Shule ya English Medium imegoma kumuhamisha mwanangu. Hatiani kukosa mtihani wa darasa la nne

Lipa deni.
Uliyekuwa unamlipa hakuwa akipeleka pesa shule hivyo unadaiwa
 
Hakika, mfano mimi kama mwanaume ningehitaji kulipa karo katika account sahihi na hata kama ningekuta kamtumia mtu lazima ningefanya follow up kupata matokeo ya hiyo fedha.
Kingine kuhusu hili ningekuwa nshafika hapo shuleni physicaly, kama hakuna msaada ningepanda halmashauri ya hiyo eneo kwa afisa elimu kisha nikikosa mssada napanda afisa elimu Mkoa. (lazima wangepata majibu)

Sasa huyu ukimfuatilia ni mtu wa kupiga simu hajawahi hata kufika ilipo shule na sidhan kama anaijua. Yeye ndio yuko Dsm ila majukumu alipewa bibi yao masikini wa Mungu.


Sikatai kukosana katika mapenzi kupo, ila tusikimbilie kuachana na kujazana zile sumu za kwenye vijiwe vya wanawake kwamba hata akiniacha nitalea wanangu peke yangu.

Mwanaume atabakia kuwa mwanaume no matter tikitaka zote za mapinduzi yanayolazimishwa kufanywa na jinsia ya ke.
 
Hili ni jambo dogo sana kama angefuatilia katika sehemu sahihi kama ulivyoandika.

Inaonekana mtoa mada hajui wapi aanzie, au hana ufahamu juu ya mamlaka zinazosimamia shule na Elimu.

Akifika Halmashauri tu mtoto atahama wakati hayo mengine yanaendelea kusikilizwa. Afike Halmshauri aonane na DEO tu.

Inaonekana hiyo shule inaendeshwa kienyeji.
 
Umenena vyema ndugu.

Pia sisi wanaume tunajua kabisa ni mwanamke yupi akibaki na watoto atawamudu vizuri.

Kumuachia bibi majukumu yote ni chaguo lenye hatari nyingi ikiwemo udumavu wa watoto katika elimu na maisha.
 
Wewe hiyo shule ukitajiwa itakusaidia nini? Mnapenda sana kuharibu kazi za watu...tatizo liko kwa mzazi hajalipa ada kwa shule Bali alikuwa anamchangia mwalimu
 

Watoto wasome miaka yote hiyo bila kulipa Ada halafu bill iwe 1.2m only sio kweli.

Naona Mkuu anataka kutengeneza madeni hewa kupitia hela alizokuwa anapokea mwalimu Kishoka.

Fika Halmashauri ya wilaya onana na Afisa Elimu Msingi ukiwa na Vielelezo vyako vyote utasaidiwa.
 
Kiukweli niliposoma kichwa cha habari nikajua kuna ukiritimba nikawa tayari kukupa mtu wa kukusaidia. Ila baada ya kusoma kisa kizima, nasikitika kwamba siwezi kukupa mtu wa kukusaidia.

KUNA UKWELI HAPA LAZIMA TUKUAMBIE
Jambo la muhimu lipa ada wanayokudai au peleka uthibitisho kuwa umelipa mfano risiti, ila sio vikaratasi vya maelezo. Shule wana haki ya kukudai iwapo huna uthibitisho hawana jinsi.

Kuna makosa umeyafanya mwenyewe kumtumia mwalimu hela badala ya akaunt ya shule. Hili ni kosa ambalo hata mahakamani shule haikutambui. Ili kumuokoa mwanao apate haki, Lipa kwanza ada inayodaiwa na zile ulizolipa peleka risit ili wapige hesabu wajue unadaiwa kias gan kisha ulipe, then suala la kumtafuta tapeli wako ni la baadae.
 
Swala lake dogo kuliko anavyopanik, afike kwa afisa elimu ndio ana computer yenye taarifa zote za hiyo shule, namba ya mtoto na ndie anahamisha mtoto kutoka shule moja kwenda nyingine.

Ataelekezwa barua za kuandika na sehemu za kuzipitisha kazi inaisha.

Apunguze kutegemea kupiga simu sana ila afike katika maeneo husika uso kwa uso.
 
Ni hivi baada ya kuachana na baba wa watoto wangu niliwapeleka wanangu kwa bibi yao Mwanza.
alafu bado mnasema wanawake mnaweza🤣🤣🤣🤣 mmekubali kuingia kwenye mfumo wa wazungu mtanyooshwa sana...... majanga yanayokukuta ni kwakua hukuwa na akili ukahisi unaweza sana bila mwanaume.....

maisha haya tunategemeana sio mwanaume sio mwanamke endeleeni kusema mnaweza wenzenu waliofunguka akili wana vipato ila wanajua thamani ya mwanaume ndani.


kuachana na baba yao tu ukawabwaga kwa bibi yao...... what a fkn useless and hopeless woman
 
Kwani siku hizi mtoto akiwa darasa la mtihani inawezekana kuhama shule??? Kwa bibi tatizo ni nini?? ukizingatia mtihani wa mwisho unakaribia na shule inakudai hela uliyotapeliwa jifanye mjinga vumilia amalizee la nne au hongaa pakubwa itumiie nguvu toka juu.
 
Siku ya mtihani aende akafanyie huko.

Mtihani ya Taifa mtoto haruhusiwi kunyimwa kuifanya Kwa sababu yoyote Ile iwe kudaiwa ada au vyovyote vile.

Wakimzuia kuifanya nenda Baraza la mitihani pale mwenye kituo Cha sheli , andika barua ya kuhusu kuzuiwa kuifanya mtihani mtoto wako.

Should hiyo inaweza kufungiwa kuwa kituo Cha kufanyia mitihani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…