DOKEZO Shule ya Kibaigwa Girls imekataa kumpokea Mtoto wangu sababu sijamaliza Hela za Michango

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu sio fagio tu,kumpeleka mtoto advance ili apokelewe vitu walivyoorodhesha at least uwe na laki nne ndio pesa ya chini kabisa
Uko sahihi.

Nilikabidhiwa mwanafunzi nimpeleke kwenye hiyo shule mbona nilikiona cha moto.

Mazagazaga yote kuanzia shopping, michango, vifaa zaidi ya laki 6 ilikufa.

Hapa bado nadaiwa Jembe walisema mwezi wa 12 apeleke, ngoja nisubiri kama watafuatilia ila najua ishaisha hivyo
 
Michango ya shule ya serikali inafika laki kweli? Najua ada ni elf 35 Kwa muhula!

Isije kua mleta mada kaenda chako ni chako(jokes)
 
Laki sita unapeleka shule ya aina Gani hiyo! Isije kua unazungumzia uniform viatu godoro sijui uchafu Gani wa mwanafunzi
 
Heb share hivo vitu vinavyofika laki nne,
Wote tumesoma siku hizi, wew peleka michango mtoto apokelewe, kwa hio unataka vyoo vya mtoto wako visafishwe kwa fagio ya nani?
Jumla ya michango inayotakiwa kulipwa Bank na upeleke pay slip ni elfu 80.

Vifaa unapeleka ukiwa nacho mkononi kama Jembe, Kwanja, Ufagio wa Nje, Mopper, reki, Rimu, ndoo, Godoro, Neti n.k

Then inafuatia Shopping ndio inakula hela ndefu, kumbuka ni watoto wa kike.
 
Wamesikia. Na umeshajulikana
 
Uza hiyo smart phone mtoto asome!!
 
Jaman elimu bure ni ada tu !! Ila mahitaji ya mtoto ni wewe mwenyewe mzazi na CCM walivyo wajanja wakasema elimu bure , wazazi msibweteke kusomesha bado ni gharama aseee

Angalau kama una mtoto anaenda kidato cha tano andaa 500k umekosa sana 350k iwepo na kama huna hela weka mambo ya msingi mbele kwanza.
Mfano sare za shule (mashati) atumie alizomalizia kidato cha nne , suruali au sketi apate moja na ya kushindia !! Viatu Pair moja anaweza kuanzia !! Shoe polish ndogo counter book sio lazima aende na Quire 4 aende na ndogo ! Bananeni hivyo hivyo dogo akasome ! Huku akiondoka na wewe unacheki mazingira jinsi ya kumwinua !

Mnavyolalamika hivi dogo akienda ndo imeisha hiyo mtoto anaishi kwa tabu vibaya mno ! Hatukatai kukosa kupo ila ukishapata mtoto na mradi ulimtafuta ukiwa kwenye furaha zako huo ni wajibu sio hiyari tena!
-mzazi mtarajiwa 😂
 
Ipo hivyo mkuu,yan inabidi kujipanga hasa sio ile elimu bure basi kila kitu atakuta huko shuleni ni tofauti mkuu
 
Kwa hiyo unataka mwanao afanye usafi bila vifaa? Ninyi wazazi mnataka serikali iwanunulie watoto wenu mpaka chupi? Changieni kidogo basi na ninyi ili watoto waishi vizuri shuleni. Kam unaona ni ghali kununua mafagio mpeleke private za katoliki
 
Elimu ya TZ ni rahisi sana, yani unaambiwa fagio tu nalo hutaki kupeleka unalalamika.Tuache ujinga
Nadhani kinacholeta mtanziko hapa ni serikali kuhubiri elimu bure mpaka form 6 halafu pia jamani kuna watanzania bado ni maskini lazima hii hoja ya mkuu ipewe mashiko
 
Mleta uzi sikutetei ila huyo mkuu wa shule kama ni dada mmoja hivi mfupi na amehamia HAPO mwaka juzi basi inawezekana malalamiko yako yana ukweli maana ana kashfa ya upigaji hata huko alikotoka ngoja niishie hapa mamlaka zake zitafwatilia.
Mkuu funguka.
 
Hongera umetoa ufafanuzi vizuri, maana watu humu wanacomment kama wamekatwa vichwa,


Mtoto wa kike yupo na mahitaji mengi sana,,,,
 
Bro si ulipie tu uachane na hizo Mambo
 
Elimu ya TZ ni rahisi sana, yani unaambiwa fagio tu nalo hutaki kupeleka unalalamika.Tuache ujinga
Unajua nchi zilizoendelea na zenye elimu bora inayoendesha hii dunia, wanafunzi hawafuti hata vumbi katika viti vyako, wachilia kuleta fagio? Elimu (rahisi sana) ni nini kwa mtazamo wako?
 
Sasa wewe ukitetewa huoni na Wazazi wengine watapuuzia suala la kukamilisha ada wakitegemea kutetewa? Shule itaendeshwaje?

Kwanini hukuomba ukamilishe ada na kununua vifaa ndio uende?

Hukuwa na mawasiliano ya Mkuu wa shule na makamu wake?
Na muda unamsubiri yeye tu au huoni changamoto licha ya kueleza bayana umbali anakotoka hivyo kuna gharama nyingi tu mpaka afike shuleni? Kwa uchumi gani wa MTz wa kawaida?
 
Uongozi wa shule umeshindwa kuweka utaratibu wa malipo kufanyika kwa awamu? Kwa nini wanakataa kumpokea mwanafunzi?
 
Vitabu ni hiyari acha kudanganya watu hapa....pumbav
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…