Mkuu, naelewa sana suala la barabara za PPP. Hizo hutolewa kama alternative roads, ambapo kunakuwa na barabara ya serikali na ile ya PPP. Nilikuwa Turkey nikataka kusafiri kwa gari toka Ankara kwenda Istanbul. Unakuwa na choice - kutumia barabara ya PPP ambayo ni fenced road three lanes kila upande na haina speed limit na ina vibanda vya road toll kila umbali fulani, au ile ya serikali ya free ambayo ni single lane. Kama huo ndio utakuwa mpango sina tatizo.
Na kama ukileta suala la kusema kuna barabara za PPP sijui, basi ondoa tozo la kujenga na kukarabati barabara kwenye dizeli na petroli.
Bila hayo ni kweli nitapinga. Angalia hapa chini sehemu ya mkeka wa Ankara-Istanbul ambao ukitumia unalipia. Sasa ukiweka huu kwa ajili ya Dar - Arusha ukasema tulipie na hauna tochi wala spidi limit, leta fyombo tu!
View attachment 1620141