Shingi 200 leo kidogo inivue utu

Shingi 200 leo kidogo inivue utu

Wataalam,

Leo nmepanda daladala hapa Dar, Yani saivi tu kama nusu saa ilopita nilikuwa natoka job nmeachana na yule broo aliyeniunganisha na hyo kazi(nmemuachia 30k)....

, Sasa nauli nakoenda ni 800, mi konda nikampa buku ila hakunrudishia chenji.
Ile nashuka nkadai chenji akasema eti ameshanipa halafu anakaza kichizi.

Nikamwambia "acha uxenge we kima, em tapika hyo 200"
Kumbe jamaa naye anataka anioneshe umwamba. Yeye anadai ashanipa chenji...nikimcheki juu ana rasta halafu macho mekundu. Mimi apo nmechomekea shati jeupe viatu vinang'aa kiwi.

Kujisächi mfukoni sioni hyo 200.

Nkaona huyu boya anataka anizoee,

Nikamshika shati Nikamwambia "we kima huondoki apa mpaka uniachie iyo 200"

Akasema '' nshakupa, kwahyo unataka nkurudishie chenji mara mbili upate na faida? "

Nkwambia "boya we hunijui"

Nkamkamata shingo apo nikashuka chinj huku namvuta kwa nje ya gari. Mda huo abiria wanalalamika wanawahi na dereva anamwambia anipe halo ka 200 waondoke.

ila jamaa akawa anaona kama zarau kuaibishwa vile, kwahyo tukawa tunadindiana kama majogoo wawili pale stendi.

Afu jamaa akiona nmechomekea anachukulia mim mchumba.

Stendi Zima ikasimama watu wote wameacha shughuli zao wanashangaa Hilo tukio la bro mtanashati aliyechomekea anadindiana na konda mvuta bangi kisa 200.

Nikamwambia "Oya, leo umeyakanyaga kmmk, Yani huondoki apa. hao abiria waambie watafute gesti maana watalala hapa, huondoki apa bila kuachia iyo 200"

Dah! Jamaa alivoona nmekaza sana na Niko serious halafu yeye ndo anapata hasara ikabidi aiteme hyo 200 na kuniachia.

Funzo: Sio Kila aliyechomekea ni don, mtumishi, wakuja au boya. Kuna wengine sisi ni maninja ila tunajidisguise kwenye mavazi tu. Msituchukulie simpo.
Huyo jamaa alokuunganisha kazi angejua ni kiazi kiasi hiki angekutema...japo sijui kazi unayofanya lakini umeonesha personality ya aina ya kazi inayokustahili
 
Kazi aina gani inanistahili?
Kwa kugombania 200 stendi tena kwenye kadamnasi ya watu usiowajua kisa tu kupata sifa umejitia doa. Kuna watu wamekuona na ipo siku watakumbuka ulichofanya ila wewe hutowakumbuka. Na utanyimwa fursa kirahisi tu hivyo kwa aina ya personality uloionesha. Anyway nadhani umeelewa nachomaanisha sbabu title ya uzi wako tu ishajieleza
 
Nina sura moja ya kikomando nikikaaga kwenye dalalada kaz yangu ni kununa na kumkata jicho konda akija kudai nauli basi konda huniruka mwenyewe
Hahahah umenikumbusha kipindi nasoma chuo, ndo zilikuwa Zangu hizo. Sikuwahi kulipa nauli.
 
Kwa kugombania 200 stendi tena kwenye kadamnasi ya watu usiowajua kisa tu kupata sifa umejitia doa. Kuna watu wamekuona na ipo siku watakumbuka ulichofanya ila wewe hutowakumbuka. Na utanyimwa fursa kirahisi tu hivyo kwa aina ya personality uloionesha
Aaah usiiishi kwa uoga ivo. Amna aliyenijua pale. Hamna atakayenikumbuka.
 
Usipende kuvimbiana na mtu kwa kesi ndogo kama hiyo mwengine anaweza kuwa na bisibisi akakumaliza,sometime unajifanya mjinga coz miambili ni hela ndogo sana.Kuna watu walishakata tamaa hawana cha kupoteza
 
Utakuja kupata madhara usipende kugombana na WATU .

Hiyo miambili ungrmuachia tu.
Sio kinyonge sasa! Nakumbuka siku nimeenda kumpokea wife mbezi hapo konda anadai hela ya mizigo nikamtoa aftatu (in wavaadela'svoice)anakaza nimuongeze nikaona isiwe shida. Nipe tiketi uliyokatia mzigo, anamuambia utingo rudisha mzigo kwenye buti
nikamuliza wife huu wote si mzigo wetu
ye: ndio...
Mimi: we sindio umeambiwa uchukue mzigo urudishe kwenye buti, mzigo huu hapa chukua hapo nimekunja ndita sio kitoto namsikia konda achana nae tuondoke hata aftatu wakasamehe
 
Utakuja kupata madhara usipende kugombana na WATU .

Hiyo miambili ungrmuachia tu.
Nipo radhi nimpe mhitaji yeyote sh 10,000 ya bure tu,hata akiniambia anaenda kunywea pombe poa tu,ila sikuachii 100 yangu kwa ubabe wako,nipo radhi nipoteze nyingi zaidi ili ku set precedence,nikikuachia leo utaona kumbe inawezekana,utatudharau watanzania wote, kataa ujinga kwa gharama yoyote
 
Back
Top Bottom