusikia na asikie neno hili! [emoji115][emoji115]
 
Hii makala imenasia wapi tena?
 
shigongo ni kiboko hapa tusiposhtuka atafika hadi sehemu ya 100....
kweli pesa inatafutwa
 
Ungefafanua kaka mkuu kvp jamaa anaelekea shimoni?kvp mameneja wake wanampeleka jamaa shimoni?
 
Keshalipwa hela zake na CCM? Halafu Meghiji keshatolewa sijui nani atampa maji akienda Lumumba kudai hela zake. Mbali ya hayo Kakobe alishawatabiria wana CCM kwamba watakuwa wanapishana Lugha kama ilivyokuwa wakati ujenzi wa mnara wa babeli ulipoparaganyika!
 
Siku za nyuma kabla ya mitandao ya kijamii kupamba moto watu walinunua sana magazeti ya udaku, na ama kwa hakika waliamini kila kinachoandikwa na magazeti ya udaku ni ukweli usio na hata chembe ya uongo. Na ilikuwa ngumu kwa msanii kujisafisha maana njia ya kujisafisha ilikuwa ni kutumia magazeti hayo hayo ya udaku. Sasa hivi mambo yamebadilika sana, uongo na ukweli wote unapatikana kwenye mitandao ya kijamii. Hivyo gazeti la udaku likiandika habari zinakuwa tayari zimeshachacha, na pia kama ni habari ya uongo inajulikana mapema. Hii hali imepunguza kwa kiasi kikubwa sana wanunuzi wa magazeti ya habari za udaku. Yawezekana kabisa hii hali imemuathiri sana Shigongo.

Brand inatengenezwa kwa gharama kubwa sana. Diamond kufika level aliyopo sasa hivi si mashabiki peke yake, bali pia ni kujinyima, kujituma, ubunifu, kujitangaza na kuwekeza. Nyuma ya Diamond kuna timu kubwa inayomfanya afanikishe kazi zake. Unapotaka Diamond apige shoo kwa gharama ya shilingi elfu mbili je umefikiria kundi la wawezeshaji wake waliopo nyuma yake? Wapiga picha, wacheza shoo, fashion designers, mameneja, wapiga vyombo vya muziki, mavazi na wengineo. Je hawa wote wanalipwaje? Unaposema Diamond Platinumz unamaanisha kundi la watu linalomfanya awe level alizopo sasa hivi. Ni upuuzi sana kuhoji uhalali wa kiwango anachotoza Diamond wakati kazi zake tunaziona. Uwekezaji anaoufanya Diamond hauwezi kufanikiwa kwa kulipwa shoo moja milioni 3. Brand inapopanda thamani inamaanisha pesa nayo inaongezeka.

Kwa hili Shigongo kachemka na anapaswa kuwaomba radhi WCB. Asifanye njaa zake kuwa njaa za kila mtu. Yeye kama kashindwa kuaandaa shoo ni vyema atafute wadhamini wa kuweza kumuongezea pesa kama anaona ana ulazima wa kuandaa show inayomuhusisha Diamond. Ni vyema ifike mahali tukawaacha wasanii wafaidi matunda ya muziki wao kuliko kubaki waburudishaji kwenye bar.

[HASHTAG]#unfollowshigongo[/HASHTAG] [HASHTAG]#unfollowglobalpublishers[/HASHTAG]
 
Kwa sababu wana dalili zote za kimaslahi ya kwao wenyewe wawili. Shigongo ana hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…