Shituka kijana, wewe sio benki kwenye mahusiano yako

Shituka kijana, wewe sio benki kwenye mahusiano yako

Kila mwanamke ana potential kwa mtu sahihi,si lazima akupee pesa,awe na akili ya maendeleo..ila anaweza kuwa potential tu kwa maumbile yake yakakupa nguvu ya kutafuta zaidi,sauti yake ikaleta amani ya moyo na ubongo hivyo itapelekea amani nafsini mwako hata kama hauna pesa,heshima yake kwa elimu ndogo aliyonayo hata kama hana elimu kubwa ikakupa nguvu ya kutafuta na kumuwezesha zaidi,

Tabasamu lake tu pale hata kama siku hiyo hujarudi na kitenge yake/hujamletea mascara,necklaces ukajihisi umefika kwa Mungu baba mbinguni umeketi na malaika wa pekee uliyekabidhiwa kwa ajili yako

.......Wait nipokee simu ya bibi ako na nafahamu hapa ataniambia "usisahau kusali hapo ulipo na mimi nakuombea afya njema"
Endelea kudanganywa na conspiracy za majangili😂🤣.

Msalimie bibi, Mwambie am also doing fine.
 
Kibuti ni uhakika kama tarehe ya kifo
Kuna jomba ali niagiza nimtagutie iphone 11 Dem wake 🤓.
Nika mpiga lecture, aka ishia ku block namba ya jini😂🤣.

Ila yupo mwingine asha pukutishwa, ni Kama kasha pigwa limbwata.
Kapeleka mayai 5 na chipsi yai, Dem kala kidogo aka mwambia jomba Eti acha nimpe mtoto wa jirani🤣🤣
 
Mwanangu natamani huu ujumbe angesoma mshikaji wangu mmoja kazama Kwa Dem mmoja hv aiseee mshikaji Hela zake zote kawekeza Kwa Dem Kila cku namwona anavyoporomokaa kiuchumi tu mpk wafanyakazi wake wameanzaa kumkimbia kisa hawalipi aiseeee mwanaaa alikuwa ana plan kibao na zote zilikuwa Kwenye njia inayoonekanaa ,ilaa ndio kashazamaa Kwa Dem kumtoa huko mmmmhhh n ngumu ,maana bhana mapenzi Huwa hayaingiliwi Wala ushauri ..
 
Kuna jomba ali niagiza nimtagutie iphone 11 Dem wake 🤓.
Nika mpiga lecture, aka ishia ku block namba ya jini😂🤣.

Ila yupo mwingine asha pukutishwa, ni Kama kasha pigwa limbwata.
Kapeleka mayai 5 na chipsi yai, Dem kala kidogo aka mwambia jomba Eti acha nimpe mtoto wa jirani🤣🤣
Behind every successful man…there is a woman. You know why? Well…that’s because women DON’T follow unsuccessful men.
Tafuta pesa mwenezi. Ukijipata unawapa kama sadaka tu
 
Vijana wengi wasio na wake wanapaswa kuwa na mafanikio zaidi kuliko walivyo sasa, Lakini kwa sababu wanatumia pesa nyingi kwa wanawake ambao sio wake zao, ndio maana hawafanikiwi.

Bro unajua mapenzi yanaweza kukurudisha nyuma kama usipoingia kwa akili?Ila mapenzi ni matamu sometimes lakini mpaka upendwe kwa dhati.

Unaamini demu wako anawezakuwa drawback yako katika maendeleo? Sa skia mwanangu, usiruhusu mwanamke akutengenezee failure.

Kuna maoni mengi potofu kuhusu pesa na mahusiano kwa baadhi yetu vijana.
Vijana tunapaswa kudhibiti uwezo wetu wa kutaka kuaminisha upendo kwa kuwapatia wanawake ambao sio wake zetu pesa.

Je, huna Mama, Baba, ndugu wanaohitaji?Hao ndio unapaswa kuwasaidia na sio mpenzi wako na familia yake. Hautasonga mbeleMungu hatakubariki kwa kile unachofanya.
Utabarikiwa na Mungu pale tu unapowasaidia wenye uhitaji, wazazi wako, mke wako na watoto wako.

Je, mpenzi wako ni mtu mwenye uhitaji maalum?Je, ulikutana nae kwenye nyumba ya watoto yatima?Ulikutana nae mitaani?Je, alikuwa akiishi vipi kabla ya kukutana nae?Nyote mnahitaji kuwa waangalifu juu ya jinsi mnavyojaribu ku'show love kwa mademu wenu.

You also have to know that women are more loyal to their feelings than your sacrifices.Ni bora mkewako akuulize kwamna"what have you ever done for me?"Kuliko akuulize dem hilo sio jukumu lako we sio baba yake. Wanawake wanapenda pesa, na ukitaka kuwapa kwa sana, hawata zikataa.

Lakini usifikiri kwamba matumizi yako juu yake, yatakuhakikishia chochote. Tumeona mara ngapi jinsi wanaume wanavyolipia ada mademu chuo, Na mwisho wake waliwaacha??Unatakiwa kumpa nini mpenzi wako?Zawadi za hapa na pale, kulipa bili unapoenda maeneo ya starehe, na mara chache unaweza kumsaidia kwa fedha kidogo pale tu inapohitajika.

Na hata sio inshu ya kufanya wiki chache baada ya kukutana nae. Lazima uchukue muda kumjua ni mtu wa aina gani.

Pesa yoyote unayotumia kwa demu sio investiment, haijalishi ni kidogo kiasi gani. So, fanya kidogo unachopaswa kufanya where necessary, Lakini usije kuingia kwenye deni kwa sababu yake.

Usikope pesa kwa sababu ya mpenzi wako.Usilipe ada zake Usimlipie kodi.Ngoja nikuambie.Unachodaiwa na mpenzi wako ni yeye kukuona ukiendelea.

Acha akuite bahili lakini akiona maendeleo unayo yapata katika maisha atalazimika kuendana na mifumo yako kwa sababu anajua unajenga maisha yajayo.Kama hataki kuwa na subira, mwache aende zake.

Yeye hatokulisha wewe.Wewe ndiye utamlisha.Kumpa pesa sana, unajiweka kwenye hali ya kushindwa kufanya maendeleo yako.
Hutakuwa na akiba na hutapata baraka zozote kutoka kwake Utakachopata ni usaliti, majuto na machozi.

Mnapopigiwa mademu hamuumii kisa kukaziwa, Mnaumizwa na pesa na muda mliopoteza kwa watu ambao sio sahihi.

I mean no malice to nobody!
View attachment 2928505
MKUU HII UMETOA TWITTER KWA MKUU PROSPER.......NIMEFURAHI UNAWASAMBAZIA MADINI MPAKA HUKU.....BIG UP BRO
 
Nawasikitikia sana vijana wanaojichanga halafu bado wanahudumia mademu. Kila wiki wanawatoa out na bado kuwanunulia vitu kede kede. Kuna strategy inabidi tuwapatie vijana.
 
Behind every successful man…there is a woman. You know why? Well…that’s because women DON’T follow unsuccessful men.
Tafuta pesa mwenezi. Ukijipata unawapa kama sadaka tu
Behind every successful man, Kuna hustles na sacrifice zake.

Hizo ulizo andika ni chai za majangili ya kike🤓😂🤣
 
Nawasikitikia sana vijana wanaojichanga halafu bado wanahudumia mademu. Kila wiki wanawatoa out na bado kuwanunulia vitu kede kede. Kuna strategy inabidi tuwapatie vijana.
Uko sahihi, Ina bidi washituke ili wakae kimasta.
 
MKUU NAKUONA NA KULE TWITTER KUNA BANDIKO HILI...🤣🤣🤣🤣 AU WW NDIO PROSPER MZEE WA KUTOA MADINI????
BIG UP
 
Back
Top Bottom