Shillingi ya Tanzania yazidi kuporomoka dhidi ya shillingi ya Kenya

Shillingi ya Tanzania yazidi kuporomoka dhidi ya shillingi ya Kenya

Ndugu zangu kuna tatizo gani kwa shillingi yetu kuporomoka dhidi ya shillingi ya Kenya?. Juzi juzi shillingi shillingi 1 ya Kenya ilikuwa ikibadilishwa kwa Tshs.16.40 leo hii shillingi 1 ya Kenya inabadilishwa kwa Tshs.19.82. Kulikoni?. BOT mko wapi?.
Mkuu hii ni market forces.yaani ni kwamba shiling ya kenya imekuwa mhimu sana kwetu kuliko shilingi yetu kwao.Maana yake ni kwamba tunafanya miamala mingi ya shilingi ya kenya kuliko wakenya wanavyofanya miamala ya shlingi ya Tanzania

Dawa yake ni kuuza sana(finished good) kenya kuliko wao wanavyotuuzia sisi watanzania.Tuuze unga badala ya kuuza mahindi etc
 
Kenya kuwa nchi ya viwanda hiyo ni stori ya zamani. Hebu niambie kwa sasa Tanzania inaagiza vitu gani kutoka Kenya.
Bidhaa nyingi sana za plastic, soli za viatu, gundi, kiwi, dai, vikoi, cosmetics aina kibao, dawa za meno nk nk
VItu vyote hivyo vinapatilana ktk ubora wa juu zaidi.
Hata bidhaa wanazoagiza China ambazo nasi tunaagiza ila bado watuzidi ktk kuchagua ubora & design...wafanyabishara kibao wabongo huwa wanafuata nguo, vitambaa nk Kenya kuja kuuza Tz.
 
Mahaba kwa kenya yamezidi uwezo wako wa kufikiri.
Economics siyo maeno matupu bali ni mathematics. Hebu tuambie Trade balace kati ya Kenya na Tanzania

Anzia hapa kwanza:

Nimekuuliza TZ na KE tunanunua mafuta sote kwa Dollar nje ya nchi lakini huko kenya yanauzwa juu kwanini?
Nijibu kiuchumi.
Sio nikujibu kiuchumi! Simple reason ni Kodi na tozo TU hapo hakuna kingine maana geographically wote tuko Eneo Moja na wote tuna bandari kwa hiyo hakuna kisingizio cha gharama za usafirishaji.
 
Sio nikujibu kiuchumi! Simple reason ni Kodi na tozo TU hapo hakuna kingine maana geographically wote tuko Eneo Moja na wote tuna bandari kwa hiyo hakuna kisingizio cha gharama za usafirishaji.
Kwanini wanakuwa na Kodi na Tozo zinakuwa juu huko Kenya?
Wanataka kufidia kitu gani?
 
Kwanini hilo unalichukulia kuwa ni tatizo?
Pesa Yako kupoteza thamani unachukulia kuwa si tatizo, Tena kwa uchumi unaotegemea kununua nje zaidi ya kuuza! Si ajabu Kuna ajuza alisema "afadhali sisi tunanunua mafuta bei ya chini kuliko Marekani kwenye vituo"
 
Kwanini wanakuwa na Kodi na Tozo zinakuwa juu huko Kenya?
Wanataka kufidia kitu gani?
Sidhani kama hili ni swali la kuuliza maana nilishasema kuhusu sera za serikali husika. Mfano ukinunua umeme unakatwa REA. Je, ni lazima iwekwe hapo!? Ni mipango ya serikali.
 
Sidhani kama hili ni swali la kuuliza maana nilishasema kuhusu sera za serikali husika. Mfano ukinunua umeme unakatwa REA. Je, ni lazima iwekwe hapo!? Ni mipango ya serikali.
Ndio maana nikasema uchumi ni mathematics siyo emotions.
Unatakiwa ulete evidences za kimahesabu siyo maneno matupu.

Nimekuuliza simple question kuhus Petrol Price umeanza kuruka ruka.

Basi tueleze Faida ya pesa ya kenya ukiwa nayo hapa nchini on top of Tsh.
 
Pesa Yako kupoteza thamani unachukulia kuwa si tatizo, Tena kwa uchumi unaotegemea kununua nje zaidi ya kuuza! Si ajabu Kuna ajuza alisema "afadhali sisi tunanunua mafuta bei ya chini kuliko Marekani kwenye vituo"
Wewe zidisha kuzalisha halafu uuze bidhaa zako kwa bei uitakayo.

Unazalisha nini hapo ulipo zaidi ya mashuzi tu?
 
Ndio maana nikasema uchumi ni mathematics siyo emotions.
Unatakiwa ulete evidences za kimahesabu siyo maneno matupu.

Nimekuuliza simple question kuhus Petrol Price umeanza kuruka ruka.

Basi tueleze Faida ya pesa ya kenya ukiwa nayo hapa nchini on top of Tsh.
We mchumi uchwara, kwa nini mafuta Kenya bei ni juu ya Tz!?
 
Kweli tunao vilaza wa kutupwa hapa nchini. Hebu ndugu zangu fanyeni hii hesabu,,,

Dola moja hivi sasa ni Ksh 129.50 kutoka 162..75 mwezi wa Januari mwaka huu. Hii ina maana shilingi ya Kenya imezidi kuimarika katika kipindi hicho.

Hiyo hiyo dola moja kwa sasa ni Tsh 2,575.00 kutoka 2,510.00 mwezi wa Janauari mwaka huu ikiwa na maana shilingi yetu inazidi kuporomoka.

Jamani tuache unafiki, tuna hali mbaya. Ni vigumu hata kufikiria kuna wakati pesa hizi zilikuwa na thamani sawa...kwa kweli CCM inaiangamiza taifa hili.
huu ndio ukweli mchungu, hali itazidi kuwa mbaya Taifa linazidi kuingia mikopo mikubwa kwa ajili ya miradi ambayo hatma yake ni mashaka
 
Back
Top Bottom