Shirika la umeme Zanzibar lagoma kuilipa TANESCO

Wacha kihereher deni la Taifa si lenu wenyewe
ZANZIBAR ilikua mwanachama wa EAC mulioivunja watanganyika jee sehemu ya ZANZIBAR baada kuvunjika jumuia mbnona hamjatupa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitu ambacho watu tunashindwa kufahamu ni kuwa kituo cha kufufua umeme cha bonde la Mtera ni mali ya SMZ. Ndio jeuri inatokana na ukweli huo.

Siku itakayokatwa umeme Zanzibar siku ya pili yake Muungano ni historia.
 
kama mmebanwa mnasubiri nini kuuvunja mpk mchukie watu wasokua na hatia? mnapambana na mashine kisa unyonyaji wa mwenye mashine?
 
Wacha kihereher deni la Taifa si lenu wenyewe
ZANZIBAR ilikua mwanachama wa EAC mulioivunja watanganyika jee sehemu ya ZANZIBAR baada kuvunjika jumuia mbnona hamjatupa
Wewe mtoto mdogo sana. Hivi hujui kwamba kwa miaka zaidi ya 10 SMZ ilikuwa haijwezi.
Muulize komandoo, muulize Basil Mramba, Muulize Rais Kikwete, muuliza Shamsa Vua n.k.

Kile kifaa cha umeme cha bilioni 5 si mlikaa miezi 3 baada ya Kikwete kuwaacha na mambo yenu.
Shamsa Vuai alikuja kuhemea , muulize. Mishahara ya SMZ ilitoka hazina Dar! Komandoo Salimin anajua vema

Hizi hadithi za bank kuu ni za kitoto sana. Leo ikipigwa hesabu kamili mtauza kisiwa.

Ni hivi bwana mdogo, bilioni 10 za umeme ni nyingi sana ZNZ huku bara ni kodi za TBL. Umeelewa?

Tunachokataa hapa ni SMZ kutumia umeme halafu kutaka mwananchi wa Nzasa alipe starehe zao.

Yapo ya kunyamaza hili la umeme ni fedheha sana. Yaani mwananchi wa Sinza anajua wajibu, SMZ haijui maana ya bill
 
Kitu ambacho watu tunashindwa kufahamu ni kuwa kituo cha kufufua umeme cha bonde la Mtera ni mali ya SMZ. Ndio jeuri inatokana na ukweli huo.Siku itakayokatwa umeme Zanzibar siku ya pili yake Muungano ni historia.
Walaa muungano haushikiliwi na umeme. Wazanzibar wakiondoka na kurejea kwao muungano umefikia mwisho.

Hakuna Mtanganyika atakayeathirika. Nusu ya Wazanzibar inaishi bara na ndilo eneo lililobeba wazanzibar wengi duniani.

Ni kuamua tu, pandeni boti, katazeni wabunge wenu wasije Dodoma, mwiteni VP arudi nyumbani.

Hakuna Mtanganyika atakayeshtuka znz kuondoka. Hawa wasioweza kulipa bilioni 10 wakiwa na SMZ! Teh teh , no way.
 
Kwanini wasiachiwe kabisa badala ya kufanywa mkoa? Huoni kama Tanganyika ndio inaihiyaji Zanzibar?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Rodiriki Alekizanda, hili jambo ni kweli kama ifuatavyo
  1. Ni kweli Tanesco inaidai Zeco deni kubwa la umeme la muda mrefu. Mwaka 2012 Tanesco ilisamehe deni la zaidi ya bilioni 50. Sababu ya deni hilo ni Zesco inauza umeme Zanzibar kwa bei ya chini kuliko bei ya Tanesco hivyo mapato yote ya umeme yanayokusanywa Zanzibar hayawezi kulipa bili ya Tanesco. Hivyo ni kama Tanzania tunawapa Zanzibar umeme bure.
  2. Magufuli alipoingia akaziamuru Taasisi zote za umma kulipa madeni yake ikiwemo maji na umeme na wasipolipa, wakaruhusiwa kukata huduma, hivyo Taasisi za bara zilikatiwa huduma za maji na umeme isipokiwa Ikulu, Tiss, Jeshi na Muhimbili.
  3. Magufuli akaamuru hata Ikulu ama ilipe au ikatiwe, Ikulu ikalipa, akairuhusu Tanesco ikate umeme Zanzibar.
  4. Dr. Shein akahutubia kuwa kama ni kukata umeme, wakate tuu, Zanzibar watatumia hata vibatari. Ndipo Tanesco wakazuiwa kukata umeme Zanzibar.
  5. Ni kweli kwenye mgawanyo wa pato la taifa, Zanzibar inastahili kupata 4.5% ya fedha zote za misaada kutoka nje, kitu ambacho ni kweli hakijafanyika, hivyo ni kweli SMZ inaidai Serikali ya JMT kiasi kikubwa cha fedha.
  6. Serikali ya JMT imegoma kuilipa Zanzibar fedha hizo kwasababu Zanzibar haichangii hata senti tano gharama za uendeshaji wa serikali ya muungano, wanaajiriwa bure, wanalipwa mishahara bure, gharama zote za kuiendesha serikali ya muungano zinabebwa na upande mmoja.
  7. Zanzibar imegoma kuchangia gharama za uendeshaji wa serikali ya muungano kwasababu mpaka sasa serikali ya JMT haijawahi kuainisha gharama za uendeshaji wa serikali ya muungano kwasababu serikali ya muungano ndio hiyo hiyo serikali ya Tanzania Bara.
  8. Mpaka leo serikali ya JMT imegoma kufungua Account ya pamoja ya kuendesha muungano, joint Account kwasababu the dividing line between Serikali ya Tanzania Bara na serikali ya JMT ni very thin.
  9. Hoja kuwa Zanzibar ilichangia hisa asilimia 11% uanzishwaji wa BOT ni uongo. Katika set up ya BOT ni mali ya JMT 100% bila mgawanyo wowote wa shares.
  10. Issue ya uchangiaji gharama za uendeshaji wa serikali ya muungano ni moja ya kero za muungano wetu tangu ulipoanza, Zanzibar ilichangia miaka michache ya mwanzo, Karume akauliza Tanganyika inachangia nini, haikuonekana mpaka wa serikali ya Tanganyika na serikali ya muungano, hivyo akaona ni ujinga, anaweza kuwa Zanzibar inachangia kuendesha serikali ya Tanganyika kwa jina la muungano. Akasimamisha kuchangia hadi mambo yarekebishwe. Akasema "muungano ni kama koti, ukiona linakubana, unaweza kulivua".
Hitimisho.
Suluhisho la kudumu la kero zote za muungano ni moja tuu, the one and only, serikali moja!. Tanzania inakuwa nchi moja chini ya rais mmoja na serikali moja yenye majimbo mawili, Bara na Zanzibar ambayo yataongozwa na ma gavana.
P
 
jamaa anakaza fuvu afu hana reasons za maana


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini wasiachiwe kabisa badala ya kufanywa mkoa? Huoni kama Tanganyika ndio inaihiyaji Zanzibar?

Sent using Jamii Forums mobile app
emu tumia akili watu milioni karibia 60 tutegemee watu hawafiki 3m na cha muhimu apo znz n nn yani tunganganie ungekuta hata watu wake n vichwa au wachapakazi sawa ila huku mtaa wa Zanzibar wapo wengi na ni mamwinyi tu hawajui hata kujishuhulisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda Zanzibar uwaeleze hayo wale Watanganyika kule kwamba warudi kwao kama hutorudi kwenye sanduku kwa hasira zao juu yako!
 
True, Zanzibar inadekezwa sanaa....Na hali ya kuwa na serikali yao inawapa kiburi

Jamuhuri ya Muungano iifute SMZ.....India upuuzi wa namna hii wameuhitimisha
 
Unadangaya mkuu, fafanua ni kwa namna gani wazanzibari wamebanwa na muungano, mbona hao wapemba ndio wamejaa huku bara wakifanya biashara zao??

Au wewe unatamaa tu ya madaraka hivyo unaona kama Muungano unakubana kudanganya wenzako??
 
Nenda Zanzibar uwaeleze hayo wale Watanganyika kule kwamba warudi kwao kama hutorudi kwenye sanduku kwa hasira zao juu yako!
Yes nao Watarudi tena wanatosha boti moja. Kazi ipo kwa Wazanzibar maana nusu wamekimbia wapo bara na ndilo eneo pekee duniani lenye Wznz wengi.

Ondokeni tu kwa amani, wale watanganyika nao tutawaambia warudi nyumbani .
 
Tanganyika ni nchi pekee yenye Koloni Africa.
 
Hawawezi kukiona cha mtema kuni,ninyi watanganyika ndiyo mnaifanya Zanzibar kuwa kisiwa masikini zaidi duniani,kwa Tanganyika kujifika koti la Muungano na kujifanya ninyi ndiyoTanzania .uliona wapi kisiwa kikawa masikini hadi kukosa umeme kama siyo koloni jeusi Tanganyika.
 
Yani tena inatakiwa tuwaomgeze na pesa juu.
Ila kiufupi watakatana huko huko juu kwa juu
 
Kujishukhulisha sio lazma kulima na kuranda na nyungo mitaani, au kufanya kazi nzito, Zanzibar ilikuwepo kabla ya muungano na ilikuwa na maendeleo makubwa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katiba inatamka kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanganyika.

Nikiwa Rais nitaibadili isomeke "Zanzibar na Pemba ni mikoa ya Tanganyika."

Kama ni urojo mtaruhusiwa kupika hizo rojo mahali popote. Lakini nchi hakika hamtapewa hata kwa dawa.
Mkoa ujulikane kwa jina la Zanzibar, then wilaya zake ziwe ni Unguja na Pemba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…