Shukrani,Tahadhari na Rai yangu baada ya mchakato wa awali kura ya Maoni Rombo

Shukrani,Tahadhari na Rai yangu baada ya mchakato wa awali kura ya Maoni Rombo

Ben Saanane

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2007
Posts
14,580
Reaction score
18,193
Mchakato wa awali wa kura za maoni Rombo katika kinyang'anyiro cha ubunge jimbo la Rombo umekamilika. Ingawa kura za awali zilizopigwa na wajumbe hazikutosha lakini ili mchakato huu ukamilike ni hadi kamati kuu itakapofanya maamuzi kwa kuwa ndicho chombo chenye jukumu hilo kikatiba. Sitapenda kuingia kwa undani kuhusu kasoro na mambo mengine kuhusu uchaguzi huu

Kwanza,Nampongeza sana Mbunge wa Zamani wa Rombo Mhe.Joseph Selasini kwa idadi ya kura alizopata. Ni jambo la kheri kuwa kabla na baada ya uchaguzi tumeendelea kuheshimiana kwa kuwa kila mmoja anamuhitaji mwingine katika kipindi hiki na sote tunatambua kuwa chama chetu ni kikubwa kuliko sisi. Maslahi ya Rombo na watu wake yatakuwa salama zaidi chini ya CHADEMA ambayo haina migawanyiko

Pili,Nawashukuru wagombea wenzangu kwa kunipigia kura nyingi katika kipengele cha Wagombea kupigiana kura.Niliongoza kwa kuwa Wagombea wote walinipigia kura akiwemo mbunge wa zamani.Kila mmoja wao alipiga kura ya kunipendekeza kuwa mgombea wa ubunge ikiwa wao hawatapitishwa na chama.Hii ni imani kubwa sana kwangu.Nina kila wajibu wa kuilinda imani hii walionionyesha

Tatu,Nawapongeza wajumbe wote walionipigia kura.Sikutumia fedha nyingi.Sikuwashawishi kwa fedha bali kwa hoja zangu.Nina deni la kuwalipa kwa imani hii kubwa walionionyesha.

Nne,Nawashukuru sana marafiki zangu walionipa sapoti kwahali na mali katika mapambano haya.Kuna kaka na Dada zangu wa JF walionisapoti kwa hali na Mali.Wakiridhia nitawataja katika pongezi zangu.Hakika sikuwahi kujisikia mwana-Familia wa JF kama kipindi hiki.

Nawashukuru sana wanahabari kwa kuwa mstari wa mbele na hasa vyombo vya habari vilivyogoma kutumika vibaya katika kipindi hiki.Kwa kuwa istilahi ya kiswahili ina upungufu mkubwa wa misamiati,nyote naomba mridhike kwa neno moja tu ninalowaambia ''ASANTENI". Asanteni sana sana

Tano,Natoa Rai kwa wagombea wenzangu,viongozi na wanachama wadumishe utulivu katika kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote

Aidha,Ninasikitishwa na kulaani vikali kitendo cha baadhi ya makamanda kupandisha bendera za chama kingine baada ya kupata taarifa za matokeo ya uchaguzi.Naomba tuwe na subira kwani maamuzi ya kamati kuu bado.Rufaa na malalamiko yatafanyiwa kazi na chombo husika.Na tuwe tayari kwa maamuzi yoyote ya kamati kuu ya chama.
Tudumishe utulivu na nimetoa Rai kwa viongozi na wafuasi wa wagombea wenzangu tuwe na uvumilivu kwani uvumilivu ndio ukomavu wa kisiasa.

CHADEMA ni kikubwa kuliko sisi sote,Rombo ni Kubwa kuliko sisi sote

Mungu Ibariki CHADEMA,Mungu Ibariki Rombo Yetu

Aluta Continua,Victory Ascerta

Ben Saanane
 
Safi,ila hapo kwenye sentence hukutumiq pesa mingi..., either ungetaja kiwango au usingeandika kabisa!!!

So far inaonyesha kama boya la tuhuma kwa mshindi na wapinzani wenza na pia boya la kukuvua wewe kwenye tope!!

Otherwise,Hongera na pia bado ni nguzo CHADEMA ambayo unastahili kusimikwa pahali kuongeza nguvu na uimara!!!
 
Kamanda Ben Saanane, Usife moyo kaza buti!
Wewe bado kijana sana naamini ipo siku utashinda tu!

Unganisha nguvu na mshindi tulitetee jimbo letu la rombo!(nimefurahi sana kwa maneno haya~chadema ni kubwa kuliko sisi sote na rombo ni kubwa kuliko sisi sote!)

USIKATE TAMAA KAMANDA!


USHAURI:

Gombea UDIWANI, THEN TARGET IWE NI KUISHIKA HALMASHAURI YA ROMBO THEN UGOMBEE UENYEKITI WA H/SHAURI~then safari ya kuelekea Dodoma iendelee taratibuuu 2020 yes itakuwa!
 
Last edited by a moderator:
huu tunauita uvumilivu wa kisiasa (political tolerance)

wewe na lowassa hamtofautiani sana mnaijua siasa sana.

please baada ya maamuzi ya kamati kuu usijehamia act
 
Nashauri Chama kifanyie mabadiliko Katiba yake. Iwe marufuku kwa mwananchama kuwa mbunge zaidi ya mara mbili katika jimbo ambalo alikuwa mbunge au Chadema ilikuwa na mbunge; kama vipi wale wazoefu waende kwenye majimbo mengine yenye magamba au wasaliti. Hii itasaidia kupanua wigo wa wanachama wengi zaidi kutumikia wananchi.
 
Mkuu Ben

Kwanza pole kwa kura kutotosha ndani ya kikao, pili nakupongeza wewe kuja hadharani na kuwathibitishia watu kwamba CHAMA ni kikubwa kuliko WEWE/SISI, na ukakubaliana na matokeo. Hilo tu linatosha kuonyesha busara kubwa uliyonayo.

Nikutakie kila lakheri kaka, Na ktk hili tuna hujashindwa peke yako. Tumeshindwa wote!! Lakini uzuri ni kwamba, sote tunatambua kwamba, Sote kama chama Tumeshinda.!!

BACK TANGANYIKA
 
Ungekuwa humble hivi miaka yote
na usingejihusisha na mgogoro wa aina yoyote ndani ya CHADEMA
nina uhakika leo ungekuwa unashukuru kupewa nafasi ya kugombea ubunge au chochote kile
anyway...jipange upya...kuna so many opportunities still huko mbele
 
Ben umeongea kwa busara sana. Nilihuzunika niliposikia na kuona matokea ya kura ulizopata. Ila huku field watu wanakuitaji zaidi kuliko 30. Trust my word.

Bravo ben
 
Ungekuwa humble hivi miaka yote
na usingejihusisha na mgogoro wa aina yoyote ndani ya CHADEMA
nina uhakika leo ungekuwa unashukuru kupewa nafasi ya kugombea ubunge au chochote kile
anyway...jipange upya...kuna so many opportunities still huko mbele
Dah,mkuu umeandika kile nilichokuwa nataka kuandika,kabla sijaandika nikajipa muda wa kusoma maoni ya wengine. Heko mkuu The Boss labda kwa nyongeza tu,hata maneno aliyoweka kwamba hakutumia pesa,kwa busara ambayo ameionyesha hapa,asingeyaweka kwa sababu yanaleta tafisiri nyingine. Maneno ya hekima aliyotoa yangebaki km yalivyo,yanamjenga zaidi kuwa kiongozi kwa siku za usoni.
 
Last edited by a moderator:
Safi sana Comrade Ben...

Ingawa kuna sehemu bado sijaelewa vizuri...Hasa hapo kuhusu Rufaa na Maamuzi ya Kamati kuu...Na kuwataka watu kutulia kusubiri maamuzi ya CC...Je unategemea kunaweza kuwa na mabadiliko ya nani agombee Rombo kwa tiketi ya CHADEMA badala ya Selasini ambaye amepata kura nyingi sana ukilinganisha na wagombea wengine?
 
Back
Top Bottom