Mkuu nakubaliana nawe sarafu imeshukaJe, 'factor' ya dollar moja ya kimarekani kuwa sawa na madafu yetu zaidi ya 2,000/ haionyeshi kushuka kwa thamani ya madafu? Nakumbuka tuliwahi kuwa na $1 sawa na madafu 7 enzi fulani. Nini kilitokea tukafika hapa tulipo leo?
Siamini kuwa ni hayo uliyoeleza hapo wewe.
Huyo ndugu kajibu Yes and No, amejichanganya.
sarafu ni medium of exchange ambayo stabilization yake ni indicator ya hali ya uchumi. Ingawa kuna mazingira nchi inaweza kwa makusudi ikashusha thaman ya sarafu yake ili bidhaa zake ziwe cheap. Japan, China, Vietnam ni mifano ya nchi ambazo zinashusha thamani ya sarafu zao kwa makusudi.
Lakini hii ya Tanzania inatokana na factors za nje pamoja na ndani. Nje ni criss ya vita kubwa za Ukraine na Gaza ambako kumefanya suppy ya Nishati ipungue. Sababu za ndani zipo kadhaa ikiwemo BoP deficity iliyochochewa na Dola kutumika katika Ulipaji wa madeni makubwa ya Serikali nje ya nchi, Dola kutumika kununua mitambo na chuma kwa ajiri ya Miradi ya Nyerere Dam, SGR na Madaraja makubwa, na kudumaa kwa sekta za Utalii, Madini na Kilimo (wanasema zinakuwa lakini ukweli ni kuwa zimedumaaa ikilinganishwa potential yake). Sababu nyingine ni kushamiri kwa money rounderling inayotokana na kuongezeka kwa finacial crimes na mismanagement ya uchumi.
Hali hii siyo ngeni, iliwahi tokea mwaka 1980-1996 ambapo hali ilikuwa mbaya kuliko sasa. mfano mwaka 1991-1995 inflation ilipaa hadi 30%.
Aidha, Upo uwezekano hali kuwa mbaya zaidi 2025-2030 kwani serikali imekopa sana na ulipaji wa madeni hayo utakuwa katika peak kipindi hicho. Aidha, kipindi hicho kitakuwa ngwe ya lala salama ambayo mra nyingi ugubikwa na financial crimes za hatari ambazo uchochea inflation, Kumbukeni hali ilivyokuwa miaka ya 1990-95 (Ruksa); 2003-2005; 2012-15.
Mungu awasaidie viongozi wetu walipatie suluhisho hili.