Uchaguzi 2020 Shinyanga: Salum Mwalimu amepata ajali eneo la Msoka akitoka kwenye kampeni za Urais jimbo la Msalala

Uchaguzi 2020 Shinyanga: Salum Mwalimu amepata ajali eneo la Msoka akitoka kwenye kampeni za Urais jimbo la Msalala

Sasa wewe unaguna akishauriwa Mgombea Mwenza akasaidiwe na Magufuli japo gari moja?
Hata wao wanajua ni ubishi tuu, hata hospitali walipopelekwa baada ya ajali ni kazi ya rais, tena utakuta ni kati ya zile hospitali mpya alizojenga kwenye 5 ya kwanza.
Gerald .M Magembe John Pombe Magufuli ni kama maji, usipoyanywa utayaoga
 
Tunapokea habari kuwa mgombea mwenza wa CHADEMA ndugu Salum Mwalim amepata ajali ya gari nadhani maeneo ya Msalala
====
Tumepata ajali mbaya sana eneo la Msoka Kata ya Ngogwa, Jimbo la Msalala tukitoka kwenye mkutano wa Kampeni jimbo la Msalala tukienda kwenye mkutano wa Kahama.

Kwenye gari alikuwepo Mgombea Umakamu wa Rais (CHADEMA), Mheshimiwa Salum Mwalimu, Katibu wa Makamu wa Rais, Gerva Lyenda, Mlinzi, Omary na Dereva, Haule.

Gari ilipinduka kuzunguka mara tano.

Mpaka sasa wote tupo salama, labda kama kutakuwa na maumivu ya ndani.

Dah pole sana Salum Mwalim. V8 zinahitaji madereva wenye uzoefu na barabara za vumbi zinahitaji mwendo mdogo.
 
Mkuu kuna mgombea udiwani ni mtoto wa mganga wa kienyeji aliwambia wasikanyage huko wakawa wabishi
Kumbe uganga wa kienyeji una nguvu kiasi hichi?
basi tuangalie jinsi ya kutumia hiyo teknolojia kwa maendeleo ya taifa💃💃💃💃
 
Dah pole sana Salum Mwalim. V8 zinahitaji madereva wenye uzoefu na barabara za vumbi zinahitaji mwendo mdogo.
pale kuna mauzauza hakuna kampeni yeyote inaendelea kuna mtoto wa mganga wa jadi anagombea hata ccm hawafanyi kampeni huko
 
Poleni sana wahanga, Mnapaswa kuwa makini barabara hiyo ni ya udongo ,vumbi na rasta za kutosha. Hupaswi overtake na speed ama zaidi ya 60..... ama chini ya 20.
 
Poleni sana wahanga, Mnapaswa kuwa makini barabara hiyo ni ya udongo ,vumbi na rasta za kutosha. Hupaswi overtake na speed ama zaidi ya 60..... ama chini ya 20.
Sema V8 kwenye vumbi hazifai kabisa. Tena ni hatari mno, zinahitaji mzoefu wa barabara za vumbi
 
Hua zinafanyaje?
Dereva akikanyaga mbav za mbwa na akijaribu eithe kushika brake au kuirejesha gari basi hapo utaona gari imeanza kukatika mauno na mwisho wake ni kuzunguka mara kibao. Zile za PSU zimetengenezwa maalumu lakini hizi za kawaida zinakuwa nyepesi sana.
 
Barabara za vumbi bado zipo?!

Nilisikia 2015 mkinichagua naenda kumalizia tu, barabara nchi nzima zitakuwa lami!
 
eddy funguka zaidi.
Kuna mwanamziki nae aliangukia hapohapo yule mganga ni noma
Poleni sana wahanga, Mnapaswa kuwa makini barabara hiyo ni ya udongo ,vumbi na rasta za kutosha. Hupaswi overtake na speed ama zaidi ya 60..... ama chini ya 20.
Hilo eneo linaitwa nyanhwale, lina mauzauza ya kichifu mtu anaanguka anaendesha baiskeli sembuse gari, hata halmashauri ya msalala iko kahama mjini ndo ujue hapafai
 
Mungu yupo upande wetu.

Alegee na kushindwa yule muovu shetani anayetaka kuingilia mpango wa Mungu kuifanya Tanzania na wananchi wake 2020 wapate neema, furaha na uhuru katika maisha yao ya Haki.
 
Back
Top Bottom