#COVID19 Shirika la Afya Duniani (WHO) laitaka Tanzania kujiandaa kupokea chanjo ya Corona

#COVID19 Shirika la Afya Duniani (WHO) laitaka Tanzania kujiandaa kupokea chanjo ya Corona

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mwisho wa siku hii chanjo tutapewa bure huku wengine wakiinunua kwa gharama mara mbili!

Saa nyingine mikwara ya JPM inasaidia sana.
wachahe saana watakuelewa
 
It is a small World after all. Kama Dunia ilivyopambana na magonjwa ya kutisha polio, kifua kikuu, Ebola (ambayo bado inasumbua) Surua n.k. ndiyo hivyo hivyo juhudi ya Dunia yote kwa kushirikiana na WHO inahitajika ili kupambana na COVID-19. Huyo anayejiita mwendawazimu hana ubavu wowote wa kushindana na Dunia.
angalia hayo mauzauza ya chanjo yenyewe.. acheni ukilaza
IMG-20210128-WA0007.jpg
 
Namuona mtu akiinua mikono juu kutii amri..! Mwisho wa ubaya ni aibu
 
Mwanzo baada ya serikali kuacha kutoa takwimu tuliambiwa tutatengwa hadi na majirani ila naona lilipita hilo,sasa hivi limekuja la chanjo hebu tuone nalo litaishiaje.
Wewe unafikiri kupigwa ban kuingia nchi za ulaya sio mwanzo wa kutengwa.
 
Naina muda wa kulazimishwa unakaribia pamoja na kuonyesha tuna msimamo, tena siyo msimamo wa wananchi bali wa baadhi ya watu.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao, Mkuu wa shirika la afya kanda ya Afrika WHO Dkt. Matshdiso Moeti amesema kuwa Tanzania inatakiwa kutumia mwanya wa upatikanaji wa chanjo kwa faida ya wananchi wake na kanda ya Afrika mashariki kwa ujumla.

''Tumeanza kuwasiliana upya na ngazi za juu za uongozi, na tunatoa mchango wetu kama ilivyokua hapo mwanzo, na tunataka kushirikiana na Tanzania, kwa niaba ya watu wa Tanzania, nchi jirani na dunia kwa ujumla.

Sehemu ya mawasiliano yetu na Tanzania ni kukumbusha serikali kuwa, hii ni sehemu ya makubaliano ya kanuni za afya za kimataifa ambapo nchi wanachama wamekubali kwa pamoja kuzuia kusambaa kwa magonjwa'' anasema Dkt. Moeti.

WHO inasema kuwa imekua ikitoa mchango na kuwasiliana na serikali ya Tanzania kuanzia mwanzo wa janga hili la Corona.
Shirika hilo pia limesisita Tanzania kutoa takwimu za mwenendo wa Corona nchini Tanzania ili iwe rahisi katika kupambana na kuzuia maambukizi mapya.

''Moja ya makubaliano ya wanachama ni kutoa takwimu za mwenendo wa ugonjwa, nimewakumbusha serikali ya Tanzania na ninayo kumbukumbu kwa maandishi kuwa wao ni sehemu ya wanachama hivyo wanatakiwa kuitikia wito huu. Tuna imani kuwa mawasiliano yetu kuhusu chanjo yatazingatiwa ili kukabili maambukizi ya virusi," ameongezea Dkt. Moeti.

source: bbc
 
Nimekagua maktaba ya Taifa kuona kama kuna Rais yeyote wa Afrika aliyewahi kupambana na the so called mabeberu akashinda. Aibu inamnyemelea Jiwe.
Mtu kama wewe ungekuwepo kizazi cha Nyerere naona ungeenda kutoa hata niniliu kwa wazungu ili uwe upande wao.
 
Sijaelewa kwanini waafrika wengi wanaigomea hii chanjo. Kuanzia wa huko mbele mpaka sisi huku Afrika.
Mbona tuna chanjo nyingi ambazo wametuletea mabeberu kuanzia zile za uchanga mpaka chanjo ya homa ya ini hakuna hata moja tunazotengeneza wenyewe.
 
Kuhusu Chanjo, ni kweli Tanzania sio kisiwa hivyo kwa niaba ya wananchi, serikali Ina wajibu wa kukubaliana na suala la Chanjo kwa raia wake.
Lakini suala la kutangaza taarifa sidhani Kama linaathiri mapambano dhida ya janga Hilo.
Ili upate chanjo ni lazima uwe na takwimu, idadi ya chupa za chanjo hazisafirishwi kama mananasi ya Chalinze mnaishia kuyatupa nusu na kula nusu!
Tufunge mipaka tuone wataingilia wapi na makorona yao, wameona utajiri wetu wanataka watuue wote ili warithi mali.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mwisho wa siku hii chanjo tutapewa bure huku wengine wakiinunua kwa gharama mara mbili!

Saa nyingine mikwara ya JPM inasaidia sana.
Hee kumbe mikwara yote ni kwa sababu serikali haina pesa? Sasa huo utajiri wa tanzania anaopigia kelele kila siku upo kwenye nini?
 
Sijaelewa kwanini waafrika wengi wanaigomea hii chanjo. Kuanzia wa huko mbele mpaka sisi huku Afrika.
Mbona tuna chanjo nyingi ambazo wametuletea mabeberu kuanzia zile za uchanga mpaka chanjo ya homa ya ini hakuna hata moja tunazotengeneza wenyewe.
Ninachofurahi ni kwamba dunia sasa imeanza kuamka na kugundua janja janja ya wazungu
 
mkuu wewe uko kama wafuasi wa Kibwetele walioamriwa kuvua barakoa huko Moshi au uko tofauti ?
Bwashee kwa sasa kuvaa au kutovaa barakoa ni hiyari ya mtu hakuna kulazimishana.

Pale muhimbili hauingii bila kuvaa barakoa, unaelewa maana yake?
 
Kuhusu watu walioenda nje wakachanjwa huko na kutuletea korona za ajabu ajabu ulimsikia akisema?au masikio yako yanachagua cha kusikia?
Nilimsikia,lakini dhamiri yake ilikuwa juu ya kupata chanjo ambazo hazijathibitishwa au kufanyiwa upembuzi yakinifu na wizara yetu.

Ndo maana kaitaka wizara ya afya kuwa makini dhidi ya chanjo

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Siku moja baada ya Rais wa Tanzania, John Magufuli kutaka wizara ya afya kutokukimbilia chanjo ya Corona, Shirika la Afya Duniani WHO imeitaka nchi hiyo kujiandaa na chanjo ya Corona kama mataifa mengine duniani.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao, mkuu wa WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshdiso Moeti amesema kuwa Tanzania inatakiwa kutumia mwanya wa upatikanaji wa chanjo kwa faida ya wananchi na kanda ya Afrika Mashariki kwa ujumla.

''Tumeanza kuwasiliana upya na ngazi za juu za uongozi, na tunatoa mchango wetu kama ilivyokua hapo mwanzo, na tunataka kushirikiana na Tanzania, kwa niaba ya watu wa Tanzania, nchi jirani na dunia kwa ujumla. Sehemu ya mawasiliano yetu na Tanzania ni kukumbusha serikali kuwa, hii ni sehemu ya makubaliano ya kanuni za afya za kimataifa ambapo nchi wanachama wamekubali kwa pamoja kuzuia kusambaa kwa magonjwa'' anasema Dkt. Moeti.

WHO inasema kuwa imekua ikitoa mchango na kuwasiliana na serikali ya Tanzania kuanzia mwanzo wa janga hili la Corona.
Shirika hilo pia limesisita Tanzania kutoa takwimu za mwenendo wa Corona nchini Tanzania ili iwe rahisi katika kupambana na kuzuia maambukizi mapya.

Naye katibu mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Tedros Ghebreyesus anasema anaunga mkono alichosema @MoetiTshidi, anatoa rai hatua dhabiti za kiafya kukabiliana dhidi ya corona zinapaswa kufuatwa na kujiandaa kupokea chanjo.

Takwimu ni suala la muhimu pia kwa Tanzania kuzitoa, tena baada ya kesi za miongoni mwa wasafiri na wageni katika miezi ya hivi karibuni.

Chanzo: BBC SWAHILI

Hii ni habari njema sana. Ile mijamaa ya chama fulani imechutama karibu yote kama mi nanihii.

Inasubiri amri tena tokea kwa master. Ikumbukwe inatakiwa kutotofautiana naye hata kwa kama.

Hiiii bagosha.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom