DOKEZO Shule ya Kibaigwa Girls imekataa kumpokea Mtoto wangu sababu sijamaliza Hela za Michango

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sijaelewa hilo zingatio lako kwamba wewe unatoka Mtwara!
 
Mleta uzi sikutetei ila huyo mkuu wa shule kama ni dada mmoja hivi mfupi na amehamia HAPO mwaka juzi basi inawezekana malalamiko yako yana ukweli maana ana kashfa ya upigaji hata huko alikotoka ngoja niishie hapa mamlaka zake zitafwatilia.
Amuone Diwani mheshimiwa Chande anaweza msaidia.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Mmmmh!! Laki nne ni vitu gani hivyo?
Tena hiyo laki 4 nimefanya kupunguza tu ila zaidi,kwa upande wa michango ya shule aizidi laki 1 kwenye mahitaji ya vitu atakavyotumia akiwa shule ndio gharama na kama mzazi utakiwi kuvikwepa kama wajibu ila pia na kipato wazazi awafanani pia
 
Vipaumbele, kipaumbele cha mwanafunzi ni kupata elimu Bora lakini shule za serikali walimu, vitabu sio kipaumbele wakati hivyo ni vitu vya misingi anavyotakiwa kupata mwanafunzi.
Kuna bwege huko juu anadai vitabu ni hiyari kama mzazi unampelekaje mwanao shule bila vitabu si bora abaki tu nyumbani!
 
Sasa Laki 4 ni hela ya kulalamika kweli? Tanzania Ina watu wazemne sana,basi akashitaki Chadema Ili wampost Twitter,stupid father
Unaiona laki 4 ndogo but on ground kuna watu wanalipwa mshahara hadi laki 2 kwa mwezi,hiyo hiyo asomeshe,anunulie chakula na alipe kodi,shida inakuja wenzetu wapenda siasa mkiwa na uwezo wa kushika mia 2 mia 3 basi mnaona kila kitu rahisi!
 
Inaskitisha sana. Wazazi wengi sana isivyokawaida wanapeleka watoto private o level to a level, ada so chini ya Million 2.

Hawa waliobaki wanadai elim bure, watoto hata kiatu soksi ni ugonvi.

Nchi yyt ile mchaw ni mwananchi mwenyewe
 
Mzazi acha malalamiko
 
Sasa sijui alitaka nani amfanyie shopping mwanae
 
Sasa sijui alitaka nani amfanyie shopping mwanae
Ninachokiona kwa huyu mleta mada ni kuwa, hii huenda ni mara ya kwanza kwake kuepeleka mwanafunzi shule ya bweni.

Angekuwa kashawahi asingetatizika kupambana. Inabidi ajitahidi akope hiyo hela ili alipie na mwanafunzi apokelewe halafu awaahidi kumalizia vitu vingine vidogo vidogo.
 
Sasa Bro si ukaripoti kwa Afisa Elimu Kata au wilayani kama unaona hupati usaidizi nenda hata kwa Mkuu wa Wilaya,kwa nini wakusumbue namna hiyo?
 
Unaiona laki 4 ndogo but on ground kuna watu wanalipwa mshahara hadi laki 2 kwa mwezi,hiyo hiyo asomeshe,anunulie chakula na alipe kodi,shida inakuja wenzetu wapenda siasa mkiwa na uwezo wa kushika mia 2 mia 3 basi mnaona kila kitu rahisi!
Kwa nini wasiongeze kipato? Harafu mtoto kufaulu sio kama msiba kwamba unakuja ghafla
 
Vipaumbele, kipaumbele cha mwanafunzi ni kupata elimu Bora lakini shule za serikali walimu, vitabu sio kipaumbele wakati hivyo ni vitu vya misingi anavyotakiwa kupata mwanafunzi.
Sawa kipaumbele ni elimu Bora,Je mazingira wanayoishi Ili kupata hiyo elimu Bora hayatakiwi kuwa masafi?
 
Haya malalamiko mengine muwe mnaangalia na nyie kosa lenu liko wapi sio kulaumu walimu tu.

Utaratibu ni upi, na fomu ya hiyo shule wamekwambiaje, isijekua unalalamika tu ilhali kwenye fomu umeambiwa umalize kila kitu ndo umpeleke mtoto.

Wanasiasa wanatumia fursa kama hizi kujinufaisha kisiasa ilhali wanawaumiza wale waliosimamia haki.
 
Walimu wanapewa sana lawama na mara nyingi hawastahili hizo lawama toka kwa wazazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…