Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
1F70230F-13AA-4521-B56F-33278A4DC9F4.png

Jamii Forums (JF) ni Asasi ya Kiraia inayoratibu mtandao wa JamiiForums na kuhamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora.

Jamii Forums imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (citizen journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi wao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai. Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye mashindano ya uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko(Stories of Change).

Awamu ya kwanza ya shindano hili itaanza Julai 14 hadi Septemba 30, 2021.

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Uchumi na Biashara, Afya, Maendeleo ya Jamii, Utawala Bora na Uwajibikaji, Demokrasia, Kilimo, Sayansi na Teknolojia, Haki za Binadamu n.k.
  • Andiko linaweza kuwa la Kiswahili au Kiingereza lenye maneno yasiyozidi 1,500.
  • Mshiriki atapewa saa 2 tu kulihariri andiko lake baada ya kulichapisha jukwaani hivyo atatakiwa kuwa makini katika uwasilishaji wake
  • Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili
  • Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa ushirikiano endapo ataibuka mshindi
  • Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism haitaruhusiwa
  • Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki atalazimika kutaja chanzo
Jinsi ya kushiriki:
  • Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili
  • Maandiko yawasilishwe kati ya Julai 14 – Septemba 30, 2021 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )
  • Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.
ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Zawadi kwa Washindi

Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (40%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (60%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo

Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-

Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu shilingi Milioni 5
Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu shilingi Milioni 3
Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu shilingi Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop, Tablet na Simu za mkononi.

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
 
Upvote 0
Ukiamua andishi liwe la Kiswahili, tafadhali liwe la Kiswahili tu. Kama ni Kiingereza, basi tumia Kiingereza tu.

Tumeona ni busara kutoweka kiwango cha chini ili mtu ajipimie. Fupi sana isiyo na clarity itamuangusha mtu kirahisi lakini ndefu sana inayochosha itaifanya hadhira kutokumpa mtu kura.

Kuhusu umri: Mwishoni endapo mshiriki atakuwa ameshinda, proof ya umri itafikiwa. Ni wazi akiwa under 18 atakuwa amekosa kigezo hiki
Je mwisho wa kupost mada ni lini au ndio hio siku ya 15 Sep?
Yaani Deadline ya kuwasilisha mada ni lini?

Je maneno yasiwe chini ya mangapi?? Au hata maneno 300 rukhsa

NB. Walozi wa jf Tafadhali msiwaroge bodi ya majaji wa hili shindano maana hamshindwi kitu.
Tafadhali mkiwa mnazichambua mada kabla muitishe uwepo wa roho mtakatifu awaongoze na kuwalinda😅
 
Kuhusu umri:
Mwishoni endapo mshiriki atakuwa ameshinda, proof ya umri itafikiwa. Ni wazi akiwa under 18 atakuwa amekosa kigezo hiki

Hii si sawa hata kidogo, JF haina age limit kwenye kujiunga…. iweje kwenye mchele tubaguane.

Nilitamani sana mtoto wangu ashiriki, basi atashiriki kwa ID yangu na zawadi nitampokelea…. I’m way too 'giant' kugombea milioni TANO.[emoji1614][emoji36][emoji1493][emoji1493]
 
Hii si sawa hata kidogo, JF haina age limit kwenye kujiunga…. iweje kwenye mchele tubaguane.

Nilitamani sana mtoto wangu ashiriki, basi atashiriki kwa ID yangu na zawadi nitampokelea…. I’m way too 'giant' kugombea milioni TANO.[emoji1614][emoji36]
JF ina age limit. Wakati unaanzisha akaunti, system ilikuhoji juu ya umri ili ukiwa underage usiingie. Kama ulidanganya, basi ulikosea!

Hata hivyo, masuala ya mashindano yanayohusisha fedha yana sheria zake na mtu anayeruhusiwa kwa mujibu wa sheria kushiriki mashindano kama haya lazima awe na miaka 18 na kuendelea.

Pole sana
 
Naruhusiwa kupost mada ambayo nishawahi kuipost humu???

Pia mtu unaruhusiwa kuchanganya kiswahili na kingereza kama itahitajika kufanya hivo au ni kugha moja tu
chalii jaribu unaweza ukawa hata kwenye tatu bora
 
Je mwisho wa kupost mada ni lini au ndio hio siku ya 15 Sep?
Yaani Deadline ya kuwasilisha mada ni lini?
Septemba 15 kama tangazo linavyoeleza
Je maneno yasiwe chini ya mangapi?? Au hata maneno 300 rukhsa
Endapo wadau wataridhika kuwa maneno yako 300 yamebeba ujumbe mzito na unaoleta mabadiliko chanya katika jamii, sisi ni kina nani tukukatalie? Lakini, jopo la majaji pia litajiridhisha kuwa andiko lako ni ORIGINAL kwa maana kuwa hujatumia kazi ya watu na kuwa vigezo vingine vyote vimezingatiwa.

NB. Walozi wa jf Tafadhali msiwaroge bodi ya majaji wa hili shindano maana hamshindwi kitu.
Tafadhali mkiwa mnazichambua mada kabla muitishe uwepo wa roho mtakatifu awaongoze na kuwalinda😅
Hahaha, ndumba ngumu kufanya kazi katika shindano hili
 
Mapenzi, mahusiano na ujinsia, sasa sijaona muongozo wake ndo naulizia kwanza hapa.
Hiyo n.k kwenye tangazo inamaanisha hatujaweka mipaka uandike kuhusu jambo gani isipokuwa kigezo kikubwa ni kuwa liwe jambo linachochea mabadiliko chanya (sio lazima ya kisiasa).

Yawezekana andiko lako likanusuru mahusiano ya watu, ndoa ya watu au kuwasaidia wazazi katika kuwalea watoto kwa namna nzuri zaidi
 
Maxence Melo Mr samahani naomba ujibu swali langu.
Vipi kuhusu maudhui ya mapenzi, mahusiano na ujinsia inahitajika au?
 
Septemba 15 kama tangazo linavyoeleza

Endapo wadau wataridhika kuwa maneno yako 300 yamebeba ujumbe mzito na unaoleta mabadiliko chanya katika jamii, sisi ni kina nani tukukatalie? Lakini, jopo la majaji pia litajiridhisha kuwa andiko lako ni ORIGINAL kwa maana kuwa hujatumia kazi ya watu na kuwa vigezo vingine vyote vimezingatiwa.

Hahaha, ndumba ngumu kufanya kazi katika shindano hili
Ucahwi hauendi kwa mentali asee..😅
Haina shida mimi ngoja ninoe kichwa. Ila Kigezo cha mada kutokua imechapishwa mahala kisongekuwepo mambo yangenoga sana upande wangu
 
JF ina age limit. Wakati unaanzisha akaunti, system ilikuhoji juu ya umri ili ukiwa underage usiingie. Kama ulidanganya, basi ulikosea!

Hata hivyo, masuala ya mashindano yanayohusisha fedha yana sheria zake na mtu anayeruhusiwa kwa mujibu wa sheria kushiriki mashindano kama haya lazima awe na miaka 18 na kuendelea.

Pole sana

Mkuu, rejea upya mfumo wa kujiunga huenda kuna kitu mmesahau.

Ni kweli kwenye kujiunga tunajaza email na username tu, kama unamaanisha age limit ni muhimu basi rejea mfumo na urekebishe.
 
Hiyo n.k kwenye tangazo inamaanisha hatujaweka mipaka uandike kuhusu jambo gani isipokuwa kigezo kikubwa ni kuwa liwe jambo linachochea mabadiliko chanya (sio lazima ya kisiasa).

Yawezekana andiko lako likanusuru mahusiano ya watu, ndoa ya watu au kuwasaidia wazazi katika kuwalea watoto kwa namna nzuri zaidi
Naomba niweke wazi je kuhusu mada ya mahusiano ya mapenzi hasa kwa jinsia 1? Japo bandiko litahusu pia uchochezi wa mabadiliko ya fikra kwa upana wake kuhusu jambo hilo, vipi inakubalika au?
 
Naomba niweke wazi je kuhusu mada ya mahusiano ya mapenzi hasa kwa jinsia 1? Japo bandiko litahusu pia uchochezi wa mabadiliko ya fikra kwa upana wake kuhusu jambo hilo, vipi inakubalika au?
Ah, unataka kuandika kuhusiana na mapenzi ya jinsia moja? Tutaliangalia bandiko lako limekaaje kabla halijaenda kwa umma.

Again, mradi hujavunja sheria za nchi na taratibu za JF basi bandiko ambalo linaleta 'an impactful change' ambayo inaweza kuwa hata ni ya kubadili mindsets tu basi bandiko linakidhi vigezo kuingia kwenye shindano.

Karibu
 
Nilikujibu ndugu. Nadhani si vema nirudie majibu. No limits!
Baada ya ushindi utaratibu wa mshindi kulipwa hauwezi kukeuka usiri ambao mtu alijiwekea ?

Au mtatumia utaratibu upi kuhakikisha sisi wenye ID's ambazo zomejificha hatujulikani wazi kwa sababu za kiusalama binafsi ?
 
Kwenye kutangaza mshindi, tumekuwa wazi: Kama hutaki ku-disclose your identity usishiriki shindano kwa jina la kificho.

Hatuwezi kutoa zawadi kimyakimya, washindi wataonekana na watapewa zawadi zao wazi na kutakuwa na sherehe kwa ajili ya tuzo hizi.

Asante
 
Asante kwa ufafanuzi.
 
Ah, unataka kuandika kuhusiana na mapenzi ya jinsia moja? Tutaliangalia bandiko lako limekaaje kabla halijaenda kwa umma.

Again, mradi hujavunja sheria za nchi na taratibu za JF basi bandiko ambalo linaleta 'an impactful change' ambayo inaweza kuwa hata ni ya kubadili mindsets tu basi bandiko linakidhi vigezo kuingia kwenye shindano.

Karibu
Ahsante sana Mr kwa jibu lako zuri na maelezo yaliyokuwa safi na sahihi.
Ubarikiwe sana.
 
Back
Top Bottom