Shukrani kwa Jamii Forums kwa kunipa Tuzo ๐Ÿ™๐Ÿฝ

Naunga mkono hoja kuna haja ya serikali kulifanyia kazi hili, watu wa makundi maalum wanateseka sana kwenye jamii kuna makundi mengine hayaguswi kabisa kwa kupata huduma.
.
Nami naunga mkono hoja hii,Waziri itisha kikao humu jf,wakupe mapendekezo jinsi Gani nasi wadau twaweza kuchangia chochote kitu,wakupe mawazo Yao.

Binafsi nikupongeze Kwa Kuwa karibu na jamii,usiwe Kama huyu๐Ÿ‘‡
 
Mimi pia nakupongeza sana kwa kutwaa tuzo hii kutoka jamii forum,uwezi kupewa tuzo kama hakuna ambacho umeifanyia jamii inayokuzunguka

Ina maana kuna jambo ulilifanya hapo before shukrani ziende kwa Maxence Melo
 
Tunafanyia kazi. Mafundisho yake hakika yanapotosha ajenda nzuri ya maendeleo ya usawa wa kijinsia. Haiko hivyo anavyofundisha.
 
NATAMANI UNGEPATA JUKUMU KUBWA NNCHI HII WATANZANIA WANGEFURAHI,SANA LAKINI TUNAENDELEA NA MAOMBI JUU YAKO
 
Hongera sana mheshimiwa ila ningeshangaa nisingeona jina la Samia
Hujambo mwanangu? Ukweli utabaki hivi, yeye ndiye aliyeniteua tena kwenye Awamu yake ya uongozi na kunipa nafasi ya kutumika kwenye serikali yake hadi hapa nilipo sasa. Asingeniteua na kunipa nafasi kwenye serikali yake na kunipa haya majukumu, huenda nisingepata nafasi ya kutumikia jamii kwa hatua hii. Ni vema kuwa na mioyo ya shukrani siyo tu kwa Mwenyezi Mungu bali kwa Kila aliyekuamini na kukupa nafasi utumike hapo unapotumika. Ndiyo maana hata watoa hoja za humu jukwaani nimewashukuru pamoja na wewe ndugu yangu mwema๐Ÿ™๐Ÿฝ
 
Hongera Mh Waziri, Sijui kwanini hawakupi Wizara ya Afya uimarishe tiba na afya kwa Watanzania.
 
Tunafanyia kazi. Mafundisho yake hakika yanapotosha ajenda nzuri ya maendeleo ya usawa wa kijinsia. Haiko hivyo anavyofundisha.
Ahsante sana Mhe Wazir.
Nadhan kama alivyofanya Waziri wa Mambo ya Ndani kuwadhibiti Manabii Tapeli kina ZUMARIDI na KIBOKO YA WACHAWI. Vivyo hivyo Simama Imara kudhibiti Waendeshaji wa VIPINDI VYA LUNINGA, Mitandao ya Kijamii na Online TV hasa Akina MAUKI, MC, MAKUNGWI nk. Ambao kutwaaa kucha na kueneza chuki na mtanzuko wa Kijamii.
Ikiwezekana kama wanavyosajiliwa Waganga wa Kienyeji, Wachungaji nk. na wao wafuate mkondo huo.

Hawa akina Kajala, Wema, Kiria nk wanaoendesha Vipindi mbalimbali vya masuala ya Kijamii maudhui yao yadhibitiwe na Wizara yako kabla ya Vipindi kwenda hewani ikiwa ni pamoja na kupewa semina. Kuna jambo hapa limeachwa bila udhibiti TCRA Peke yao hawatoshi Mhe. Waziri fanya jambo.
 
Hongera sana Mheshimiwa Waziri. Ama hakika ulistahili kupata hii tuzo
 
Salaam. Ahsante kwa maoni.

Naomba awali nikupe ufafanuzi kidogo kuhusu mfumo na utaratibu Ili tushirikiane vema zaidi: ni kwamba; wizara zenye dhamana ya sheria ya kudhibiti wote hao uliowataja ni pamoja na wizara ya mawasiliano, habari na Teknolojia ya habari na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kinachofanyika ni hivi, Mimi na wewe tunatoa malalamiko wizara ya mambo ya ndani kuhusu jinsi gani wenzetu hao wanachangia mmomonyoko wa maadili kisha, wizara ya mambo ya ndani huchunguza na wakiona Wana kesi ya kujibu, ndiyo Sheria za wizara husika hufanya kazi kupitia mahakama.

Njia ingine ni Wizara zenye dhamana na Sheria husika kuwaita kwa hatua kabla ya utaratibu wa kwenda mahakamani.

Hivyo, kwa upande wa wizara hii ya maendeleo ya jamii, tumekuwa tukiripoti mambo mengi yakiwemo hata hayo ya zumaridi, kiboko ya wachawi, Babu wa TikTok, na wale wachezeaji wa nyoka, nabii Tito nk. Hata Hawa nao uliowataja, kwa upande wetu tutawaripoti. Kifupi, hatuna sheria za moja kwa moja Bali za kisekta hivyo, tuendelee kushirikiana Ili turatibu kwa ajili ya sheria husika kufanya kazi chini ya wenye dhamana na Sheria hizo.

Ahsante
 
Kila la kheri katika kulitumikia Taifa
 
Hii tuzo unastahili, viongozi wengi hawapendi kukosolewa lakini watu watu wanapokukosoa au kutoa maoni umekuwa ukichukulia kama changamoto na kufanyia kazi.
Umeweka mfano kiasi viongozi wengine wataacha kuona mitandao ya jamii Kama adui
 
Hongera sana Dr wetu tuna tambua sana mchango wako ubarikiwe mno.


NB:Aliyekuvalisha Hilo wigi mtumbue hata kama jipu halijaiva.
 
.

Nami naunga mkono hoja hii,Waziri itisha kikao humu jf,wakupe mapendekezo jinsi Gani nasi wadau twaweza kuchangia chochote kitu,wakupe mawazo Yao.

Binafsi nikupongeze Kwa Kuwa karibu na jamii,usiwe Kama huyu๐Ÿ‘‡View attachment 3102981
Naunga mkono hoja yako mkuu, zipo taasisi nyingi binafsi zinazojihusisha na makundi hayo wajaribu kuzifikia ili ziweze kuwafikia watu wengi zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ