Usitafute vijisababu ku justify makosa ya DIKTETA. Ndege za ATCL jazikuwapo kabla ya Magufuli, kwani tulikuwa hatusafiri?
Kwanza ilikuwa cheap kusafiri na Fast Jet kwa Tsh 90,000 Mwanza -Dar kuliko sasa ATCL kwa Tsh 300,000+
Ila
Kilatha bado uko kwenye blanketi la Mwendazake maana hata CAG ameripoti kuwa ATCL ni loss making parastatal kwenye 2020/21 report
ATCL kupata hasara hiyo sio news, labda siku wakipata faida.
Sikuwahi kuwa shabiki wa manunuzi ya ndege mainly kwa sababu niliamini kulikuwa na investment nyingine zinaleta social utility zaidi.
Kwakuwa zipo na mali ya Tanzania busara ni kuona shirika linafanya vizuri, and I have always been a critic of their pricing strategies.
So sishangai shirika kupata hasara but that has nothing to do with Magufuli it’s purely a management issue.
Kosa la Magufuli lilikuwa kusikiliza makelele ya mitandaoni sijui Rwanda, Kenya, Uganda na nchi za africa zinatushinda wana ndege zao sisi hatuna tunakodi, ohoo biashara ya ndege inalipa, sijui national flag carrier inatangaza nchi etc with nonsense. Hizo ndio zilikuwa hoja za mitandaoni enzi za J.K.
Walau J.K wakati wake alikuwa mkweli kwenye hili la ndege hao jamaa tumeshajaribu kuwawezesha kwa kila namna hiyo biashara awaiwezi kuwanunulia ndege ni kutupa hela tu.
Magufuli yeye akasikiliza vilio vya mitandaoni ndio hayo; unawezaje tengeneza hasara kwenye ndege ambazo umepewa at low interest payment charges and you are pretty much a monopoly on the local market.
Wameshindwa ata kuingia strategic alliance na ndege za kimataifa zinazoishia Nairobi, kuleta abiria wanaokuja Tanzania. Matokeo yake abiria wote wa ndege hizo wanaokuja Tanzania wanaletwa na Kenya Airways na ni sehemu kubwa ya mapato yao.
Yaani Kenya wakileta fujo mpakani Tanzania ikisema Kenya Airways isitue KIA tu dakika moja wanaomba yaishe maana ndani ya miezi tunalitia shirika lao hasara kubwa sana. Sisi wenyewe hatuna muda wa kutafuta hizo strategic alliances.
Ni hivi kufeli kwa ATCL ni management problems sio Magufuli kuna makosa luluki ya kimkakati sasa kwanini tushangae kupata hasara.
Kwetu kumekucha 👋