Shukrani,Tahadhari na Rai yangu baada ya mchakato wa awali kura ya Maoni Rombo

Haaaa kashatoa tamko anasubiri maamuzi ya chama kuhusu kugonbea ubunge rombo zile ni kura za maoni tu.

So, anadhani kamanda Selasini atakatwa na wakuu na badala yake awekwe yeye? sidhani kama CHADEMA kuna upuuzi huo kama wafanyavyo CCM.
 
Ben is very smart..... kwa umri wake mfupi katika siasa za Tanzania unaweza kuona namna anavyojijenga bila papara.... very potential politician in near future..... chama mtengenezeni huyu..... msikwazwe na pressure ya kiu iliyo ndani yake.....taratibu tutafika.....
 
Sasa Ben kwanini hujawalalamikia moderators kukuwekea heading isiyoendana na uzi wako wa kushukuru?
 

Paragraph 1: Tafsiri yake ni kwamba umepata kura chache kwa sababu ulitumia fedha kidogo! Kwa maana nyingine unadai mwenzio alipata kura nyingi kwa sababu alitumia fedha nyingi.

Paragraph 2: Kama sijakosea rufaa itakuwa inatokana na maelezo yangu hapo juu! Tungoje matokeo lakini sioni dalili za wewe kupewa jimbo CDM, kamwe!
 
Kura si za siri! Sasa unajuaje kuwa ulipigiwa kura na flani? Au zilipigwa za wazi!
 
. Ben Saanane,

..kwa mtizamo wangu utakisaidia chama zaidi ukijikita ktk masuala ya UTAFITI na SERA.

..jaribu kukaa na wasomi kama Prof.Safari, Prof.Baregu, na wengine, kuwasaidia viongozi wakuu, pamoja na wabunge wetu.
 
Last edited by a moderator:
Ushauri wangu kwako ndugu yangu ben, watumikie wananchi wa rombo kupitia udiwani huku ukijijenga kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao, sio lazima kuwatumikia kupitia ubunge. Aluta continue

Wakati akijijenga kwenye udiwani. Selasini anazidi kujijenga kwenye ubunge..teh teh teh
 
Kweli. . .. .sijui system ya kukuza watu huko ndani ikoje. . . . . Na sioni akiwa anatumika katika maeneo ambayo angeweza kuwa na manufaa zaid kwa chama huku naye akikua. . . . . natamani angewekwa kurugenzi ya mafunzo anoe vijana. . . .Uwezo wa kujenga hoja na kujiamini nadhani huko angeweza kutumia uwezo wake vizuri sana naye angekomaa zaidi. . . .
 
. Ben Saanane,
..kwa mtizamo wangu utakisaidia chama zaidi ukijikita ktk masuala ya UTAFITI na SERA.
..jaribu kukaa na wasomi kama Prof.Safari, Prof.Baregu, na wengine, kuwasaidia viongozi wakuu, pamoja na wabunge wetu.

Kwani yeye anachagua pa kukaa au viongozi ndio wanatakiwa kuona uwezo wa vijana na CV zao ili wawapangie majukumu stahiki???!

Ukitoa siasa na utashi binafsi Ben Saanane sio mtu wa jukwaani, ukisoma hoja na maandiko yake huyu ni mtendaji zaidi kuliko siasa za majukwaani. . . . . . Sijui think tanks wa CHADEMA wanamuangaliaje
 
Last edited by a moderator:
Ukiacha Akunay, hakuna mbunge mwingine hadi sasa wa CDM aliyeangushwa katika kura za maoni. Hii inatoa picha fulani beyond Rombo. Kwa maoni yangu ni kuwa nchi nzima, wananchi wanaounga mkono CDM, wanaiunga kwa sababu wanatamani kuiondoa CCM. Hivyo katika majimbo yanayowakilishwa na CDM unaweza kuona kabisa wanaCHADEMA wanaona kama mbunge ndiye kamanda yao katika movement dhidi ya serikali... Kama ni vita basi mbunge anatazamwa kama kamanda wa kikosi aliyeko mbele kabisa.

Wananchi hawajali sana juu ya utendaji wa mbunge kwenye mambo ya maendeleo jimboni maana wanatambua kuwa kizingiti kikubwa ni serikali kuu, ya CCM.

Naamini itakuwa ngumu kidogo, au itahitaji strategy tofauti sana kuwashawishi wanaCHADEMA kuwa "kamanda tuliye naye sasa sio sahihi"...
 
Duh umekatwa mara nyingi wewe kijana tafuta kazi nyingine ufanye

kinachonishangaza kwa vijana wenzangu hasa wanaojiita wasomi kila mmoja kawa muoga wa maisha na kufikiri kias kwamba kila mmoja anadhan lazima awe kiongoz wa siasa-mim sipingi kuwa wana siasa napinga kuwalazimisha wananchi wawadhani kuwa ninyi ndio suluhu ya matatizo yao-kama lengo ni kuikomboa jamii kwann sasa msitumie elimu na weled wenu kuanzisha projects zitakazosaidia jamii na kutengeneza ajira? kwann mnadhadhalika kwa kutumikia matakwa ya akili zenu wakat uwezo huo hamna-Ben Saa 8 nakushaur fanya shughuli nyingine hizo kura ndio kauli ya wana Rombo kwako. utajidhalilisha wewe na Chama chako sasa umeanza kuutangazia umma wa Tz kuwa CDM wala sio kimbilio kwamba rushwa ni nje nje sasa km mnatoa rushwa mtaweza kweli kuisimamia Serikali-achen hizo baaana fanyeni kaz
 

Wazo la kufanyiwa kazi. . . .
 
Kura si za siri! Sasa unajuaje kuwa ulipigiwa kura na flani? Au zilipigwa za wazi!

Wagombea walikua watano. Nilipata kura zote tano.Kwa hiyo Wagombea wote walinipigia kura

Huo ulikua uchaguzi mwingine tofauti na wa wajumbe wa Mkutano Mkuu Wa Wilaya
 
Hongera.

Umeonyesha ukomavu kisiasa.

Hata hivyo, sehemu moja katika maandiko yako (hoja ya Tatu) umeandika "Sikutumia fedha nyingi...".

Maana yake nini:

1. Ulitumia fedha, ila aliyeshinda alitumia fedha nyingi kushawishi wapiga kura?

2.Ungetumia fedha nyingi, zingeweza kukupatia ushindi?

Mwisho, bado kijana. Siasa za Tanzania bado zinakuhitaji. Unanafasi. Huu uwe mwanzo, kuwa na subira utafanikiwa...
 
Wagombea walikua watano. Nilipata kura zote tano.Kwa hiyo Wagombea wote walinipigia kura

Huo ulikua uchaguzi mwingine tofauti na wa wajumbe wa Mkutano Mkuu Wa Wilaya

Sawa,Jipange pange twenty twenty.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…