#COVID19 Shirika la Afya Duniani (WHO) laitaka Tanzania kujiandaa kupokea chanjo ya Corona

Thanks
Nyerere alikua Ana akili ndugu,tumechanjwa enzi za Nyerere chanjo za polio,ndui na magonjwa mengine.
Kiambie kimungu chako kikatae changing hii uone jinsi kitakavyo tengwa Hadi na mke wake.
Suala la afya Ni la kidunia wewe kichwa sambusa.
Ndio maana mnakuwa wapumbavu sana!

Kwa sababu miafrika kama nyie hata akija mtu akisema tufanye hili na lile ili tutoke kwenye makucha ya mzungu mtakuja na kusema hoo unataka tutengwe

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mtataliwa hadi mwisho wa dunia
 
Naona afadhali tupewe chanjo za nchi za mashariki kama urusi, chanjo za nchi za magharibi siyo. Sijawahi kuwa amini sana wazungu wa magharibi.
Kwani chanjo zote tunazotumia toka enzi na enzi huwa zinatoka nchi za mashariki au magharibi tuanzie hapo.
 
Pole sana. Mpaka umri huo, bado hujui kuwa nchi maskini kama Tanzania, miaka yote hatununui chanjo? Mama yako aliwahi kukueleza kuwa alilipa chanjo yako ya polio, surua, kifaduro au pepopunda?

Chini ya makubaliano ya kimataifa, we maskini ambaye unatoka katika nchi ambayo wastani wa kipato ni chini ya dola 1 kwa siku, unapewa bure. Wanalipa wenye pesa. Kwa akili yako, serikali hii ya Jiwe inaweza kutoa dola 200 ya chanjo kwa kwaajili ya kila mtanzania?

$200 × 60,000,000 = 12,000,000,000.

Hata ile ya kupambana na Covid 19, dola 3m, alikopa. Baadaye tukaonewa huruma, tukachangiwa changiwa zikafika karibia $50m. Jiwe kuona zipo nyingi akazipeleka kugharamia uchaguzi, halafu akajigamba, "kwa mara ya kwanza tumefanya uchaguzi kwa kugharamia wenyewe", wajinga wengi wakashangilia!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Endeleeni kuzunguka zunguka mtasema tu muda ukifika .[emoji23][emoji23]
 
Ndiyo sasa wao wanatulazimishaje?

Ndio maana nasema mwisho wa siku watatubembeleza alafu wataleta chanjo bure
Kwahiyo mnataka kubembelezwa ndio mtazipokea na kuzitumia?
 
Huna imani na hiyo chanjo kwa vigezi vipi? kwa study zipi? WHO lazima watamuuliza waziri wa afya ni kwanini wana kataa chanjo na lazima atoe majibu ya kisayansi sio hapa tuu bila sababu.

Lazima WHO wapewe sababu za msingi kinyume na hapo ni lazima tanzania ipokee chanjo hiyo, au kama Tanzania imetengeneza chanjo yake itatakiwa kuweka wazi kabisa ili chanjo hiyo itazamwe na kupimwa. Chanjo ni lazima tuipokee.
 

Usanii mwanzo mwisho, eti Serikali ya Tanzania ikubali tu kupokea chanjo, hasa eti tukiwekea maanani wasafiri wawili wa Tanzania kugundurika wana virus variant ya kovid kutoka Africa kusini - yaani wanatufanya Wantanzania hatuna akili za kugunduwa kinacho endelea nyuma ya pazia, kwa nini wanatumia kigezo cha abiria wawili kutoka Tanzania kiwe kama ni shinikizo la kutaka kulazimisha Serikali yetu kununua chanjo ambazo zina walakini sana ie hazijafanyiwa majaribio ya muda mrefu kujuwa madhara yake, kwa nini baadhi ya watu walio chanjwa na chanjo za Oxford na washitika wake walikuja kukutwa wameambukizwa virusi vya ukimwi, wengine walipooza, wengine wakapata ugonjwa wa kifafa - madhara hayo hawataki yajulikane.

Big Pharma Companies zinazo fadhiliwa na Bill Gates na Mkewe ndio wamepania kulazimisha Dunia ikubali kununua chanjo na madawa yao kwa bei mbaya, wanatumia vyombo vya habari vya magharibi kulaghai Dunia eti chanjo/madawa yao ni effective by 95.5% huku wakijuwa wazi wazi hiyo si kweli hata kidogo - hata madaktari walio kuwa wanamtibu Rais Donald Trump walikataa kutumia dawa/chanjo zinazo zalishwa na makampuni yenye tantacles za Bill Gates na genge lake.

Serikali yetu ikumbuke kwamba Bill Gates ana influence kubwa ndani ya moja wapo ya taasisi za Umoja wa Mataifa ie W.H.O, anatumia taasisi hiyo kutimiza ajenda zake za siri, sisemi WHO ni sehemu ya njama za William Gates na genge lake, far from it - wao wanatumiwa tu, kutokana na aidha kutojijuwa au wanakuwa funika kombe mwanaharamu apite, narudia kusema kwamba akili zote za Mr.Gates zipo kwenye njama za ku-depopulate third World Nations and he means it, come rain come shine lengo lake lazima litatekelezwa unless third World leaders waki-team up na kukataa chanjo zinazo zalishwa na Makampuni yanayo fadhiliwa na mfuko wa Bill Gates na mkewe, tutakuwa salama tukitumia chanjo zinazo zalishwa Uchina na Urusi hao hawana ajenda zozote za siri kuhusu population ya bara la Africa - my opinion.

Msifikiri namsingizia William Gates kwa conspiracy theories - no Sir, ukweli wa mambo ni kwamba jamaa huyu amepania kweli kweli ku-depopulate binadamu wa Dunia ya tatu kwa kupitia chanjo zake - fatilieni kwa karibu historia yake pamoja na imani yake linapokuja suala la wakazi wa Dunia ya tatu kuzaliana kwa wingi - suala hilo linamkera sana msije mkadangajwa na Ucheshi wake hasa akiwa mbele ya Public, kumbe kilichopo under the hood ni kitu tofauti kabisa.

Nimalizie kwa kuonya tena kwamba WHO ku-declare kwamba virusi vya COVID-19 ni pandemic kulimfurahisha Bill Gates maana anajua kwamba hivi sasa Dunia haina ujanja tena kila binadamu Duniani atalazimika kudungwa sindano za chanjo, wanasayansi wanao msikiliza Gates watatengeneza batch aina mbili za chanjo batch ya kwanza itatumika katika Mataifa ya Ulaya na Merikani, batch ya pili itakuwa ni ile ile lakini itaongezewa ingredients/customised kwa lengo la kudhuru Africans and Asians specifically Africans, tukichanjwa tutajikuta tunakumbwa na magonjwa ya kutumaliza taratibu mmoja baada ya mwingine pamoja na kuwafanya wasichana/wanawake wawe wagumba - njama za Bill Gates za kupitia njia ya chanjo ni za muda mrefu sana, pandemic hii ndio inempatia a golden chance ya kutekeleza malengo yake bila ya WHO na baadhi ya Viongozi wa Kiafrika kumshtukia.
 
Wewe ni kapumbavu sana yani.

Nani kakwambia chanjo ya corona utapewa bure?

Ile chanjo Magufuli akiamua kuileta atatumia kodi yako wewe na bibi zako kule kijijini kuinunua. Kama unataka ya bure subiri 2030 mataifa tajiri yakishajichanja yote ndipo wewe utaanza kugawiwa bure!

Yani unafananisha chanjo za polio za enzi hizo na hii ya corona?

Kenya tu hapo wameagiza dozi milioni 20 na bado wamewekwa pending mpaka wenye hela ndefu ziwatoshe ndio na wao wapewe. Afrika kusini wameuziwa bei mara 2 au 3 ya bei halisi. Alafu wewe unaongelea bure?
 
Kwahiyo mnataka kubembelezwa ndio mtazipokea na kuzitumia?
Hujasikia mkuu who amesema anafanya mazunguzmzo na tz?

Au ulitaka na sisi tununue kwa bilion 6 badala ya 2 kama ilivyotkea kwa Afrika kusini?
 
Mwambie Meko atoe ushahidi wa kisayansi wa kutokuwa na imani sio maneno matupu,halafu atengenenze dawa ipelekwe WHO kuthibitishwa ili achanje Watanzania wasiendelee kufa.
 
Tupo pamoja na Magufuli hatutaki huo upumbavu wao wa chanjo za ajabu ajabu. Wajichanje wao huko, kama kuna Mtanzania anataka chanjo aende huko akachanjwe.
 
Lakini siyo lazima kila Mtanzania achanjwe. Chanjo hata leo hii zipo nyingi tu hapa TZ lakini hawalzkmishwi kuchanjwa. Juzi tu watu watz walikuwa wanachanjwa chanjo ya Homa ya Manjano lakini siyo lazima.
Uwe una fikiri nje ya box. kila chanjo ina masharti yake na mazingira yake na si kila chanjo ni lazima lakini kuna chanjo ni lazima hasa ya magonjwa kadhaa kama hii ya COVID 19.

Chanjo nyingine zina masharti ya umri fulani ndio maana kuna chanjo kama za polio, pepopunda n.k watu wengi tumechanjwa tukiwa wadogo hivyo unaweza ukadhani una survive tuu kumbe ulisha chanjwa ndio maana kuna magonjwa hupati. Hata hii ni lazima kulingana na hali ya dunia.

Tanzania inategemea watalii na inategemea watu wa mataifa mengine kiuchumi hivyo swala la chanjo ni lazima.
Tunataka hoja za kisayansi kukataa chanjo hizo
 
Mkuu nenda kachanjwe kama unataka
Your browser is not able to display this video.
 
Kwa hivyo tutachanjwa kwa lazima whether we like it or not!

Mimi nasimama na Jiwe hachanjwi mtu hapa hahaa!
Kaka, Mimi nakazia kabisa, sichanjwi, na sina mpango wa kuchanjwa hata Rais akibadirika.

Kwenye chanjo hiyo iko Siri kubwa, na tusije kuwa tunaoneshwa tu kwenye luninga wakichanjwa kumbe ni danganya toto tu, na Naamini, chanjo itakayotumika ulaya si itakayotumika Africa.
 
Kama kuna Mtanzania yeyeote hataki kama nchi tufanye chanjo kuna mawili.

1. Hawajui umuhimu wa chanjo
2. Ubinafsi, uligi wa kubiashana bila sababu, kujionyesha utofauti pasipo umihimu na kutafuta umashuhuri

Wanasiasa wengi siku hizi imekuwa sifa kuamini ujinga ili waafurahishe wale watu ambao hawawezi kuwapa elimu ya kujitambua
 
Kama korona haipo chanjo ni ya nini?

Pia kama Marekani imeshindwa kutengeneza chanjo ya HIV imewezaje kutengeneza ya Covid 19 kama siyo utapeli na uhuni wa akina Billgate.

Chanjo ipokelewe tu ila ikatupwe tu kwani kila chakula anachokuletea jirani yako lazima ule?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…