Shinyanga: Basi la shule laua Mwanafunzi muda mfupi baada ya kumshusha

Shinyanga: Basi la shule laua Mwanafunzi muda mfupi baada ya kumshusha

Boss la DP World

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
2,318
Reaction score
8,464
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Dereva wa gari la shule ya Msingi Samuu, Kassim Said Mahona (40) kwa kusababisha kifo cha mwanafunzi wa shule hiyo Godlight Chisawilo (04) kwa kumgonga na gari la shule hiyo Mjini Shinyanga.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema mwanafunzi huyo amegongwa na gari hilo baada ya kushushwa na gari hilo akitokea shuleni.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando tukio hilo limetokea Jumanne Juni 21,2022 majira ya saa 12 jioni katika maeneo ya Majengo Mapya Manispaa ya Shinyanga.

“Gari lenye namba za usajili T.151 DAG Toyota Coastar mali ya Malatia wa Shinyanga likitokea shule ya msingi Samuu kuelekea Majengo Mapya likiendeshwa na dereva aitwaye Kassim Said Mahona (40) na mkazi wa Nguzo Nane Shinyanga, lilimgonga mtembea kwa miguu Godlight Chisawilo (04) mwanafunzi wa shule ya chekechea Samuu na kumsababisha kifo chake”,ameeleza Kamanda Kyando.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari kutochukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara na tayari mtuhumiwa amekamatwa.
 
Kila bus la shule awepo mtu maalamu wa kuwavusha watoto sehemu salama kabla ya bus kuondoka.


Kwioooo [emoji239][emoji239][emoji239]
 
Utaratibu ,inatakiwa kila mtoto ashushwe na konda sijui msaaidiz unamvukisha barabara au kuhakikisha
Anapokelewa,
Sasa kuna hawa wengine wa magari wa ni kuwashusha tu kama abiria wa kawaida

Ova
 
It's sad kwa kila mmoja wetu humu hasa kama ni mzazi, hizi accidents za namna zinatokea mara kwa mara na kuzuia kunahitajika uwe na displine ya hali ya juu, wengi wetu humu ni madereva, je huwa tunaangalia chini ya uvungu wa gari kabla huja piga start?,je wakati w ku reverse huwa tunaangalia nyuma ya gari kama ni salama?
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia dereva wa gari la Shule ya Msingi Samuu, Kassim Said Mahona (40) kwa kusababisha kifo cha mwanafunzi wa shule hiyo Godlight Chisawilo (04) kwa kumgonga na gari la shule hiyo Mjini Shinyanga.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP George Kyando amesema tukio hilo limetokea jana Jumanne Juni 21, 2022 majira ya saa 12 jioni katika maeneo ya Majengo Mapya Manispaa ya Shinyanga.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari kutochukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara na tayari mtuhumiwa amekamatwa.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema mwanafunzi huyo amegongwa na gari hilo baada ya kushushwa na gari hilo akitokea shuleni.

Source: Malunde
 
Kila bus la shule awepo mtu maalamu wa kuwavusha watoto sehemu salama kabla ya bus kuondoka.


Kwioooo [emoji239][emoji239][emoji239]
Mkuu, huyo mtu alikuwamo kabisa kwenye bus. Sema tu hawa dada zetu nao na uvivu unawasumbua. Sasa hatukuelewa kwa nini alishindwa kuwavusha hao wato mpaka kwa dada wa kazi aliyekuwapo kuwapokea. Yaani watoto wameshuka tu yeye akabaki kwenye gari. Kumbe maskini watoto wamevukia mbele ya Bus. Dereva alikuwa mzembe na Madam alikuwa mzembe! Almanusura alete majanga makubwa maana katoto kalikuwa kameshikwa mkono na mkubwa wake, sasa angeua wote wawili sijui ingekuwaje!
 
Kila bus la shule awepo mtu maalamu wa kuwavusha watoto sehemu salama kabla ya bus kuondoka.


Kwioooo [emoji239][emoji239][emoji239]
... kwani wa kwetu Kanumba wanavushwa na nani alisikika mlevi mmoja uswahilini huko akiropoka.
 
😭😭😭😭😭inallilah wainailah rajiun Allah ni mjuzi
 
Iko Hivi,
Dereva Baada ya Kumshusha Mwanafunzi,Yuke Mtoto akawa anapita Kwa Mbele ili Aende Kwao,Dereva Akaondoa Gari akamgonga,
Anasema Alidhani Mtoto amepita kwa Nyuma ya Gari![emoji24][emoji24]
Note:Usalama:
Madereva na Wafanyakazi wa haya mabasi wanatakiwa Kufundishwa safety,
Kuhakikisha Mtoto waliemshusha amefikaNyumbani au Amevuka Barabara ndio Aondoe Gari!
Alitakiwa Kumuuliza Tingo wake/Mhudumu wake kuhakikisha Mtoto amevuka salama!
Shinyanga Is My home!
 
Back
Top Bottom