Shukrani,Tahadhari na Rai yangu baada ya mchakato wa awali kura ya Maoni Rombo

Ben Mimi nimekuangalia for while una chance kubwa ya kukuwa kisiasa lakini una safari ndefu Sababu kuna mambo bado unatakiwa kuyadevelop kuweza kuwa na mvuto na ushawishi katika siasa
 
Kamanda nakukubali sana lakini kwanini usinge gombea jimbo jipya..jaribu majimbo mapya
 
Mkuu Ben, asante kwa maneno haya, umeonyesha ukomavu mkubwa na wa hali ya juu katika medani za kisiasa, kukubali kushindwa, lakini pia kushukuru kwa kidogo ulichopata!, pia najua japo hujalalamika humu, lakini natumaini utakuwa umepeleka malalamiko yako ndani ya vikao rasmi vya chama, ila kwa vile Chadema sio chama sikivu, kule hutasikilizwa, atapitishwa tena Joseph Selasini, and that being the case, na kufuatia track record ya utendani wake, kama CCM wakimsimamisha mtu makini!, Jimbo la Rombo linarejea CCM!.

Hongera for trying, hongera kukubali matokeo!, na hongera kuendelea kuwa mwanachama mwaminifu, mtiifu na mvumilivu wa Chadema, angekuwa mwingine, saa hizi mawazo yake yangekuwa kuelekea kwenye next destination!.

Pasco
 
Nashauri Chama kifanyie mabadiliko Katiba yake. Iwe marufuku kwa mwananchama kuwa mbunge zaidi ya mara mbili katika jimbo ambalo alikuwa mbunge. Hii itasaidia kupanua wigo wa wanachama wengi zaidi kutumikia wananchi.
Mkuu , huu ni ushauri wa busara sana, ili ukiishachaguliwa kiongozi Chadema, unajua deadlines zako, katika kipindi hiki cha miaka 10, Chadema inakuwa iko kwenye mikakati ya kuandaa succession plan, na kama ikitokea jimbo fulani halina able people, grooming inafanyika kabla, mfano jimbo la Moshi mjini, naamini tangu ile 2010 Ndesapesa anarudi, aliishajua hiki ndio kipindi chake cha mwisho, tangu wakati huo succession plan mechanisim would have been in place!.

Hivi ndivyo walivyotaka waasisi wa Chadema, na kipengele hiki kilikuwepo kwenye the original Katiba ya Chadema iliyowasilishwa kwa Msajili wakati Chadema inaundwa!, ila kwenye mabadiliko ya Katiba ya Chadema ya mwaka 2006, kipengele hicho kilinyofolewa kinyemela, na hakuna maelezo yoyote kiliondokaje!. Niliwahi kulizungumzia hili humu, Jee CHADEMA inaendeshwa Kwa Katiba "Fake"?. Japo wengi walinishukia, lakini Mkuu Ben Saanane, ni miongoni mwa wachache walionielewa!. Up to date, hakuna jibu lolote credible, kwa sababu waasisi walikiweka kipengele hicho for a reason, kilipoyeyuka tuu kimya kimya na wahusika kukaa kimya as if nothing has happened, pia it is a reason enough kuwa hakikujiyeyukia tuu hivi hivi just like that!.

May be in future, Chadema kikikua zaidi na kukomaa zaidi hili litawezekana!.

Pasco
 
Mkuu MTAZAMO, naunga mkono hoja, kilichomkuta ZZK ni funzo tosha kwake!.

Pasco
 
Mkuu , asante kwa hili, JF n darasa, naamini hili somo Ben Saanane atakuwa amelielewa!.
Pasco
 
Kamanda Ben umekata rufaa ya nini?
 
Kwa nini ulienda kugombea jimbo la Kamanda mwenzio? Kwani alisema hagombei tena?

Swali zuri mkuu though kwa upande mwingine hii hali ikiendelea ni nzuri kwa kuboresha demokrasia nchini vinginevyo tukisema huyu ni mwenzetu tumwache mpaka atakapoamua ni kufifisha demokrasia, kikubwa wakati watu wanashiriki kura za maoni kusiwe na hali ya kuleta hujuma
 

Succession plan. . . . .hapa ndio pana shida nadhani. . . . .au pako tricky and hazzy. . . . .

Uko sahihi Pasco
 
Last edited by a moderator:

Pasco,

Asante sana kaka.Tafadhali Check Pm yako
 
Last edited by a moderator:
Ben hakika Mungu akujarie hekima zaidi, busara zaidi, maarifa zaidi na ujuzi zaidi nafurahishwa na utilivu na uvumilivu wako. Wewe ni kioo cha watu wote wenye nia ya kuleta MAGEUZI Afrika Mungu wako hatakuacha endelea kuamini kuwa yeye yupo na atakupa zaidi ya unaovyo. Unanivutia sana Ben thanks a lot.
 
Katika ustawi wa kisiasa, mwitikio wa namna hii ni bora sana na unaonyesha ukomavu wa kisiasa
 
Hongera sana na usife moyo wala usiwakwe na tamaa ya kwamba lazima huwe...
 
Makamanda wa chadema hapa tu ndo hunifurahisha!,hongera sana mkuu ben
safari bado ni ndefu tu na utendaji na uvumilivu wako ukitukuka ndani ya chama basi utapata malipo chanya hata kama sio leo basi hata kesho!,na ukumbuke hakuna mbadala wa chadema kwa sasa ,kilichobaki ni kushirikiana na mzee selasini kwenye huu ukombozi wa pili.
Ukifanya ivyo basi siku ukinikuta nakunywa kinywaji changu mahali nitakukaribisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…