Si kwa ajili ya ubaguzi, bali namshauri Rais Samia aepuke kufanya maamuzi makubwa ya muda mrefu yanayohusu upande wa Tanzania bara peke yake

Si kwa ajili ya ubaguzi, bali namshauri Rais Samia aepuke kufanya maamuzi makubwa ya muda mrefu yanayohusu upande wa Tanzania bara peke yake

..Suluhisho ni muungano wa serikali 3.
Kuwe serikali tatu.
Yaani kuwe na federal government itakayo fanya mambo ya serikali kuu ya jamhuri ya muungano na kuwe pia na serikali mbili za ziada za States.
Yaani Tanganyika State na Zanzibar State.
Hapa Tanganyika kwa sasa tunatawaliwa na mzanzibari wakati Zanzibar hairuhusiwi kutawaliwa na mtanganyika.
 
Anakasirika kusikia tu tunasema maamuzi kama ya bandari kwa DP World, kuchimba madini ndani ya Serengeti, Samia asiyafanye kwa sasa, bali yaje yafanywe na raisi kutoka bara kwa sababu impact yake iko zaidi upande wa bara, na kama ni makosa isije ikasemwa mtu wa Zanzibar alituponza. Huyo lazima ana wajomba kule uarabuni.
Mimi nafikiri wa kulaumiwa ni nyerere aliyewaponza zanzibar kwa kuwaamulia kujiunga na tanganyika na pia kuwaamulia Tanganyika kuungana na zanzibar kwa mihemko na maslahi ya zanzibar zaidi kuliko tanganyika,
Yote kwa yote, nadhani suluhu la yote haya ni kuuvunja tu huu muungano, full stop,
Anayetaka kuishi huku atakuwa mtanganyika na atakaetaka kuishi kule atakuwa mla urojo, basi shughuli imeisha
 
Mkuu hoja yako ya Serikali tatu ama moja ni mzuri, lakini ni ngumu kutekelezeka; maana mshirika mmoja wa huo Muungano bado ana Nchi yake yenye hadhi ya kuwa NCHI na wakati huo huo mshiriki mwingine hana Nchi, alishaigawa kwa sababu ali iona ni kubwa mno.
Linatekelezeka kwa kuirudisha nchi ya Tanganyika.
Kwanini iwe dhambi kuirudisha hiyo nchi?
 
Tanganyika haihitaji Zanzibar! kuna athari gani Tanganyika ikiwa Zanzibar wataondoka katika muungano!
Hakuna jambo wazanzibari wanalisubiria kwa hamu kama kutoka ndani ya muungano, tatizo tu ni kwamba kwanini watanganyika tunalazimisha? Hapo tu ndio shida, kama ni hasara tanganyika inapata sana ila sisi ndio tunalazimisha muungano, kwanini lakini?
 
Shida kubwa sio maamuzi ya Honorable causa,bali Watanganyika tunasalitiwa na Watanganyika wenzetu,hivyo adui yetu ni Watanganyika wenye uroho wa madaraka.
 
Najua kwamba Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, lakini ni jambo lililo wazi kwamba yeye kama Rais wa Tanzania, maamuzi yake kwa zaidi ya 98% yanahusu upande wa Tanzania bara peke yake, kwa sababu upande wa Zanzibar wana raisi wao na serikali yao.

Katika hali kama hii, na ukizingatia kwamba Rais Samia anatokea upande wa Zanzibar, ningeshauri sana kwamba Rais Samia ajiepushe kufanya maamuzi makubwa ambayo ni ya muda mrefu (yana lock-in effect ya muda mrefu) upande wa bara peke yake. Kumekuwa na hisia zinazozidi kukua kwamba Rais Samia anafanya maamuzi ambayo baadaye yatakuwa na athari mbaya upande wa Tanzania bara, wakati yeye amemaliza muda wake na kurudi Zanzibar, na kuwaacha Watanzania bara wakisumbuliwa na matokeo ya maamuzi yake.

Mifano ya maamuzi ambayo Rais Samia anachukua juu ya mambo yanayohusu bara peke yake ni kama suala la mkataba wa bandari kwa DP Word ya Dubai, na hili la kuchimba madini ndani ya mbuga ya Serengeti na nyinginezo, ambapo, TANAPA, chombo cha utalii Tanzania bara, kilishalikataza sana.

Ingekuwa busara sana kama Rais Samia angeonyesha subira na kuacha maamuzi juu ya mambo makubwa kama hayo, yenye long term lock-in effect, yafanywe wakati Rais wa Tanzania ni mtu kutoka upande wa bara. Hii itasaidia kutokuza chuki na kutoa hofu upande wa bara kwamba Raisi Samia hafanyi mambo kwa manufaa ya watu wa bara, na labda ana ajenda ya siri.
Mmeisha anza kusaga kunguni baada ya kina marope kusafishwa?
 
Hakuna jambo wazanzibari wanalisubiria kwa hamu kama kutoka ndani ya muungano, tatizo tu ni kwamba kwanini watanganyika tunalazimisha? Hapo tu ndio shida, kama ni hasara tanganyika inapata sana ila sisi ndio tunalazimisha muungano, kwanini lakini?

..sasa hivi wanaolazimisha ni Wazanzibari.

..Wazanzibari ndio wameshika hatamu za Uraisi wa muungano, na Uraisi wa Zanzibar, kwa hiyo wana fursa ya kipekee kurekebisha au kuvunja muungano.

..Tatizo Mama Abduli amevutiwa mno na mali anazovuna toka Tanganyika.
 
Ni wasanii haswa, Zanzibar wanautaka muungano 100% sababu hawezi kupata nchi nyingine ya wajinga kama bara, huku wapo huru kwa lolote kufanya, nenda wewe sasa ukaonyeshwe kazi.
Ukitaka kujua Zanzibar ni watu wa aina gani, subiri awamu ya Samia iishe, utaona kelele za kero za muungano na tuvunje muungano zitakavyoongezeka!
 
Hakuna jambo wazanzibari wanalisubiria kwa hamu kama kutoka ndani ya muungano, tatizo tu ni kwamba kwanini watanganyika tunalazimisha? Hapo tu ndio shida, kama ni hasara tanganyika inapata sana ila sisi ndio tunalazimisha muungano, kwanini lakini?
Siyo Watanganyika ni CCM na Wabunge wa CCM pamoja na VIongozi wa Serikali wasioijali mama Tanganyika.

Nakuhakikishia kama kuna kitu kinawatia hofu Wazanzibar ni kuvunjika Muungano.
Usiwasikilize akina '' wa Oman koko'

Wana uwezo wa kuvunja muungano, hawana hawana uthubutu au ubavu wala pumzi
 
..sasa hivi wanaolazimisha ni Wazanzibari.

..Wazanzibari ndio wameshika hatamu za Uraisi wa muungano, na Uraisi wa Zanzibar, kwa hiyo wana fursa ya kipekee kurekebisha au kuvunja muungano.

..Tatizo Mama Abduli amevutiwa mno na mali anazovuna toka Tanganyika.
Kwanini hutaki kukubali ukweli kwamba watanganyika ndio wanafosi muungano?
Unajua wale kule zenji walianzisha hata harakati za uamsho kudai Zanzibar yao na waliishia wapi?
Acha masihara kwenye mambo makubwa bwashee
 
Siyo Watanganyika ni CCM na Wabunge wa CCM pamoja na VIongozi wa Serikali wasioijali mama Tanganyika.

Nakuhakikishia kama kuna kitu kinawatia hofu Wazanzibar ni kuvunjika Muungano.
Usiwasikilize akina '' wa Oman koko'

Wana uwezo wa kuvunja muungano, hawana hawana uthubutu au ubavu wala pumzi
Wazenji hawautaki muungano ila hawajui wanauvunjeje?
Watanganyika kwanini wanafosi muungano?
 
Back
Top Bottom