Si sahihi kumpa maagizo Waziri Mkuu hadharani, si kila kiongozi anaweza kupewa maagizo hadharani

Mi naona kama utovu wa nidhamu. Waziri mkuu ni kiongozi mkubwa hapaswi kuagizwa kufanya jambo fulani na katibu muenezi wa chama. Serikali ni kubwa kuliko chama. Kuna nchi rais wake anaweza kuachana na chama chake kilichomuingiza ikulu na akaanzisha chama kingine huku akiendelea na urais wake
 
Anachokifanya Makonda ndicho haswa alichoteuliwa kukifanya.

Makonda ni mithili ya udongo, unamfinyanga vile unataka awe.

Makonda ni mouthpiece ya waliomteua ili aongee yale wasioweza kuyaongea kwa wanaotakiwa kufikishiwa ujumbe.
Umemaliza kila kitu mkuu!! Bila shaka mhusika anajua fika kuwa nyuma ya Makonda kuna nguvu kubwa ambayo hawezi kuthubutu kuhojiana nayo!! Sana sana anaweza kukaa kimya tu!! Mwulize Warioba alivyofanyiwa na Makonda kwenye mchakato wa katiba mpya!! We unafikiri Makonda alikuwa na ubavu gani wa kufanya hayo aliyoyafanya? Hata wakati wa JPM, Makonda alikuwa ni "mouthpiece"/kinywa cha kigogo wa juu kabisa!! Mwulize aliyekuwa waziri wa habari na michezo wakati ule(Moses Nauye) akuambie yaliyompata alipojaribu kupambana na Makonda!! Mama saa hizi roho kwatu na atalala usingizi mwanana maana amempata mwarobaini wa waliokuwa wasumbufu kwake!!. Tatizo tarajiwa kwa Makonda ni moja tu: nini hatima yake mama akitoka hapo? Je atakayemrithi mama ataendelea kumlinda Makonda kama yeye alivyoendelea kumlinda baada ya JPM kuondoka? maana lazima kuna siku mama atatoka hapo!! Mama kamlinda sana Makonda (kimya kimya) vinginevyo saa hii habari ingekuwa nyingine kabisa.​
 
ukimuona nyanii mjini jua kuna mwenye nae...!!
 
we kenge kasome
Na huu ndio ukomo wa fikra zako kushindwa kuelewa kilichoandikwa na kukimbilia matusi/dhihaka, sina sababu ya kukujibu kwa tusi maana hapo hakutokuwa na tofauti yeyote baina yetu.

Maisha ni mafupi mno kuwa na ghadhabu hata pale pasipohitaji hasira. Uwe na siku njema yenye amani ya nafsi.
 
Tuende mbele na kurudi nyuma: Baada ya JPM watendaji serikalini wamejisahau sana!! Mama hawamheshimu, uuonevu makazini umerudi tena kwa kasi, ubadhirifu umerudi kwa kasi! Mabosi kuweka kikao ofisini na kula sitting allowance kumerudi kwa kasi!! Semina, warsha na makongamano yasiyokuwa na kichwa wala miguu yamerudi kwa kasi!! Uonevu kwa wananchi umerudi kwa kasi. Na vyote hivi vimeendelea bila mkemeaji!! Matatizo huko Ardhi hasa baada ya kuondoka huko yule waziri nguli, yamerudi upya!! Yote haya yanataka mtu jasiri, anayeweza kukemea na kuwajibisha kwa ujasiri na kufuatilia mguu kwa mguu kama Makonda!! Uwepo wa Makonda ni kete nzuri sana kwa CCM na kwa mama katika kurejesha tena imani ya wananchi kwa serikali yao, hasa tunapoelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025. Kwa dati kabisa ninapongeza sana uteuzi wa Makonda!!
NIPENDEKEZE: Makonda awe mgombea mwenza wa Samia kwenye uchaguzi mkuu!! Watanzania tutashuhudia namna makamu wa Rais anavyoweza kupiga kazi!!​
 
Kuna namna Waziri Mkuu anapaswa kusoma alama za nyakati na kuamua namna nyingine. Kwanza ameletewa naibu hii nikusema kwamba hatoshi lakini pia hizi amri za Makonda zina baraka za aliyemteua. Ni fedheha mtu kama Majaliwa kupewa amri hadharani na Makonda jinsi ya kutekeleza majukumu yake.
 
Waungwana wa JF nawasalimu,

Nimesoma, nimesikia na kuona kuwa Katibu wa Halmashauri ya Taifa Itikadi na Uenezi wa CCM Paul Makonda akitoa maagizo kwa Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa na kumapa miezi sita kuyatekeleza. Makonda alitoa maagizo hayo aliyoyasema kuwa ni ya chama (CCM) huko Dodoma.

Pamoja na nguvu kubwa ya chama tawala (CCM) juu ya Serikali ambayo huundwa na chama hicho, si sawa kumpa maagizo Waziri Mkuu hadharani. Hata Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa huepuka kumpa maagizo Waziri Mkuu hadharani. Vivyohivyo kwa Makamu wa Rais.

Waziri Mkuu, kichama, ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM; Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM. Kwa nafasi yake, ni sehemu ya ndani kabisa ya chama. Waziri Mkuu, kiserikali, ni mtendaji mkuu wa serikali na mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni. Hushauriana na Rais hata kwenye teuzi mbalimbali, zikiwamo za Mawaziri.

Kulingana na nafasi ya Waziri Mkuu ndani ya CCM na Serikali, si sawa wala busara kumuagiza hadharani kufanya hili au lile. Pamoja na kuwa mwanachama wa CCM katika nafasi nilizozitaja, ni kiongozi wetu kitaifa. Tunamheshimu na anapaswa kulindiwa heshima yake. Kumuagiza kwa kumtaja hadharani kunaweza kutafsirika kama kumtweza na kumbagaza.

Waziri Mkuu ana majukumu makubwa na mengi. Anafanya kazi kubwa na nyingi. Anafanya kazi za chama chake-CCM na Serikali yetu. Tumheshimu Waziri Mkuu wetu....asitwezwe kwa mgongo wa chama na maagizo ya chama.
Mimi nilishangaa au siku hizi hawafanyi vikao? Ni kichekesho kinacho sikitisha.... ndiyo hivyo Mama alitegemea Makonda mzima? Acha kuchezea damu ya watu,jamaa ndiyo kaisha Chisinau hivyo.
 
Umemaliza kila kitu mkuu!! Bila shaka mhusika anajua fika kuwa nyuma ya Makonda kuna nguvu kubwa ambayo hawezi kuthubutu kuhojiana nayo!! Sana sana anaweza kukaa kimya tu!! Mwulize Warioba alivyofanyiwa na Makonda kwenye mchakato wa katiba mpya!! We unafikiri Makonda alikuwa na ubavu gani wa kufanya hayo aliyoyafanya? Hata wakati wa JPM, Makonda alikuwa ni "mouthpiece"/kinywa cha kigogo wa juu kabisa!! Mwulize aliyekuwa waziri wa habari na michezo wakati ule(Moses Nauye) akuambie yaliyompata alipojaribu kupambana na Makonda!! Mama saa hizi roho kwatu na atalala usingizi mwanana maana amempata mwarobaini wa waliokuwa wasumbufu kwake!!. Tatizo tarajiwa kwa Makonda ni moja tu: nini hatima yake mama akitoka hapo? Je atakayemrithi mama ataendelea kumlinda Makonda kama yeye alivyoendelea kumlinda baada ya JPM kuondoka? maana lazima kuna siku mama atatoka hapo!! Mama kamlinda sana Makonda (kimya kimya) vinginevyo saa hii habari ingekuwa nyingine kabisa.​

Ni kweli....Ulinzi utaendelea au itakuwaje baadae.
 
Waungwana wa JF nawasalimu,

Nimesoma, nimesikia na kuona kuwa Katibu wa Halmashauri ya Taifa Itikadi na Uenezi wa CCM Paul Makonda akitoa maagizo kwa Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa na kumapa miezi sita kuyatekeleza. Makonda alitoa maagizo hayo aliyoyasema kuwa ni ya chama (CCM) huko Dodoma.

Pamoja na nguvu kubwa ya chama tawala (CCM) juu ya Serikali ambayo huundwa na chama hicho, si sawa kumpa maagizo Waziri Mkuu hadharani. Hata Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa huepuka kumpa maagizo Waziri Mkuu hadharani. Vivyohivyo kwa Makamu wa Rais.

Waziri Mkuu, kichama, ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM; Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM. Kwa nafasi yake, ni sehemu ya ndani kabisa ya chama. Waziri Mkuu, kiserikali, ni mtendaji mkuu wa serikali na mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni. Hushauriana na Rais hata kwenye teuzi mbalimbali, zikiwamo za Mawaziri.

Kulingana na nafasi ya Waziri Mkuu ndani ya CCM na Serikali, si sawa wala busara kumuagiza hadharani kufanya hili au lile. Pamoja na kuwa mwanachama wa CCM katika nafasi nilizozitaja, ni kiongozi wetu kitaifa. Tunamheshimu na anapaswa kulindiwa heshima yake. Kumuagiza kwa kumtaja hadharani kunaweza kutafsirika kama kumtweza na kumbagaza.

Waziri Mkuu ana majukumu makubwa na mengi. Anafanya kazi kubwa na nyingi. Anafanya kazi za chama chake-CCM na Serikali yetu. Tumheshimu Waziri Mkuu wetu....asitwezwe kwa mgongo wa chama na maagizo ya chama.
"mtoto pendwa" wa SHUJAA karudishwa kundini baada ya kutengwa na kondoo zingine, sasa kapanda juu ya meza na kujamba mbele ya wageni!
 
Kwa Waziri Mkuu chawa Kama Majaliwa aendelee kumdharilisha. Na ikiwezekana Makonda amwite ofisini kwake ajielezee akiwa Kapiga magoti.
 
Back
Top Bottom