Shule ya Msingi ya Museveni, Chato: Watoto wa nani watasoma humo?

..amefanya kuenzi mchango wa Tz ktk kuikomboa Uganda toka ktk makucha ya udikteta wa Iddi Amin.

..bila Tz kuingia kijeshi Uganda uwezekano mkubwa Iddi Amin angefia madarakani.
Kwanini hiyo shule haikujengwa Butiama, nyumbani kwao Nyerere aliyemfurusha Idd Amin?
 
We we hueleweki, umeambiwa kuwa shule za aina hiyo mkoa wa Geita ziko 2 tu na kati ya hizo 2 mojaawapo ndio hii. Unajotoa ufahamu unaposema shule zaidi ya hii ziko nyingi.
 
Kwanini hiyo shule haikujengwa Butiama, nyumbani kwao Nyerere aliyemfurusha Idd Amin?

..Museveni amejenga shule nyingine maeneo ya Kagera ambako aliwahi kupata hifadhi.

..ilimradi shule iko Tz maana yake kila raia ana haki ya kusoma hapo.

..aliyemfukuza Iddi Amin sio Mwalimu Nyerere, bali makamanda na wapiganaji wa Jwtz walio-risk maisha yao kwenda vitani.
 
Like really? Mzazi au ndugu unampeleka mtoto Chato kwenda kusoma?
Ulizeni wenyeji!!
 
Asome mtoto wa kikwete,ama wa mama Samia au wakwangu wote hao ni watanzania ,kwangu sioni shida kwani baada ya kupata elimu jukumu Lao Ni kuwahudumia watanzania!!
Rudi chekechea; unajua maana ya "equal opportunity" au ulidesa?! [emoji23]
 
Shule za kanisa/seminari zipo vijijini tena porini kabisa mbona wazazi wanawatoa watoto wao kutoka kwenye majiji na wanakwenda kusoma huko?
 
Acha hofu. Hata hapa Mwanza Jiji ipo inaitwa Nyanza English Medium na bado haijajaa. Nayo inatoa matangazo kila siku ya watoto kuja kujiunga.
 
Shule za kanisa/seminari zipo vijijini tena porini kabisa mbona wazazi wanawatoa watoto wao kutoka kwenye majiji na wanakwenda kusoma huko?
Ni kweli, nilimpeleka binti Yangu shule ya Kilomeni (kijijini hasa hasa na kwelikweli) kutoka shule ya Jangwani girls Dar es salaam.
 
Asome mtoto wa kikwete,ama wa mama Samia au wakwangu wote hao ni watanzania ,kwangu sioni shida kwani baada ya kupata elimu jukumu Lao Ni kuwahudumia watanzania!!
Watasoma watoto wa chatu.
 
Mimi nimefurahishwa na ramani ya ujenzi ya hii shule. Nimesikia Ummi Mwl akisema gharama za kujenga shule ni milioni 600 sasa nawashauri hii ramani iwe kwa mashule yote ya umma.
 
Andiko lako limejaa chuki..punguza chuki na ubinafsi havitakusaidia...chuki na umasikini ni ugonjwa mbaya sana.

#MaendeleoHayanaChama
Yuko sahihi, let's be honest wewe kama unaishi Dar au Morogoro unaweza kumpeleka mtoto huko akasome wakati kuna same schools nearby??
 
Yuko sahihi, let's be honest wewe kama unaishi Dar au Morogoro unaweza kumpeleka mtoto huko akasome wakati kuna same schools nearby??
Ulishawahi kutafuta nafasi ya mtoto wako kusoma kwenye shule za English medium za serikali?

Bei ya chini Ada kwa shule ya msingi binafsi ni sh 2,000,000 wakati ada kwa shule ya serikali ni 300,000 tu. Kuna mkanyagano mkubwa kwenye kupata nafasi kwenye shule hizi za serikali. viMemo vya wakubwa wenye mbavu nene ni rundo zima, pochi nyingi ziko wazi kwa mwalimu mkuu na kamati za shule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…