Shilole athibitisha kupigwa na Uchebe, asema kuanzia leo yeye siyo mke wa Uchebe

Shilole athibitisha kupigwa na Uchebe, asema kuanzia leo yeye siyo mke wa Uchebe

Hayajakukuta mzee usiseme hvyo hujui alichokifanya huyo na huenda ukikifahamu unaweza kusema kwann asingemvunja ata mkono. Hawa wanawake hawa nadhan waliooa au wanaoishi na wanawake kwa mda mrefu watakuwa wananielewa
Hawajui jinsi gani mwanamke huwa na masimango akiwa na kazi na uwezo kifedha. "We una nini kwanza nakulisha tu" aisee hizi kauli chafu na kiburi nina hakika ndo vimemponza dada etu
 
Hii kitu hakikubaliki na kinasikitish lakini kama jamii tuache double standards. Wakati shilole anamkata makofi nuh na akihojiwa anaona kama ni sifa ila jamii na feminists walikaa kimya na wemgine kumbeza nuh atapigwaje na mwanamke. Leo mwanamke huyo huyo kapigwa naona Tanzania itasimama. Violance ni violance na inatakiwa kupigwa vita pasipo kuangalia jinsia ama umri
You're right on point son, and i like the way you think.
MKUU UISHI MILELE, NTAKUWA NAKUFUATILIA KWA KARIBU ZAIDI.
 
Kama atuna pesa hawa wasanii wa bongo freva na bongo movie sio wakuwaoa tuishie tu kuwaita ndugu ze2 na dada zetu nakumbuka ya Shamsha Ford pia, kiubwege ubwege tu mnaweza jikuta mnaharibiana maisha.
 
Mwanamke amezalishwa huko na wanaume watatu tofauti na wote kashindwana nao afu ustaadhi uchebe akajua ataweza kumtuliza?

Mambo ya kupigana ni ya kishamba lkn hivi huyu Shilole si alikuaga anambonda Nuhu Mziwanda mpk chalii anakimbilia kwny media kusema na Shilole akawa anajitapa akisema yeye hapendi upumbavu na kweli hua anampa chalii kichapo heavy.

I guess sasa amepata size yake.
Daah! Noma! Kibao kimebadilika sasa anakuja kulialia kwenye mitandao kutafuta huruma
 
Officialshilole Naandika haya, nikiwa na akili timamu na utulivu, La kwanza kabisa nataka KUOMBA RADHI JAMII YANGU. Naomba radhi kwa sababu niliwaaminisha ndoa yangu haina tatizo, huku ukweli ukiwa hauko hivyo, nimekuwa mtu wa kuambulia vipigo na MENGINE yasiyozungumzika, Naomba radhi kwa sababu niliposikia wanawake wenzangu wakipigwa niliwaambia PAZENI SAUTI, niliposikia mwanamke kule Kigamboni ameuwawa na kuchomwa moto niliomboleza na jamii na kusema Bora angesema".. huku mimi nikijikausha na kujitoa kwenye kundi lao wakati ukweli wangu MIMI NI MWENZAO, Naomba radhi.

Mimi ni kioo cha jamii, tena sura kubwa ya wanawake. Leo numeona nivunje ukimya kwa kuweka wazi kwamba MUME WANGU ASHRAFU SADIKI, maarufu kama UCHEBE AMEKUWA ANANIPIGA SAAANA, na tena hata baada ya kunipiga hajali kupiga simu wala kujua naendeleaje, nauguzwa na watu baki hospitali, na bado manyanyaso mengine yanayoikosesha hii ninayoiita Ndoa uhai na furaha

na zaidi nina WATOTO, watoto wanaoniangalia kama Baba na Mama, leo nikubali kufa na kuacha wanangu barabarani, SITAWEZA

'Uchebe' ni mwanaume niliyempenda, nilimvumilia kwa madhaifu yote, nikampa kila kitu, (Utu wangu, Mali Zangu na hata palipotakiwa kumuendeleza asimame mwenyewe nilifanya kwakuwa nilijua tuko pamoja), lakini HILO HALIKUWAHI KUZUIA VIPIGO, DHARAU NA USALITI.

Siku 2 zilizopita baada ya kutoka SABASABA KUTAFUTIA WATOTO WANGU NA KUMTAFUTIA YEYE NILIPIGWA SANA. SABABU ZA KUPIGWA NI MIGOGORO MIDOGO YA KAWAIDA AMBAYO IPO KWENYE KILA NDOA, sio kwamba amenifumania au mambo yanayoshindwa kuzungumzika, hapana, Tena Namuheshimu sana, lakini solution aliyoiona ni kunipiga kinyama bila huruma, tena kwa kunishtua na ngumi nikiwa usingizini, Kama mnavyoona picha hapo ni matukio ya siku tofauti tofauti.

Najua nitalaumiwa kwa kuweka hili mtandaoni, ILA SINA NAMNA, MAISHA YANGU NI MAISHA YA WATU KWA KIASI KIKUBWA, JAMII INANITAZAMA KAMA MFANO.. Nimefika mwisho, na kuanzia sasa naomba nisitambulike kama Mke wa Uchebe, ila Mama alieamua kuweka maslahi ya watoto wake mbele na kuamua kuwa mwenyewe kwa usalama na furaha yake

Wakati nahangaikia mambo yangu ya ndoa, post hii itumike kuwakumbusha wanawake TUVUNJE UKIMYA, TUPINGE UKATILI, TUTAKUJA KUULIWA SABABU

Pia soma > Shilole amchapa makofi mpenzi wake Uchebe mbele za watu

We Uchebe una matatizo gani.
Unapiga mtu wa watu?
Kesi kwa Mambosasa inakungoja!
 
Back
Top Bottom