Shikamoo "Muajemi"; Umeguswa, Umenuka!

Ila kwa kweli Irani jana kaonesha kitu amaizing, hajaomba kutumia nchi za jirani kufanya kazi yake, hizo nchi zilishuhudia tu anga inapitishwa silaha kuelekea nchi nyingine. Package ya kitu 300 sio mchezo
Pata taarifa sahihi, shambulizi hilo halijatekelelezwa na Iran peke yake, idadi ya hizo silaha zimechangiwa pia na washirika wake anaowafadhili kama Syria, Yemen na (Iraq?)

Halafu hii siyo mara ya kwanza kwa Israel kushambuliwa na Dola huru katika ardhi yake, Mwaka 1991 alipigwa kama hivi na Iraq lkn Israel haikujibu
Kuhusu urushaji wa hayo makombora, ni kawaida TU kwa sababu umbali kati ya Iran na Israel ni maili 620 sawa na umbali kati ya Tunduma na Dar
 
Vipi kuhusu Hamas walivyoua raia zaidi ya 1400 pamoja na Watanzania wenzetu wawili huku wakiimba allah wakbar, ?!
 
Israel sasa yupo njia panda...na kikao cha magenerali wa ulinzi kutopata jawabu la nini cha kufanya dhidi ya Iran kinaakisi hilo...Urusi nae amemtetea Iran katika Baraza la Usalama la UN kwa kusema kuwa alichokifanya Iran ni majibu ya alichokifanya Israel katika Ubalozi wa Iran, Dameski...Kwa miaka mingi Israel iliogopeka na waarabu kwa kuaminika kuwa ni wababe wa vita na teknolojia ya hali ya juu...sasa itawabidi wafanye jambo ili asionekane dhaifu...isije wadau wengine wakaendelea kumchokonoa...ila ngoma bado mbichi...
 
 
Vipi kuhusu Hamas walivyoua raia zaidi ya 1400 pamoja na Watanzania wenzetu wawili huku wakiimba allah wakbar, ?!
Ndio maana hapo chini nineongelea kisasi quran imefundisha namna bora ya kulipa kisasi

Qurani 2:194 aliyewachokoza mchokozeni kwa kadri alivyowachokoza.

42:42. Malipo ya ubaya huo sawa na ubaya huo

5:45 ....nafsi kwa nafsi

17:33 ..onyo usipite mpaka katika kulipa kisasi.

Kama hamasi kaua raia bila makadirio yuko hatiani au alichokozwa kwa kiwango kipi? Lakini vile vile vita haki kama mmevamiwa katika ardhi yenu na kufuta unyanyasaji
 
usisahau Hamas wamekuwa wanarusha rocket kwenda Israel back to back since 2014 lkn wao ndo wanaongoza kupiga mayowe
 
Hizo drones zimepotea bure tu
Israel inasema hasara iliyotumika ni kubwa ku intercept ayo makombora ya Ilani...

Hasara iliyopatikana

Iran = $60 Mil
Israel = $ 1.0 Bil
Apo wanasema hawajaweka cost za washira wake US,UK,France na Jordan....
Google uone in intercoptor moja ya Arrow 2&3 ina cost sh ngap??
Ndo maana US hataki hujinga maana anajua Israel hana uwezo wa kuzuia makombora ya Iran na American taxpayers ndo watakao umia... Iran mjanja sana hizi kamikaze zake (drone) ni very cheap $120,000 lakin kombora la kuzuia hizi linaenda mara kumi na zaidi itategemea wapi wametengeneza...So hivi vitakataka anavitumie ili vikuchoshe utumie interceptor missile zako umalize stock yako alafu nyuma anatuma madude cruise missile,Ballistic and hypersonic.....Russia walianza kuishiwa makombora wakawapigia goti wa Iran vikatumwa ivi vidubwasha easy to construct vya Iran ni long range yan kanatoka Dar mpaka Kampala usipokatungua kanakugonga ukikatungua kanakumalizoa makombola yako jiulize kwann Ukraine alipiga kelele sana baada ya Iran kuanza kuwapa Urusi ivi wakati yeye Ukraine alikua anazo Byaktar za Turkye??? Kwann US na EU waliweka vikwazo kwa Iran baada ya kumpa Mrusi ivi vitoi wakati US na wahairika wake waliwapa Ukraine airdefence zakutungua ndege na missile kwann wapigw kelele....Leo Russia akituma mzigo Ukraine anatanguliza Shaheed kamikaze drone za Iran km 40 ivi alafu yanakuja Iskender utasikia Zelensky kua tumetungua Drone za Iran 38 kati ya 40 mbili zimefikia lengo vipi kuhusu Cruise missile na iskander ballistic missile???
 
History inaonyesha ktk vita dunia ya pili, Waarabu wa palestine land walichagua upande wa Hitler ambaye alitaka kuangamiza western civilization na Wayahudi. Matokeo yake walishindwa vita. Mwaka 1948, 1967 na 1973 Waarabu walichagua kuchangamana na Soviet Union, hasimu wa western civilization matokeo yake vita zote walishindwa. Kipindi chetu Iran ameingia kwenye huo mtego wa kuungana na Urusi na Uchina ambao ni mahasimu w western civilization; mbaya zaidi kwa kuwategemea hao, Iran wanataka kulifutilia mbali Taifa la Israel. Waarabu wa Palestine, hasa HAMAS wameachana na Waarabu wenzao na kujiunga na Iran!! Je historia itajirudia?? Yaani Mamullahs wa Iran na Hamas wataendelea kuwepo? Mwaka huu wa 2024 huenda ukatuptia jubu

View: https://youtu.be/dEoVzKyD_IM?si=rrcGX4TGbyvnLxR2
 
Hypersonic zote zimepiga target.
 
Kwani hii vita ni ya kidini?.
 
.

Ningekuwa mimi ni Waziri mkuu wa Israel, huu ulikuwa ni wakati sahihi wa kurusha kombora juu ya jengo la Al Aqsa na kusingizia Makombora ya ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ท ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ท yameliharimbu jengo hilo.
Umewaza mbali mno, yaani huu ndiyo ulikuwa muda wa kuipoteza Palestine kwenye uso wa dunia...
 
Yetu macho na bundle maana yajayo ni lawama kwa u.s.a na IDF dhidi ya waarabu
 
Hahaha yani wameleta ndege vifaru na hatimae wameondoka ila jana tu iwe mwisho wa Palestina hii ni zaidi ya comedy
Wameondoka kwenda wapi? ๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„..

Wewe hujui Palestine ni Israel na Israel ni Palestine.?

Kifupi Palestine ni mchungwa wa uani wake Israel, muda wowote chungwa linapodondoka anaokota au anaacha.๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ