Shigongo adai Diamond anaelekea shimoni, awataja mameneja wake kama chanzo

Shigongo adai Diamond anaelekea shimoni, awataja mameneja wake kama chanzo

Vipi huyu msukuma wa Bamaga bado ajaweka part 2?
 
shigongo ni kiboko hapa tusiposhtuka atafika hadi sehemu ya 100....
kweli pesa inatafutwa
 
Ungefafanua kaka mkuu kvp jamaa anaelekea shimoni?kvp mameneja wake wanampeleka jamaa shimoni?
 
Keshalipwa hela zake na CCM? Halafu Meghiji keshatolewa sijui nani atampa maji akienda Lumumba kudai hela zake. Mbali ya hayo Kakobe alishawatabiria wana CCM kwamba watakuwa wanapishana Lugha kama ilivyokuwa wakati ujenzi wa mnara wa babeli ulipoparaganyika!
 
Siku za nyuma kabla ya mitandao ya kijamii kupamba moto watu walinunua sana magazeti ya udaku, na ama kwa hakika waliamini kila kinachoandikwa na magazeti ya udaku ni ukweli usio na hata chembe ya uongo. Na ilikuwa ngumu kwa msanii kujisafisha maana njia ya kujisafisha ilikuwa ni kutumia magazeti hayo hayo ya udaku. Sasa hivi mambo yamebadilika sana, uongo na ukweli wote unapatikana kwenye mitandao ya kijamii. Hivyo gazeti la udaku likiandika habari zinakuwa tayari zimeshachacha, na pia kama ni habari ya uongo inajulikana mapema. Hii hali imepunguza kwa kiasi kikubwa sana wanunuzi wa magazeti ya habari za udaku. Yawezekana kabisa hii hali imemuathiri sana Shigongo.

Brand inatengenezwa kwa gharama kubwa sana. Diamond kufika level aliyopo sasa hivi si mashabiki peke yake, bali pia ni kujinyima, kujituma, ubunifu, kujitangaza na kuwekeza. Nyuma ya Diamond kuna timu kubwa inayomfanya afanikishe kazi zake. Unapotaka Diamond apige shoo kwa gharama ya shilingi elfu mbili je umefikiria kundi la wawezeshaji wake waliopo nyuma yake? Wapiga picha, wacheza shoo, fashion designers, mameneja, wapiga vyombo vya muziki, mavazi na wengineo. Je hawa wote wanalipwaje? Unaposema Diamond Platinumz unamaanisha kundi la watu linalomfanya awe level alizopo sasa hivi. Ni upuuzi sana kuhoji uhalali wa kiwango anachotoza Diamond wakati kazi zake tunaziona. Uwekezaji anaoufanya Diamond hauwezi kufanikiwa kwa kulipwa shoo moja milioni 3. Brand inapopanda thamani inamaanisha pesa nayo inaongezeka.

Kwa hili Shigongo kachemka na anapaswa kuwaomba radhi WCB. Asifanye njaa zake kuwa njaa za kila mtu. Yeye kama kashindwa kuaandaa shoo ni vyema atafute wadhamini wa kuweza kumuongezea pesa kama anaona ana ulazima wa kuandaa show inayomuhusisha Diamond. Ni vyema ifike mahali tukawaacha wasanii wafaidi matunda ya muziki wao kuliko kubaki waburudishaji kwenye bar.

[HASHTAG]#unfollowshigongo[/HASHTAG] [HASHTAG]#unfollowglobalpublishers[/HASHTAG]
 
Mmiliki wa kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo ameandika barua yenye ujumbe mzito kwa Diamond kupitia mtandao wa Instagram.

Kupitia mtandao huo, Shigongo ameandika:

Nampenda Diamond sana, tena sana (sina uhakika kama analifahamu hili). I am too proud of him! Ni fighter (mpiganaji), from Tandale to Beverly Hills with Neyo kwenye Video ya Wimbo wa Mary You ambao nimemaliza kuuangalia kwenye YouTube hakika si kitu kidogo. Nafahamu kwa sababu nimeanzia chini sana kimaisha.

Nikimkumbuka Diamond tangu siku ya kwanza nilipomuona hakika nina kila sababu ya kumuita is the true sign of Tanzania. Bila elimu ya kubwa, bila connection, bila fedha ameweza kuvuka vizingiti vyote hadi hapo alipo. Hakika ni mfano wa kuigwa kwa kila kijana wa nchi hii na duniani kote. BRAVO!

LAKINI ninayo machache ya kusema na ninaomba wale wepesi wa kutukana wanivumilie nitoe ushauri wangu kwa Diamond kama mzazi, kaka na Mtanzania mwenzake. Huko ANAKOELEKEA DIAMOND KUNA SHIMO, ASIPORUKA ATATUMBUKIA NA HUO NDIYO UTAKUWA MWISHO WAKE. Kwenye shimo hili Diamond anapelekwa na watu watatu, nao ni NASEEB ABDUL, BABU TALE NA SALAAM.

Nimemtaja Naseeb kwa sababu Diamond na Naseeb ni watu wawili tofauti.

Nitaendelea kesho.


Unadhani kwanini Shigongo anahisi Sallam na Babutale wanampoteza Diamond?
Kwa sababu wana dalili zote za kimaslahi ya kwao wenyewe wawili. Shigongo ana hoja.
 
Back
Top Bottom