Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,818
- 7,940
Jana majira ya saa tano usiku wakati najiandaa kucheki muvi, nikapatwa na msukumo wa kutoka nyumbani na kwenda kuzurura mitaani. Huwa ninafanya hivi mara kwa mara ila msukumo wa jana ulikuwa mkubwa.
Nilipotoka ndani, kwanza nikakutana na kibaridi kinapiga, nilitaka kusitisha safari ila nikasema acha niende. Safari yangu nikapanga nitoke Mwananyamala, niende mpaka Makumbusho, hapo nipitilize mpaka Mwenge, nichukue Sam Nujoma Road halafu nikate ile barabara ya kupitia Kitambaa Cheupe, niunganishe mpaka Mori, niende mpaka Kijiweni, nichukue barabara ya Uzuri nikifika Darajani nichukue ya kwenda Kijitonyama niunganishe mpaka Mwananyamala.
Safari ya baiskeli ilianza freshi tu, nilipofika karibu na barabara ya kuelekea Kitambaa Cheupe, nikasimamisha baiskeli na kukaa kwenye kibenchi kidogo na macho yangu kuwaangalia wale watu wanaolala nje ya maduka.
Kulikuwa na washikaji saba, walilala na wakawa wamejifunika magunia kama mashuka yao. Kuna mwingine alikuwa anajiandaa kulala, alikuwa ananawa kisha kuchukua kitambaa kikubwa, kile wanachoandikia watu matangazo na kukifunga kamba, jamaa akajifunika, akakitumia kama shuka.
Niliwaangalia halafu nikawa najiuliza hapohapo. Mimi ni nani? Yaani huyu Mungu nimempa nini mpaka niwe nalala ndani ya nyumba, kitandani, nimejiachia na naota ndoto nzuri tu.
Mimi ni nani?
Ni mwema sana zaidi ya wale ama?
Nilisikia uchungu sana moyoni mwangu mpaka nikatokwa na machozi. Huwa nipo sensitive sana na maisha ya watu, napenda sana kuchukulia changamoto zao kama zangu. Nilikaa kwa dakika kama ishirini, nikachukua baiskeli na kuondoka.
Nikasikia msukumo mkubwa moyoni wa kuwatafutia mashuka wale watu. Nikasema nyumbani nina mashuka matatu, halafu kuna moja huwa nalipenda sana, ila hilohilo inabidi nilichukue na kwenda kumpa mtu mmoja.
Kumpa mtu kitu unachokipenda huwa ina nguvu kubwa. Yaani hata Mungu naye anaona kweli umefanya kitu kikubwa sana.
Tujifunze kuwasaidia hawa waungwana walioko mabarabarani, una nguo haikutosha, una mashuka, una viatu home au vitu vyovyote vinavyoweza kuwasogeza kimaisha wasaidieni. Tena ni vyema kutoa kile unachokipenda zaidi.
Sadaka sio tu kutoa makanisani au misikitini, ukiwapa hawa jamaa msaada ni kama umetoa Sadaka vilevile.