Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,193
Mchakato wa awali wa kura za maoni Rombo katika kinyang'anyiro cha ubunge jimbo la Rombo umekamilika. Ingawa kura za awali zilizopigwa na wajumbe hazikutosha lakini ili mchakato huu ukamilike ni hadi kamati kuu itakapofanya maamuzi kwa kuwa ndicho chombo chenye jukumu hilo kikatiba. Sitapenda kuingia kwa undani kuhusu kasoro na mambo mengine kuhusu uchaguzi huu
Kwanza,Nampongeza sana Mbunge wa Zamani wa Rombo Mhe.Joseph Selasini kwa idadi ya kura alizopata. Ni jambo la kheri kuwa kabla na baada ya uchaguzi tumeendelea kuheshimiana kwa kuwa kila mmoja anamuhitaji mwingine katika kipindi hiki na sote tunatambua kuwa chama chetu ni kikubwa kuliko sisi. Maslahi ya Rombo na watu wake yatakuwa salama zaidi chini ya CHADEMA ambayo haina migawanyiko
Pili,Nawashukuru wagombea wenzangu kwa kunipigia kura nyingi katika kipengele cha Wagombea kupigiana kura.Niliongoza kwa kuwa Wagombea wote walinipigia kura akiwemo mbunge wa zamani.Kila mmoja wao alipiga kura ya kunipendekeza kuwa mgombea wa ubunge ikiwa wao hawatapitishwa na chama.Hii ni imani kubwa sana kwangu.Nina kila wajibu wa kuilinda imani hii walionionyesha
Tatu,Nawapongeza wajumbe wote walionipigia kura.Sikutumia fedha nyingi.Sikuwashawishi kwa fedha bali kwa hoja zangu.Nina deni la kuwalipa kwa imani hii kubwa walionionyesha.
Nne,Nawashukuru sana marafiki zangu walionipa sapoti kwahali na mali katika mapambano haya.Kuna kaka na Dada zangu wa JF walionisapoti kwa hali na Mali.Wakiridhia nitawataja katika pongezi zangu.Hakika sikuwahi kujisikia mwana-Familia wa JF kama kipindi hiki.
Nawashukuru sana wanahabari kwa kuwa mstari wa mbele na hasa vyombo vya habari vilivyogoma kutumika vibaya katika kipindi hiki.Kwa kuwa istilahi ya kiswahili ina upungufu mkubwa wa misamiati,nyote naomba mridhike kwa neno moja tu ninalowaambia ''ASANTENI". Asanteni sana sana
Tano,Natoa Rai kwa wagombea wenzangu,viongozi na wanachama wadumishe utulivu katika kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote
Aidha,Ninasikitishwa na kulaani vikali kitendo cha baadhi ya makamanda kupandisha bendera za chama kingine baada ya kupata taarifa za matokeo ya uchaguzi.Naomba tuwe na subira kwani maamuzi ya kamati kuu bado.Rufaa na malalamiko yatafanyiwa kazi na chombo husika.Na tuwe tayari kwa maamuzi yoyote ya kamati kuu ya chama.
Tudumishe utulivu na nimetoa Rai kwa viongozi na wafuasi wa wagombea wenzangu tuwe na uvumilivu kwani uvumilivu ndio ukomavu wa kisiasa.
CHADEMA ni kikubwa kuliko sisi sote,Rombo ni Kubwa kuliko sisi sote
Mungu Ibariki CHADEMA,Mungu Ibariki Rombo Yetu
Aluta Continua,Victory Ascerta