Shingi 200 leo kidogo inivue utu

Huyo jamaa alokuunganisha kazi angejua ni kiazi kiasi hiki angekutema...japo sijui kazi unayofanya lakini umeonesha personality ya aina ya kazi inayokustahili
 
Kazi aina gani inanistahili?
Kwa kugombania 200 stendi tena kwenye kadamnasi ya watu usiowajua kisa tu kupata sifa umejitia doa. Kuna watu wamekuona na ipo siku watakumbuka ulichofanya ila wewe hutowakumbuka. Na utanyimwa fursa kirahisi tu hivyo kwa aina ya personality uloionesha. Anyway nadhani umeelewa nachomaanisha sbabu title ya uzi wako tu ishajieleza
 
Nina sura moja ya kikomando nikikaaga kwenye dalalada kaz yangu ni kununa na kumkata jicho konda akija kudai nauli basi konda huniruka mwenyewe
Hahahah umenikumbusha kipindi nasoma chuo, ndo zilikuwa Zangu hizo. Sikuwahi kulipa nauli.
 
Aaah usiiishi kwa uoga ivo. Amna aliyenijua pale. Hamna atakayenikumbuka.
 
Usipende kuvimbiana na mtu kwa kesi ndogo kama hiyo mwengine anaweza kuwa na bisibisi akakumaliza,sometime unajifanya mjinga coz miambili ni hela ndogo sana.Kuna watu walishakata tamaa hawana cha kupoteza
 
Utakuja kupata madhara usipende kugombana na WATU .

Hiyo miambili ungrmuachia tu.
Sio kinyonge sasa! Nakumbuka siku nimeenda kumpokea wife mbezi hapo konda anadai hela ya mizigo nikamtoa aftatu (in wavaadela'svoice)anakaza nimuongeze nikaona isiwe shida. Nipe tiketi uliyokatia mzigo, anamuambia utingo rudisha mzigo kwenye buti
nikamuliza wife huu wote si mzigo wetu
ye: ndio...
Mimi: we sindio umeambiwa uchukue mzigo urudishe kwenye buti, mzigo huu hapa chukua hapo nimekunja ndita sio kitoto namsikia konda achana nae tuondoke hata aftatu wakasamehe
 
Utakuja kupata madhara usipende kugombana na WATU .

Hiyo miambili ungrmuachia tu.
Nipo radhi nimpe mhitaji yeyote sh 10,000 ya bure tu,hata akiniambia anaenda kunywea pombe poa tu,ila sikuachii 100 yangu kwa ubabe wako,nipo radhi nipoteze nyingi zaidi ili ku set precedence,nikikuachia leo utaona kumbe inawezekana,utatudharau watanzania wote, kataa ujinga kwa gharama yoyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…