Shock: Hospitali ya Kairuki yakataa wagonjwa wa ugonjwa wa mifumo ya hewa kijanja, yaweka bei isiyowezekanika kwa Watanzania wengi

Shock: Hospitali ya Kairuki yakataa wagonjwa wa ugonjwa wa mifumo ya hewa kijanja, yaweka bei isiyowezekanika kwa Watanzania wengi

Vipi hakuna kodi zimeongezeka huko? Risks za wagonjwa wenye shida ya upumuaji waielewa? Gharama za ku operate hizo ventilator halafu idadi kubwa ya wagonjwa wasipone na waliobaki washindwe kulipa gharama likoje?.
 
Mzee wako atakapotaka hiyo huduma ndio utaelewa ndugu yako anatakaje?
Hakuna kitu cha bure duniani. Kuna mtu lazima alipie, unataka nani alipe?

Hata kama ni mzee wangu, nikishindwa kumlipia, atakufa... hatakuwa wa kwanza wala wa mwisho
 
Na hizo hospitali nazo zikipandisha bei na kuwa za kitalii wananchi watatibiwa wapi?
Wewe it seems una kipato, you don't care about others
Matibabu ya bei nafuu kadai huko unakolipa kodi aka serikalini, sio watu ambako wametoa jasho na mitaji yao kuwekeza.

Pambana na serikali, ndio chombo pekee una haki ya kukidai, sio hospitali ya mtu. Wewe mwenyewe unaweza kufanya kazi kwa kulazimishwa mshahara au kuuza vitu kwa kulazimishwa bei?
 
Hivi Mkurugenzi wa hiyo hospitali ni nani?

Hawa watakua ni wafanyabiashara tena wasiojua maana ya kuwa taasisi inayotoa huduma ya afya. Sijawahi kuona hospitali kukataa wagonjwa kwa sababu yoyote ile.

Halafu shida ya mfumo wa upumuaji sio lazima iwe corona, inaweza kuwa hata blood pressure au tatizo lingine
Na bado mwaka huu teh teh

Mbona hukuona serikali waliposema kupima korona ni 100usd?
 
Niko kwenye hilo hiti na mamyako.... na sijui mlikua mnaongea nini hadi akakuhadithia mambo ya wanawake? Mfyuuu

Kuna tofauti kati ya biashara ya kuuza beer na kutoa huduma ya afya. Kama hujui sheria na miongozo ya watoa huduma za afya usikurupuke, tulia weweeee

Wacha regulators waongee
Hao regulators waambie waangalie na gharama ya 100usd inayo tozwa na serikali ili kupima korona.
 
Hao regulators waambie waangalie na gharama ya 100usd inayo tozwa na serikali ili kupima korona.
Wakati watoa huduma wanasign kukubaliana na masharti hawakuyajua hayo? Kama hawakuyajua hawajui wanachokifanya
 
Kwa ni uende private na serikali sikivu imekujengea na kukusomeshea wataalam. Usilazimishe kula mkate wakati kuna ugali. Ni sawa kumpeleka mtoto IST huku kuna elimu bure.
Kulalamika kumekuwa hulka ya watu.
Ipo siku utauliza kwa nini chpsi mayai buku kwa mama ntilie na ni laki Palm hotel.
Hewa inauzwa siku hizi. Tupambane tu, maji yanauzwa kila kitu pesa
 
Wakati watoa huduma wanasign kukubaliana na masharti hawakuyajua hayo? Kama hawakuyajua hawajui wanachokifanya
SAWA WENYE UWEZO WA KU AFFORD NDIYO WATAENDA HUKO,WENZANGU NA MIE SISI TUTAENDA KWENYE HOSPITALI ZETU ZILE
AU TUKAZANE KUPIGA NYUNGU TU

ova
 
Tuake ndani tujifukize.. ukiona umezidiwa nenda Amana, Mwananyamala Muhimbili etc.. Msiwapangie kwani hawajawalizimisha kwenda
 
Korona ikishaingia kwenye mapafu Nyungu haisaidii.

Sasa Familia nzima ikichapwa na Korona halafu muwe na shida ya Oxygen muambiwe huduma ni laki nane na nusu per day kwa mtu mmoja na huduma inachukua wiki nzima.

Yaani mnapoteza familia hivihivi huku mnajiona!

Badala ya kuona hili jambo ni la kawaida (soko huria), Wafikirieni wenzenu ambao changamoto ya kupumua imeshika members wa familia let say watano kwa mkupuo!
 
Mkuu ata hosptal za serikali nadhani ata muhimbuli, bugando na nyingine ukiwa I.C.U na ukihitaji ventilator kwa siku ni laki 5 apo ni intensive care achilia mbali dawa na baadhi ya malipo menginena ni toka muda sio kwa kipindi hichi, kama nitakua nimekosea nirekebishwe na private nyingne kwa siku zinaenda hadi 1M
Na sio kama serikali haijui hizi gharama wanazijua halafu mishahara ipo pale pale,
 
Hapo saini umeiona wapi kwenye tangazo?
Wee nawe unashindwa nini kuelewa hapo? Hiyo ni fomu ya mkataba ambayo mlipaji au mdhamini wa mgonjwa anatakiwa kuijaza kabla ya huduma ya matibabu haijaanza na itasainiwa na huyo mdhamini au mlipaji wa gharama za matibabu na pia shahidi wa hospitali.
 
Back
Top Bottom