.Naunga mkono hoja kuna haja ya serikali kulifanyia kazi hili, watu wa makundi maalum wanateseka sana kwenye jamii kuna makundi mengine hayaguswi kabisa kwa kupata huduma.
Nami naunga mkono hoja hii,Waziri itisha kikao humu jf,wakupe mapendekezo jinsi Gani nasi wadau twaweza kuchangia chochote kitu,wakupe mawazo Yao.Dkt. Gwajima D ni ombi letu watanzania serikali iweze kuwalea walemavu nchini, hasa wenye ulemevu ambao hawawezi kujishugulisha na kazi za vipato including wenye matatizo ya akili. Huwa naumia sana nikiangalia kiwango cha kodi ninachotoa halafu nakutana na mlemavu hana hata miundombinu ya kumuwezesha kuishi anakuwa omba omba wakati serikali yao ipo. Yes tunajua pia kuna wajanja wanawatumia kwenye u omba omba lakini kuna sehemu kama taifa kupitia wizara yako serikali inaweza ikafanya kitu angalau hata community houses, matibabu, chakula na wanakuwa na uangalizi maalumu.
Binafsi nikupongeze Kwa Kuwa karibu na jamii,usiwe Kama huyu👇