Shillingi ya Tanzania yazidi kuporomoka dhidi ya shillingi ya Kenya

Shillingi ya Tanzania yazidi kuporomoka dhidi ya shillingi ya Kenya

Hoja yoyote ikiletwa lazima tujikite kwenye context kwa kutumia methodology ya
4WH (What, Who, When, Why, and How) Sasa kijana wangu tukikuuliza maswali ya How na Why usikimbie mada.

Kama umeshindwa kujibu waache wataalam wajibu. 🤣 🤣 🤣 🤣
Wewe unalazimisha tuendelee kuongelea WHAT tu.
Achana na mambo uliyokariri vitabuni. Sidhani kama uko kwenye level ya kujadiliana na mimi. Kwanza, naweza nikawa mzee wako badala ya kijana wako. Naona unavyosoma na ku"paste" usivyovielewa.

I only wish you knew what you are saying and who you are talking to...bye bye, nakuweka kwenye ignore list. Sina muda na wapuuzi...eti kuathili mtanzania. Rudi shule.
 
Achana na mambo uliyokariri vitabuni. Sidhani kama uko kwenye level ya kujadiliana na mimi. Kwanza, naweza nikawa mzee wako badala ya kijana wako. Naona unavyosoma na ku"paste" usivyovielewa.

I only wish you knew what you are saying and who you are taoking to...bye bye, nakuweka kwenye ignore list. Sina muda na wapuuzi...eti kuathili mtanzania. Rudi shule.
Mambo ya wewe kuwa mzee yanatoka wapi sasa. Wewe jikite kwenye mada hii. Tunaongelea Tsh.
Wewe eleza baada ya TSh kuporomoka against Ksh matoeko yake ni yapi katika jamii ya Tanzania?

Achana na personalities. Jikite kwenye mada. 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Ndugu zangu kuna tatizo gani kwa shillingi yetu kuporomoka dhidi ya shillingi ya Kenya?. Juzi juzi shillingi shillingi 1 ya Kenya ilikuwa ikibadilishwa kwa Tshs.16.40 leo hii shillingi 1 ya Kenya inabadilishwa kwa Tshs.19.82. Kulikoni?. BOT mko wapi?.
Huwa inatabia hyo Kuna kipindi ilikuwa 1 kwa 20 Tena siku zimepita sna
 
Acha uongo ni bidhaa zipi mnauza Kenya mpaka mjilinganishe na China wanaofanya over production.
Maparachichi....!!! "Shikamoo Maparachichi" muulize alianzia wapi? Mchele/Mpunga, Mahindi na gesi ya kupikia na yaviwandani nakadhalika. Najua unahitaji ushahidi.
===
The main products that Tanzania exported to Kenya were Corn ($118M), Petroleum Gas ($36M), and Kraft Paper ($32.4M). During the last 27 years the exports of Tanzania to Kenya have increased at an annualized rate of 11.7%, from $24.1M in 1995 to $482M in 2022. In 2022, Tanzania did not export any services to Kenya.

===
Hizo ni hela chache? Sasa kazi kwako. Kenya wametuuziaje? Au tumenunuaje kwao?
 
Kitu pekee mnachoweza kufanya na kupelekea devalue ni hizo rushwa na ufisadi wenu, ambazo zinapelekea miradi isiyokamilika au isiyo na tija. Kukosekana kwa utawala bora, luck of commitment n.k
Mkuu kwenye bandiko langu nimesema hoja husika Ina majibu mengi yawezekana nawe umekuja na jibu lako jipya. Asante
 
True kama nchi inazalisha sana na inashindana katika export basi unakuwa na advantage pesa yako ikiwa ina trade chini ila shida kama nyinyi kila kitu import basi tunashida. Ziko nchi pesa zao strong sana against dollar kama Djibout lakini maisha ni expensive sana na pesa yao haina soko. Tusichukuwe kila kitu negative au tusijiaminishe eti kuwa na strong Shilling ndio uchumi bora, hapana uchumi una mambo mengi sana ziko nchi pesa zao zina trade zaidi ya Dollar, mfano Kuwait, Oman hata Bahrain hawa Dinar moja ni kama dollar 3 lakini nchi za KSA na UAE hata Qatar 1 Riyal kama dola 3.6 sasa kwa akili zetu unaweza kusema hawa wanauchumi mkubwa kuliko USA, jibu hapana. Kuwait plus Oman hawafikii uchumi wa Saudia tu. Narudia kama tunashindana na Kenya kwenye export basi pesa yetu kuwa chini ya Kenya ni advantage kwetu kwanini? sababu wakija hapa na dola 100 anapata pesa nzuri Tsh inaweza kununua kwa wingi lakini ikiwa bidhaa yetu ni produce hapa hai link na US. Mfano mazao tutauza sana sababu tunazalisha ndani mkenya ataona 1000 Ksh haileti gunia lakini no nikichange Tz napata gunia na nusu. Lakini tukiwa watu wa import tu hapo tutakuwa na shida inflation itakuwa juu kwa bei za bidhaa.
Umeiweka vizuri na hoja yangu umeipa mashiko . asante sana.
 
Jamani tuache unafiki, tuna hali mbaya. Ni vigumu hata kufikiria kuna wakati pesa hizi zilikuwa na thamani sawa...kwa kweli CCM inaiangamiza taifa hili.
Heri ya Siku Kuu ya IDD, Mwalimu wangu wa Tuisheni hapa JF. Hakika nimefaidika sana na mabandiko yako hapa JF.

Kwa kuwa, Sasa hivi CCM ndiyo imeshika mpini(Ndicho Chama halali kinachoongoza serikali iliyopo madarakani), unashauri serikali hii ya CCM ifanye nini ili watanzania wanufaike na kuongezeka kwa thamani ya sarafu ya Kenya na kuporomoka kwa shilingi ya Tanzania. ?

Nina imani hutaniangusha Mwalimu, kwa kutoa majibu yanayoakisi upevu wako katika masuala haya ya maendeleo ya nchi zetu hizi, wakati wa kujibu swali hili. Asante.
 
Ndugu zangu kuna tatizo gani kwa shillingi yetu kuporomoka dhidi ya shillingi ya Kenya?. Juzi juzi shillingi shillingi 1 ya Kenya ilikuwa ikibadilishwa kwa Tshs.16.40 leo hii shillingi 1 ya Kenya inabadilishwa kwa Tshs.19.82. Kulikoni?. BOT mko wapi?.
Ninachokiona nchi sasa iende ikaboresha viwanda vyetu ili tupate bidhaa imara na bora ili tuache kutegemea maarifa ya nje.
 
Mbona hii simple tu.
Tanzania inataka ku protect wazalishaji wa ndani against wa kenya.

Maana yake import from Kenya will be expensive compare to export to Kenya.

Maana yake bidhaa za Tanzania zitakuwa cheap nchini kenya while bidhaa za kenya zitapotea kwenye soko la Tanzania.
Kama hii ndio sababu basi wataalam wetu nao watakuwa hawana akili vile vile.
Kenya ni nchi ya viwanda kuliko Tz so bidhaa nyingi zinazozalishwa Kenya huku Tz hakuna kwakuwa hatuna viwanda hivyo...sasa hiyo sera ya protectinism inatusaidia nn raia wa Tz zaidi ya kutusababishia uhaba wa baadhi ya bidhaa, tena baada ya muda ndio zitakuja kuuzwa bei juu zaidi!!.
Tz huwa inauza zaidi Kenya bidhaa za chakula kama viazi, mahindi, vitunguu nk pia mbao na mifugo kama ng'ombe na mbuzi.
% kubwa bidhaa za Kenya zinazoingia Tz hazipo huku and vice versa.
 
Kweli tunao vilaza wa kutupwa hapa nchini. Hebu ndugu zangu fanyeni hii hesabu,,,

Dola moja hivi sasa ni Ksh 129.50 kutoka 162..75 mwezi wa Januari mwaka huu. Hii ina maana shilingi ya Kenya imezidi kuimarika katika kipindi hicho.

Hiyo hiyo dola moja kwa sasa ni Tsh 2,575.00 kutoka 2,510.00 mwezi wa Janauari mwaka huu ikiwa na maana shilingi yetu inazidi kuporomoka.

Jamani tuache unafiki, tuna hali mbaya. Ni vigumu hata kufikiria kuna wakati pesa hizi zilikuwa na thamani sawa...kwa kweli CCM inaiangamiza taifa hili.
Wakati hizi pesa zilikuwa na thamani sawa, tulikuwa tumeendelea kwa kiasi gani?
 
Huyu kilaza yupo madarakani unategemea nini?
IMG-20240409-WA0000.jpg
 
Uchumi haupo hivyo kijana wangu. Ukiangalia Exchange rate anagalia pia na Inflation rate.

Uchumi ni kuhusu mtumiaji wa mwisho kijana wangu.

Ukitaka kujua hivyo angalia liter moja ya petrol kenya inauzwa dollar ngapi against bei ta Tanzania.

Kumbuka sote tunanunua mafuta in dollars.
Huu uongo wa wazi wazi. Wao kama wananunua mafuta kwa bei kubwa, unajua kwa nini bei yao ipo hivyo!? Inawezekana Kuna Kodi kubwa kwenye mafuta wao wameweka. Ila bei kwenye soko la Dunia ndiyo hiyo hiyo kwa sisi wote.

Hushangai watu wanapitishia magari kwenye bandari yetu, na Bado kwao bei zipo chini kulinganisha na sisi!
 
Kama hii ndio sababu basi wataalam wetu nao watakuwa hawana akili vile vile.
Kenya ni nchi ya viwanda kuliko Tz so bidhaa nyingi zinazozalishwa Kenya huku Tz hakuna kwakuwa hatuna viwanda hivyo...sasa hiyo sera ya protectinism inatusaidia nn raia wa Tz zaidi ya kutusababishia uhaba wa baadhi ya bidhaa, tena baada ya muda ndio zitakuja kuuzwa bei juu zaidi!!.
Tz huwa inauza zaidi Kenya bidhaa za chakula kama viazi, mahindi, vitunguu nk pia mbao na mifugo kama ng'ombe na mbuzi.
% kubwa bidhaa za Kenya zinazoingia Tz hazipo huku and vice versa.
Kenya kuwa nchi ya viwanda hiyo ni stori ya zamani. Hebu niambie kwa sasa Tanzania inaagiza vitu gani kutoka Kenya.
 
Huu uongo wa wazi wazi. Wao kama wananunua mafuta kwa bei kubwa, unajua kwa nini bei yao ipo hivyo!? Inawezekana Kuna Kodi kubwa kwenye mafuta wao wameweka. Ila bei kwenye soko la Dunia ndiyo hiyo hiyo kwa sisi wote.

Hushangai watu wanapitishia magari kwenye bandari yetu, na Bado kwao bei zipo chini kulinganisha na sisi!
Kwanini wanunue mafuta kwa bei kubwa? Hebu dadavua mwanauchumi mwenzangu.
 
Back
Top Bottom