Shule ya Msingi ya Museveni, Chato: Watoto wa nani watasoma humo?

Shule ya Msingi ya Museveni, Chato: Watoto wa nani watasoma humo?

..amefanya kuenzi mchango wa Tz ktk kuikomboa Uganda toka ktk makucha ya udikteta wa Iddi Amin.

..bila Tz kuingia kijeshi Uganda uwezekano mkubwa Iddi Amin angefia madarakani.
Kwanini hiyo shule haikujengwa Butiama, nyumbani kwao Nyerere aliyemfurusha Idd Amin?
 
Mimi ni binadamu kama binadamu wengine. Sijawahi kuwa wa ajabu, na sitarajii niwe wa ajabu. Siku nitakapokuwa wa ajabu, sitaitwa mwanadamu.

Ninachokisema ni kuwa hii shule siyo ya ajabu. Tumekuwa na shule kama hizo na hata nzuri zaidi ya hizo. Leo kwa nini tunaiona shule hiyo kuwa ya ajabu kiasi hata cha kuwa na hofu kuwa watoto wa wananchi wa kawaida hawatapata nafasi ya kusoma kwa sababu nafasi zitajazwa na watoto wa viongozi na matajiri?

Ni shule imetolewa msaada na Mseveni. Ni jambo jema. Ni sawa na mtu akikupa zawadi ya Tshirt, hata kama una suti na mashati, utaipokea ile Tshirt kutokana na dhamira njema ya yule aliyekupatia. Lakini haitamaanisha kuwa Tshirt zote, na mashati na suti ukizokuwa nazo vimekosa ubora kiasi kwamba kila siku utakuwa unapaparika kuivaa hiyo tshirt.

Shukrani kwa Mseveni kuwajengea shule wananchi wa Chato.

Gadafi aliwajengea msikiti na rest house waislam wa Butiama. Nami nilipoenda Butiama, Mwalimu akiwa hai nililala pale. Alichokifanya Mseveni ni kizuri lakini siyo cha pekee, siyo cha ajabu na wala haimaanishi hatukuwa na shule nzuri kama hiyo au nzuri zaidi kabla yake. Kwa Chato, yawezekana, hiyo ndiyo shule nzuri zaidi, sina uhakika. Lakini kwa baadhi ya maeneo ndani ya nchi yetu, hiyo shule ni ya kawaida.
We we hueleweki, umeambiwa kuwa shule za aina hiyo mkoa wa Geita ziko 2 tu na kati ya hizo 2 mojaawapo ndio hii. Unajotoa ufahamu unaposema shule zaidi ya hii ziko nyingi.
 
Kwanini hiyo shule haikujengwa Butiama, nyumbani kwao Nyerere aliyemfurusha Idd Amin?

..Museveni amejenga shule nyingine maeneo ya Kagera ambako aliwahi kupata hifadhi.

..ilimradi shule iko Tz maana yake kila raia ana haki ya kusoma hapo.

..aliyemfukuza Iddi Amin sio Mwalimu Nyerere, bali makamanda na wapiganaji wa Jwtz walio-risk maisha yao kwenda vitani.
 
Like really? Mzazi au ndugu unampeleka mtoto Chato kwenda kusoma?
Ulizeni wenyeji!!
 
Asome mtoto wa kikwete,ama wa mama Samia au wakwangu wote hao ni watanzania ,kwangu sioni shida kwani baada ya kupata elimu jukumu Lao Ni kuwahudumia watanzania!!
Rudi chekechea; unajua maana ya "equal opportunity" au ulidesa?! [emoji23]
 
Hakuna tajiri atakayemtoa mtoto wake mjini Mwanza au Dar ampeleke kijijini Chato. That is a primitive environment ambayo inaweza kuathiri maisha ya mtoto, kiasi cha yeye kuarithiwa na mazingira yanayomzunguka. Pamoja na mazingira ya shule, mazingira ya jumla yanaweza kumwathiri mtoto.

Ukimsikiliza yule Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chato, halafu yule awe mwenyekiti wa bodi ya shule au mjumbe wa bodi, unatarajia hiyo shule itakuwaje? Shule siyo majengo pekee.

Hiyo shule haina chochote cha pekee. Haitofautiani na shule nyingi zilizojengwa na kumilikiwa na watanzania. Wala haitafikia hadhi ya shule kama ya Olympio and the like.

Jipe muda, baada ya miaka 3 utajua ipo daraja gani.

Hiyo shule itatoa huduma zaidi kwa wananchi wa Chato. Watafute watu wenye exposure ili zaidi ya kutoa elimu ya darasani, jamii ya shule ibadilishe fikra za jamii, hasa kuhusiana na maisha ya ustaarabu. Yule mwenyekiti wa Halmashauri ya Chato alinipa picha mbaya sana.
Shule za kanisa/seminari zipo vijijini tena porini kabisa mbona wazazi wanawatoa watoto wao kutoka kwenye majiji na wanakwenda kusoma huko?
 
Shule hii illiyojengwa na Rais wa Uganda ni mingoni mwa shule chache za serikali zitakazotoa mafunzo yake kwa lugha ya Kiingereza sawa na shule za Olympio, Diamond, Oysterbay, nk. Shule hizi ni shule za kulipia ada ndogo kabisa kuliko shule za aina hii za watu binafsi na mashirika ya dini.

Wasiwasi wangu mkubwa ni namna watoto wa watanzania wa kawaida watakavyoweza kupata nafasi kwenye shule hiyo dhidi ya watoto wa viongozi wa Chama na serikali, walimu na wafanyabiashara wakubwa wenye uwezo wa kifesha na ushawishi.

Makundi haya ya wenye fedha na vyeo yataacha pia kupeleka watoto wao shule binafsi zenye ada kubwa na kwenda kujaza watoto wao kwenye shule hii.

Kamati ya shule lazima iwe fair kwenye selection ya watoto watakaojiunga na shule hii. Kigezo kiwe ufaulu wa mtoto kwenye mtihani wa kujiunga na shule, isiwe ni mtoto wa nani au ameletwa na nani. Kuna vi memo vingi na rushwa kubwa sana katika kupata nafasi kwenye hizi shule.

Watu wanapiga pesa ndefu kupatia watu nafasi kwa njia ya kujuana, cheo, na nafasi kwenye jamii. Matokeo yake wanasoma watoto wa kundi fulani na kuwaacha watoto wenye uwezo mkubwa kiakili wanaotoka familia zisizo na majina/wanyonge.

Hapo malengo ya Museven yatakuwa bure kabisa.

Acha hofu. Hata hapa Mwanza Jiji ipo inaitwa Nyanza English Medium na bado haijajaa. Nayo inatoa matangazo kila siku ya watoto kuja kujiunga.
 
Shule za kanisa/seminari zipo vijijini tena porini kabisa mbona wazazi wanawatoa watoto wao kutoka kwenye majiji na wanakwenda kusoma huko?
Ni kweli, nilimpeleka binti Yangu shule ya Kilomeni (kijijini hasa hasa na kwelikweli) kutoka shule ya Jangwani girls Dar es salaam.
 
Asome mtoto wa kikwete,ama wa mama Samia au wakwangu wote hao ni watanzania ,kwangu sioni shida kwani baada ya kupata elimu jukumu Lao Ni kuwahudumia watanzania!!
Watasoma watoto wa chatu.
 
Mimi nimefurahishwa na ramani ya ujenzi ya hii shule. Nimesikia Ummi Mwl akisema gharama za kujenga shule ni milioni 600 sasa nawashauri hii ramani iwe kwa mashule yote ya umma.
 
Andiko lako limejaa chuki..punguza chuki na ubinafsi havitakusaidia...chuki na umasikini ni ugonjwa mbaya sana.

#MaendeleoHayanaChama
Yuko sahihi, let's be honest wewe kama unaishi Dar au Morogoro unaweza kumpeleka mtoto huko akasome wakati kuna same schools nearby??
 
Yuko sahihi, let's be honest wewe kama unaishi Dar au Morogoro unaweza kumpeleka mtoto huko akasome wakati kuna same schools nearby??
Ulishawahi kutafuta nafasi ya mtoto wako kusoma kwenye shule za English medium za serikali?

Bei ya chini Ada kwa shule ya msingi binafsi ni sh 2,000,000 wakati ada kwa shule ya serikali ni 300,000 tu. Kuna mkanyagano mkubwa kwenye kupata nafasi kwenye shule hizi za serikali. viMemo vya wakubwa wenye mbavu nene ni rundo zima, pochi nyingi ziko wazi kwa mwalimu mkuu na kamati za shule.
 
Back
Top Bottom