#COVID19 Shirika la Afya Duniani (WHO) laitaka Tanzania kujiandaa kupokea chanjo ya Corona

#COVID19 Shirika la Afya Duniani (WHO) laitaka Tanzania kujiandaa kupokea chanjo ya Corona

Gia kivipi?

Kwani wao wanaposema tujiandae, tujiandae vipi wakati hatujaagiza dawa?
Si watatuletea bure?
Msimamo wa nchi kupitia magufuli ni kwamba chanjo hazifai na hatuzitaki hata bure.
 
Kwa hivyo tutachanjwa kwa lazima whether we like it or not!

Mimi nasimama na Jiwe hachanjwi mtu hapa hahaa!
Ni sawa na ndivyo inavyotakiwa. Hata huko wanakotoa chanjo sasa hivi hakuna anayelazimishwa.

Wewe na Rais Magufuli mna uhuru wa kukataa au kukubali chanjo. Mimi binafsi chanjo ikija hapa kwetu nitakubali kuchanjwa. Kinachotakiwa kwa serikali ni kuwapa wananchi uhuru wa kuamua kuchanjwa ama la. Sio mtu mmoja aamua hatma ya maisha ya kila mtanzania kitu amabacho si sawa.
 
Serikali lazima ikubali kupokea chanjo na kama inakataa lazima kuwa na hoja za msingi sana za kushawishi kuwa sio chanjo bora au ina shida. Lakini kuikataa tuu haitawezekana kwa sababu uchumi wetu na kila kitu kinategemea muingiliano wa watu ni lazima chanjo tukubali kwani hili ni jambo jema kwani tuna chanjo nyingi sana tumezikubali na zimeonesha ufanisi mkubwa. Serikali kukataa chanjo ni kuua watu wasio na hatia.

Tumesaini mikataba mingi ya kimataifa lazima tukubali chanjo hii.
Swala la chanjo ni lazima.

Walevi wa madaraka hawajui hilo, wakiona wanaweza kuchezea sheria na mifumo yote ya nchi, hujisahau na kudhani kuwa wanaweza kufanya watakavyo kinyume na makubaliano ya kimataifa.
 
Hatupokei chanjo za kuletewa, watusubiri tutengeneze zetu na wao wawe tayari kuzipokea! Wapuuzi sana hawa! Kwetu tatizo siyo corona sisi tunataka chanjo ya malaria, kifua kikuu, ukimwi, kisonono, gonora, pressure, na kansa!

Hiyo covid-19 wapambane nayo wenyewe, siye huku Mungu ameshatuchanja! Huo ujuha wapeane wenyewe! Tanzania tutasimama kwa neema ya Mungu!

Amemka ww, majuha wameisha ww bado unalazimisha wawepo.
 
Msimamo wa nchi kupitia magufuli ni kwamba chanjo hazifai na hatuzitaki hata bure.
Ndiyo sasa wao wanatulazimishaje?

Ndio maana nasema mwisho wa siku watatubembeleza alafu wataleta chanjo bure.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mwisho wa siku hii chanjo tutapewa bure huku wengine wakiinunua kwa gharama mara mbili!

Saa nyingine mikwara ya JPM inasaidia sana.
Umeona anaelekea kushindwa Mungu wako,unaanza kutengeneza mazingira.
Umeambiwa chanjo hiyo itauzwa?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mwisho wa siku hii chanjo tutapewa bure huku wengine wakiinunua kwa gharama mara mbili!

Saa nyingine mikwara ya JPM inasaidia sana.
Wewe nawe unaishi Ulimwengu gani! Naona kama hujitambui na hujui chochote.

Ni chanjo gani, Tanzania inalipia? Wanachi wa mataifa tajiri ndio hulipia chanjo. Lakini mataifa yote maskini hupewa chanjo bure, na pia hupewa baadhi ya ambazo ni aghali za kutibu magonjwa hatarishi bure.

Tanzania ipo katika kundi la nchi maskini, hivyo ina-qualify kupewa chanjo zote bure. Wewe huwa unadanganyika na ule uwongo wa Jiwe kuwa nchi hii ni tajiri?

Bajeti ya Tanzania ni ndogo kiliko bajeti ya jiji la Lagos. Na mapato ya Tanzania kwa mwaka ni chini kuliko mapato ya bandari moja kati ya bandari 400 ndogo za US.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani umekatazwa kuchanjwa? Hata sasa hivi nenda Marekani ama nchi wanazotoa chanjo ukachanje mkuu! Hiari yako! Pia kumbuka hata sasa hivi kuna chanjo nyingi tu watu duniani wanachanja lakini hawalazimishwi.
Kwa nini niende Marekani? Gharama za kwenda huko utalipa wewe?

Una maana watanzania wote wanaotaka kuchanjwa hawana haki ya kupata huduma hiyo ndani ya nchi yao?

Ninachotaka ni uhuru wa kuchagua ndani ya nchi yangu.
 
Hatuangalii historia we mtu mwetu mweusi. Huyuu ndo atakuwa wa kwanza kushinda hao waume zako beberuru..alaf kizaz chako cha vilaza ndo kitaanza kutambua kuwa kuna rais wa africa aliewah kuahinda beberu.
Jiwe ni Rais wa kiwango cha chini kuliko yeyote ambaye tuliwahi kumpata. Haielewi Dunia, haujui uchumi wala hekima ya uongozi. Ndiye ufikirie wa kuwashinda mabeberu? Mabeberu huwezi kuwashinda kwa porojo unazowapa wananzengo bali kwa mipango thabiti inayozingatia weledi wa kutosha kuhusu maendeleo ya Dunia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe nawe unaishi Ulimwengu gani! Naona kama hujitambui na hujui chochote.

Ni chanjo gani, Tanzania inalipia? Wanachi wa mataifa tajiri ndio hulipia chanjo. Lakini mataifa yote maskini hupewa chanjo bure, na pia hupewa baadhi ya ambazo ni aghali za kutibu magonjwa hatarishi bure.

Tanzania ipo katika kundi la nchi maskini, hivyo ina-qualify kupewa chanjo zote bure. Wewe huwa unadanganyika na ule uwongo wa Jiwe kuwa nchi hii ni tajiri?

Bajeti ya Tanzania ni ndogo kiliko bajeti ya jiji la Lagos. Na mapato ya Tanzania kwa mwaka ni chini kuliko mapato ya bandari moja kati ya bandari 400 ndogo za US.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpumbavu sana wewe!

Chanjo ya corona inatolewa bure? Kenya tu hapo wameagiza dozi milioni 20, haya Kenya ni nchi tajiri?

Afrika Kusini wamenunua hii chanjo kwa bei mara mbiri ya bei sokoni sasa wewe unaongelea chanjo ipi inatolewa bure?

Mnajidharau na kuwaabudu sana wazungu sijui mmejaza takataka gani vichwani mwenu?
 
Mpaka kitaeleweka tu. Meko kama kawaida aliropoka tu bila kujua kwamba anabanwa na makubaliano ya Kiafya ya WHO.
Magufuli sio WHO,yeye kasema kwa maoni yake binafsi,na sifikiri kama ni msimamo wa serikali.
Sema swala hilo liachiwe wataalamu wa afya,Magu sio daktari wa watu,wanyama au mimea.
 
Mpaka kitaeleweka tu. Meko kama kawaida aliropoka tu bila kujua kwamba anabanwa na makubaliano ya Kiafya ya WHO.
Ikiwa hatuna imani na hiyo chanjo tuipokee tu na tuchanjwe kwa kuwa tuna mkataba na who?

Sisi wenyewe tumo kwenye tafiti kwaajili ya chanjo yetu na kama hawataki tuwe na mtazamo wetu basi dunia ikubaliane chanjo ya aina moja itumike kwa dunia nzima Otherwise hatupangiwi maisha wapeleke iyo chanjo kwanza china kwa kuwa wote ni binadamu na wanaishi kwenye dunia hiihii sisi afrika hatujapata madhara pakubwa kama wao waanzie huko kote
 
Thanks
Mtu kama wewe ungekuwepo kizazi cha Nyerere naona ungeenda kutoa hata niniliu kwa wazungu ili uwe upande wao.
Nyerere alikua Ana akili ndugu,tumechanjwa enzi za Nyerere chanjo za polio, ndui na magonjwa mengine.

Kiambie kimungu chako kikatae changing hii uone jinsi kitakavyo tengwa Hadi na mke wake.

Suala la afya ni la kidunia wewe kichwa sambusa.
 
ni kukumbusha serikali kuwa, hii ni sehemu ya makubaliano ya kanuni za afya za kimataifa ambapo nchi wanachama wamekubali kwa pamoja kuzuia kusambaa kwa magonjwa''
Mwenye masikio na asikie, wanaompuuza Rais waendelee kumpuuza na kumkebei ila ipo siku watakuja kuelewa.
NB. Mdudu yupo tuchukue tahadhari.
 
Naona afadhali tupewe chanjo za nchi za mashariki kama urusi, chanjo za nchi za magharibi siyo. Sijawahi kuwa amini sana wazungu wa magharibi.
 
Tanzania hakuna chanjo mpaka sasa! Subiri WHO wakileta za bure ukachanje ila kama unapesa zako nenda USA au Ulaya ukawahi chanjo usije ukafa na Covid-19
Hilo linajulikana na itachukua muda kufika kwetu. Hata kama una hela ukaenda Marekani leo sidhani kama utafanikiwa kuchanjwa kwani priority ni raia wao na sasa hivi wanaochanjwa ni wazee na medical personnel tu.

Ila tunapokwenda nadhani hizi chanjo zitakuwa available either za bure au za kulipia kama ilivyo kwa huduma nyingine za afya. Kinachotakiwa ni serikali kufacilitate....Na mtu mmoja mmoja atafanya maamuzi binafsi.
 
Back
Top Bottom