Shinyanga: Polisi wafanikiwa kuzuia ndoa ya binti aliyefaulu kwenda kidato cha tano

Mbona vurugu haijatokea. Mnavamia harusi kutafuta umaarufu. Mara muanze kuwapiga picha maharusi Kama kuwadhalilisha.
Haijatokea ndio jambo la kushukuru, watu washajiandaa kwa sherehe kama hiyo alafu unaingia kati kuisitisha unafikir ni jambo dogo lazima ujiandae kwa lolote mkuu
 
Hii ishu siwezi kushangaa,mabinti wana shida sana simetime,kuna binti wa jamaa yangu alichaguliwa kwenda A-Level,likatokea jamaa linataka kumuoa,binti akamwambia baba yake asimpeleke A-Level badala yake aolewe kwanza,kisha baada ya kuolewa ndio aende vyuo vya nursing.Tukamuonya na kumshauri sana ndio akakubali,mwaka huu anahitimu Chuo kikuu.
 
Lolote linaweza kutokea mkuu lazma ujihami
Bunduki ndo njia ya kujihami kwa raia wasiokuha na record ya uhalifu….

Au ndo penye kutumia akili/skill ndo tunatumia nguvu..
 
What if kama kungetokea vurugu unafikir hao polisi wangejihami vipi ?
What if bunduki ingetumika vibaya….inaenda na bunduki kwenye watu wasio jihami tena watu wapo kwenye furaha…

Sema polisi wetu kwenye issue ya intelligensia wapo zero….ila wanatumiaka vibaya sana na wanasiasa
 
Iwe kiki,isiwe kiki,muhimu,tukio lishafanyika na ndoa kwa mwanafunzi ishazuilika
Shida sio kuzuia ndoa ya mwanafunzi shida wazuiaje hiyo ndoa.

Kuzuia ndoa ni sahihi,wanamlinda mtoto .

We unafikiri hiyo situation haitamuathiri huyo wanaemlinda??
 
Shida sio kuzuia ndoa ya mwanafunzi shida wazuiaje hiyo ndoa.

Kuzuia ndoa ni sahihi,wanamlinda mtoto .

We unafikiri hiyo situation haitamuathiri huyo wanaemlinda??
Kawaida kuzuia matukio kama haya inawezkuleta athari kama hapatokuwepo nguvu ya kutosha, kwa aina ya tukio hilo,hakuna ubaya nguvu iliyotumika.
 
Huyo mdada akienda kusema sutaki kwenda form five,badala yake nataka kwenda chuo cha kati,itakuaje?
Wamezingua.
Au akisema hataki kusoma anataka kuwa mkulima na mfanyabiashara wa mazao.
 
Acha kudanganya watu sheria ya ndoa imeruhusu mtoto wa miaka kumi na nne kuolewa kwa ridhaa ya wazazi Kama wazazi wamekubaliana wewe unaingilia Nini?. Halafu kitu kingine elimu ya msingi ni form four kwa Sasa. Sasa kashavuka huko Bado mnamfuatilia.
Acha kuchanganya mambo,sheria hiyo haijasema Mwanafunzi wa secondary ruksa kuolewa
Mnashabikia Wanafunzi kuolewa
 
Ikiwa ni tofauti ya siku mbili tangu kuadhimishwa siku ya mtoto wa Afrika ilikwend ana kauli mbiu ya Mpe nafasi msichana boresha sheria ya ndoa na kuchagizwa na mabango yenye jumbe mbalimbali kama USINIPE MUME NIPE ELIMU.


Kichwa cha Post yako na video iliyopo vinatofautiana kwani ndoa ilikwishafungwa, polisi walizuia tafrija ya mkwilima na bi harusi.
 
Nikikuuliza nionyeshe Id yake yoyote inayomtambulisha kama mwanafunzi sjui utanipa hoja gani.....

Id yake ya Uanafunzi ime-expire tarehe 31/12/2022 na mpaka sasa hana Id yoyote inayomtambulisha kama mwanafunzi wa shule flani......, Kwa mantiki hyo tayari anatambulika kama Raia wa kawaida mwenye haki zote za Msingi....

Hivyo kuingilia ndoa yake ni kama kuingilia uhuru wake na mawazo yake kwa Ujumla hivyo itampelekea kupata matatizo ya kisaikolojia mfano kutojiamini na kujiona mnyonge na asiye na thamani.

Mkuu wa Wilaya anapaswa kuwajibika kwa kumlipa fidia muathiriwa...

Nitafutieni namba za familia yao tukapande kizimbani tujibishane kidogo[emoji28]
 
Nyie wazazi mapopoma endeleeni kuuchonga tu hapa nyuma ya keyboard zenu tutawavunja miguuu! Ozesheni watoto wa kike walioko shuleni tuone kama mtasalimika!
 
Nyie wazazi mapopoma endeleeni kuuchonga tu hapa nyuma ya keyboard zenu tutawavunja miguuu! Ozesheni watoto wa kike walioko shuleni tuone kama mtasalimika!
Wewe nani amekwambia yeye ni mwanafunzi na kigezo kipi haswa wametumia kumuita yeye mwanafunzi
 
Ni wazazi ndiyo wanataka binti aolewe wapate mahari wakati binti amechaguliwa kuendelea kidato cha tano

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…