Shilole athibitisha kupigwa na Uchebe, asema kuanzia leo yeye siyo mke wa Uchebe

Shilole athibitisha kupigwa na Uchebe, asema kuanzia leo yeye siyo mke wa Uchebe

Nimesikitika sana ..Kuna wanaume hawana shukrani mwanamke akustiri uonekane mtu mbele za watu na bado wamfanyia Mambo meusi..Hana haya na sura lake baya Kama sokwe.
Hata angekua anafanyia ndani kwake hana sababu ya kumpiga. umemshindwa mtu achaneni kwa amani, kwanza mwanaume alikua analelewaalitegemea anakula vya nani kama sio wanaume wenzie? Shilole kakosea angempiga hata chupa wawe even

Kutaka mwanamke wa mjini mzuri na uwezo wa kuhudumia huna lazima "big boys" wakusaidia tu, mtoto fala sana yule, ajifunze sasa kuwa vizuri gharama.
 
Na mm namshangaa, mm uchebe namjua vzr na ukwl ni kwamb shishi anaumaarufu tuu hela hana uchebe ndio anavisenti kdgo. Ukitaka kumpata uyu jamaa jioni kwenye maduka ya simu apa Makumbusho bus stand anakuwepo sana.
We Jamaa lazima umtetee Shilole. Si ulisema unashinda kwenye mgahawa wa Shishi unakula na kunywa bure[emoji23]
 
We Uchebe hujui kwamba Neno la MUNGU linatutaka wanaume tuishi na wanawake kwa akili??. Unataka kuumuua mtia nia ya kugombea ubunge wa jimbo la IGUNGA
 
Nimeona shilole ameandika Gazeti refu sana kuhusu uchebe lakini amini Shilole ndo anazingua na hii yote sababu ana Pesa so anaishi like Uchebe hawezi mwambia kitu. Ukiwa na hela zako bhasi usiolewe wewe tafuta viben ten vya kukupa raha siku moja moja bhasii ila sio Utake MUME.

Ukishaolewa hizo hela zako weka pembeni vaa uhusika wa Mke..Fanya majukumu ya Mke pia Kuwa Mtii kwa mume wako na Upunguze Kidomodomoo lasivyoo utakuwa unapigwaa mpaka ukome sababu mwanaume kuwa juu ya mke ni Nature ukitaka wewe ndo uwe juu bhasi Utaumiaa tuuu na mimi nasemaa mpigwee tuu mpaka mnyooke.
Screenshot_20200708-161933.jpeg
Screenshot_20200708-162021.jpeg
 
Officialshilole Naandika haya, nikiwa na akili timamu na utulivu, La kwanza kabisa nataka KUOMBA RADHI JAMII YANGU. Naomba radhi kwa sababu niliwaaminisha ndoa yangu haina tatizo, huku ukweli ukiwa hauko hivyo, nimekuwa mtu wa kuambulia vipigo na MENGINE yasiyozungumzika, Naomba radhi kwa sababu niliposikia wanawake wenzangu wakipigwa niliwaambia PAZENI SAUTI, niliposikia mwanamke kule Kigamboni ameuwawa na kuchomwa moto niliomboleza na jamii na kusema Bora angesema".. huku mimi nikijikausha na kujitoa kwenye kundi lao wakati ukweli wangu MIMI NI MWENZAO, Naomba radhi.

Mimi ni kioo cha jamii, tena sura kubwa ya wanawake. Leo numeona nivunje ukimya kwa kuweka wazi kwamba MUME WANGU ASHRAFU SADIKI, maarufu kama UCHEBE AMEKUWA ANANIPIGA SAAANA, na tena hata baada ya kunipiga hajali kupiga simu wala kujua naendeleaje, nauguzwa na watu baki hospitali, na bado manyanyaso mengine yanayoikosesha hii ninayoiita Ndoa uhai na furaha

na zaidi nina WATOTO, watoto wanaoniangalia kama Baba na Mama, leo nikubali kufa na kuacha wanangu barabarani, SITAWEZA

'Uchebe' ni mwanaume niliyempenda, nilimvumilia kwa madhaifu yote, nikampa kila kitu, (Utu wangu, Mali Zangu na hata palipotakiwa kumuendeleza asimame mwenyewe nilifanya kwakuwa nilijua tuko pamoja), lakini HILO HALIKUWAHI KUZUIA VIPIGO, DHARAU NA USALITI.

Siku 2 zilizopita baada ya kutoka SABASABA KUTAFUTIA WATOTO WANGU NA KUMTAFUTIA YEYE NILIPIGWA SANA. SABABU ZA KUPIGWA NI MIGOGORO MIDOGO YA KAWAIDA AMBAYO IPO KWENYE KILA NDOA, sio kwamba amenifumania au mambo yanayoshindwa kuzungumzika, hapana, Tena Namuheshimu sana, lakini solution aliyoiona ni kunipiga kinyama bila huruma, tena kwa kunishtua na ngumi nikiwa usingizini, Kama mnavyoona picha hapo ni matukio ya siku tofauti tofauti.

Najua nitalaumiwa kwa kuweka hili mtandaoni, ILA SINA NAMNA, MAISHA YANGU NI MAISHA YA WATU KWA KIASI KIKUBWA, JAMII INANITAZAMA KAMA MFANO.. Nimefika mwisho, na kuanzia sasa naomba nisitambulike kama Mke wa Uchebe, ila Mama alieamua kuweka maslahi ya watoto wake mbele na kuamua kuwa mwenyewe kwa usalama na furaha yake

Wakati nahangaikia mambo yangu ya ndoa, post hii itumike kuwakumbusha wanawake TUVUNJE UKIMYA, TUPINGE UKATILI, TUTAKUJA KUULIWA SABABU
Mwanadada ana nido za ukweli yaani naona jamaa alikuwa anamwagia wadhugu hapo hapo kifuani
 
Nimesikitika sana ..Kuna wanaume hawana shukrani mwanamke akustiri uonekane mtu mbele za watu na bado wamfanyia Mambo meusi..Hana haya na sura lake baya Kama sokwe.
Akusitiri mbele za watu alafu mkiwa ndani analeta dharau????
 
Back
Top Bottom