Shinyanga: Polisi wafanikiwa kuzuia ndoa ya binti aliyefaulu kwenda kidato cha tano

Shinyanga: Polisi wafanikiwa kuzuia ndoa ya binti aliyefaulu kwenda kidato cha tano

Mabinti kuolewa wala hakukatishi ndoto ni kukariri maisha tu.

Rais wa nchi hii alihitimu kidato cha nne 1977 na mwaka 1978 akaolewa!

Ndoto zipi hajatimiza?
Inashangaza, hii nguvu pia ingetumika kuzuia zinaa, maana kama walikua wanafanya kwa kujificha hakukua na shida, wamefuata njia sahihi watu wanaingilia
 
Inashangaza, hii nguvu pia ingetumika kuzuia zinaa, maana kama walikua wanafanya kwa kujificha hakukua na shida, wamefuata njia sahihi watu wanaingilia
Sio kazi ya serikali kupambana na zinaa, hayo ni mambo ya dini.
 
RC ndiyo kazi aliyopewa na Rais?

Wazazi hawana pesa za kumsomesha, sasa RC agharamie gharama za matumizi na za masomo
 
Hapo Serikali wamewatumia Kama kafara la funzo kuogopesha wengine.
Wasiishie hapo wamlipie na ada kabisa.
Sasa hao ni waumini gani ambao walikuwa wanapata mafundisho ya Mapenzi ya jinsia moja? Waende madhehebu mengine ambayo yanafundisha Kweli ya Neno la Mungu siyo mafundisho machafu kama hayo!
 
Ikiwa ni tofauti ya siku mbili tangu kuadhimishwa siku ya mtoto wa Afrika ilikwend ana kauli mbiu ya Mpe nafasi msichana boresha sheria ya ndoa na kuchagizwa na mabango yenye jumbe mbalimbali kama USINIPE MUME NIPE ELIMU.

Huko mkoani Shinyanga hali ni tofauti kabisa kwani imejitokeza tukio la kuozeshwa binti aliyefaulu na kuchaguliwa kwenda kidato cha tano. Wazazi wameona ni bora mtoto huyo akaolewe na kukatiza ndoto zake za kuendelea na maso.

=====
Jioni ya jana timu ya wataalam mbalimbali ikiambatana na Mhe Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christine Mndeme na vyombo vya DOLA wamefika katika kijiji cha Mwawaza na kufanikiwa Kuzuia NDOA ambayo Bi Harusi ni Mwanafunzi aliyechaguliwa kuingia kidato cha tano ila wazazi wake wakaamua KUMUOZESHA Sasa Hawa Wazazi watajua kuwa Shinyanga ya Mndeme ni ya ELIMU na SIYO kuoa WANAFUNZI.

Daah ukute hapo muda wa mpunga ulikuwa ndio unakaribia alafu umewaambia nyumbn msipike Leo naenda kula harusini.
 
Kwenye mambo ya kutumia akili tunatumia nguvu kubwaa polee Tanzania…..sasa bunduki za nn apo,Aya tuseme bint alikuwa na mpango wa kwenda chuo
What if kama kungetokea vurugu unafikir hao polisi wangejihami vipi ?
 
Eti nipe Elimu,wanawake wangapi wanamaliza University wanakosa kazi,wanaishia kuwa michepuko au kudanga.Halafu Kuolewa si mwisho wa elimu,unaweza ukasoma chuo ukiwa umeolewa.Mimi ningekuwa huyo binti ningewashtaki hao mkuu wa mkoa,wangenipa fidia na shule siendi ningeanza kupiga biashara na mme wangu.
 
Hii nchi sasa viongozi wamekosa Kazi ya kufanya......

Binti anautaka mwenyewe mkongojo......!wanaingilia faragha za watu......

Wakati kuna Kazi nyingi tu za wao kufanya hata kumshauri mama kuhusu Bandari zetu kuuzwa...

Wao viongozi hiyo ndiyo Kazi pekee wanayoweza kuifanya.....kuingilia mapenzi watu walioridhiana kwa hiari yao.

Nonsense!
 
Serikali kujua yote yaliyonyuma ya hiyo ndoa ni jamii yenyewe waliotoa taarifa na unaweza kukuta ni Binti mwenyewe au ndugu baada ya kutokubali ndoa ifanyike.
Hapo itakuwa ni Kuna mwamba alimtaka binti kachomoa kamwambia tutaona akamchoma police
 
Hii nchi sasa viongozi wamekosa Kazi ya kufanya......

Binti anautaka mwenyewe mkongojo......!wanaingilia faragha za watu......

Wakati kuna Kazi nyingi tu za wao kufanya hata kumshauri mama kuhusu Bandari zetu kuuzwa...

Wao viongozi hiyo ndiyo Kazi pekee wanayoweza kuifanya.....kuingilia mapenzi watu walioridhiana kwa hiari yao.

Nonsense!
Ili kuzuia hii Tabia kuenea kwa wengine
 
Kama mtu anataka kudanga,adange tu,ila asiwe mtoto wala mwanafunzi,kusoma na kupata ajira ni ishu nyingine,muache asome,siyo unakuja kusema eti kwa sababu ajira hakuna basi asisome,kha ya wapi haya.
Halafu mbona unakomalia sana huyo mwanafunzi kuolewa,au na wewe ndo wale wale
Akili ya kusoma anayo? Maisha Sio shule
 
Kwani hapa Bongo Elimu ya lazima ni mpka ufike level gani!?
Hapa wamezingua mtu amehitimu form four akili yake tiari imeshakomaa kuendelea kusoma na kuto endelea kusoma ni mamuzi yake yeye mwenyew kuamua siyo kuamuliwa .

Sjui hapa ni kigezo gani kimetumika kuvuruga harusi ya huyo binti
 
Back
Top Bottom