#COVID19 Shirika la Afya Duniani (WHO) laitaka Tanzania kujiandaa kupokea chanjo ya Corona

#COVID19 Shirika la Afya Duniani (WHO) laitaka Tanzania kujiandaa kupokea chanjo ya Corona

Serikali lazima ikubali kupokea chanjo na kama inakataa lazima kuwa na hoja za msingi sana za kushawishi kuwa sio chanjo bora au ina shida. lakini kuikataa tuu haitawezekana kwa sababu uchumi wetu na kila kitu kinategemea muingiliano wa watu ni lazima chanjo tukubali kwani hili ni jambo jema kwani tuna chanjo nyingi sana tumezikubali na zimeonesha ufanisi mkubwa.
We nakujuaga nafsi yako haiko CCM kitambo kwakua una akili sana.

Vipi wale MATAGA
 
Jana mzee alisema hataki hiyo chanjo. Sasa itakuwaje😲
 
Daaah mzee anatakiwa kuchukua maamuzi magumu
Hakuna cha maamuzi magumu. Hana namna. Alichozungumza kwenye ule mkutano ni furahisha genge tu. Chanjo itakuja Tanzania kwa ajili wanaohitaji. Hama huhitaji siyo lazima. Hata nchi za Ulaya kuchanja siyo lazima.
 
Hakuna cha maamuzi magumu. Hana namna. Alichozungumza kwenye ule mkutano ni furahisha genge tu. Chanjo itakuja Tanzania kwa ajili wanaohitaji. Hama huhitaji siyo lazima. Hata nchi za Ulaya kuchanja siyo lazima.
Hio chanjo sionji hata tone
 
Serikali lazima ikubali kupokea chanjo na kama inakataa lazima kuwa na hoja za msingi sana za kushawishi kuwa sio chanjo bora au ina shida.
Kwani kuna ugumu gani kuikataa hiyo chanjo "kwa sababu za msingi" kama zile tulizotumia kuachana na kupima na kutangaza maambukizi?

Safari hii tutachanja mapapai, nyanya, kondoo, n.k., na kuzifanyia vipimo kuonyesha kwamba chanjo hazifanyi kazi!
Tuna 'Mwanasayansi' mwenye PhD pale juu,; tutashindwa kitu gani?
 
Tunatambua taasisi ya urais ina kila taarifa muhimu juu ya suala zima la matumizi ya chanjo ya COVID-19. Pengine hii ndiyo ikawa sababu ya Rais wetu kutilia mashaka juu ya uharaka wa mchakato wa kuanza kuwachanja raia zake.

Mimi nafikiri kujenga mashaka juu ya uharaka huu si kitu kibaya, lkn kutoa kauli zenye kuonyesha msimamo wa serikali majukwaani mbele ya vyombo vya habari, ni jambo ambalo linapaswa kuepukwa. Kwa kuwa kama nchi tulikwisha ridhia masuala ya afya ya kimataifa, eneo hili linapaswa kufanyiwa kazi na kutolewa na wataalamu wetu wa afya na wala si wanasiasa.

Uzoefu unatuonyesha mwishoni na mwanzoni mwa miaka ya 1970s & 1980s, aliyekuwa Rais wetu Mwl Nyerere wakati huo alikwaruzana mara kwa mara na mashirika ya fedha ya kimataifa ya fedha na hata wataalamu wa ndani kutokana na misimamo na mawazo yake binafsi. Alipinga kila "expert opinions" zilizotolewa ili kusimamia mageuzi ya sera za fedha na kiuchumi hapa nchini Tanzania. Kilichotokea kila mtu anakitambua kupitia historia.

Tunatambua Rais ana taarifa, hisia, misimamo na hata uelewa wake binafsi juu ya suala zima la COVID-19 hapa nchini. Lakini anapaswa kulishugulikia kitaasisi zaidi kuliko ilivyokuwa sasa ambapo inaonekana yupo kibinafsi zaidi. Masuala nyeti ya afya aiache Wizara ya Afya ndiyo ibebe jukumu nyeti la kukabiliana na gonjwa hili nyeti.

Mbele ya jicho la kimataifa na mikataba ya kimataifa ambayo nchi yetu imeridhia, inakuwa ni kichekesho kukwepa kuwajibika eti kwa kisingizio cha sisi kama taifa tupo salama zaidi kuwa tunategemea maombi na kupiga nyungu. Hata kama tunaona ni muhimu mno hapa nchini tuliweke tu kama "peripheral tool"
 
Kuhusu Chanjo, ni kweli Tanzania sio kisiwa hivyo kwa niaba ya wananchi, serikali Ina wajibu wa kukubaliana na suala la Chanjo kwa raia wake.
Lakini suala la kutangaza taarifa sidhani Kama linaathiri mapambano dhida ya janga Hilo.
Naamini kutangaza Ni njia namba moja ya kupambana na Covid kwasababu watu wakiujua ukweli wataongeza tahadhari tofauti na ulivyo watu wanapuuzia wakiamini hakuna wakati watu wanaondoka kimya Kimya
 
Hapo mke anapomgomea bwana ake kulala kibra [emoji23][emoji23][emoji23]

Wakati aliapa kwa shida na raha....,na Raha za misaada kwakua hatuwezi kujitegemea tujaendeshea ving'ora kila siku
Dadek.. Ndio maana kina Lisu wameona bora wahamie huko huko kabisa.
 
Hivi miaka mitano ya uongozi wa magu ameweza kutransform vipi huo utajiri wa nchi hii ureflect kwenye maisha ya wadanganyika wanaoishi kwa kipato cha chini ya dolla moja kwa siku.au kazi yakeni kupiga makelele tu
unatumiwa na mabeberu wewe
 
Back
Top Bottom