Waungwana wa JF nawasalimu,
Nimesoma, nimesikia na kuona kuwa Katibu wa Halmashauri ya Taifa Itikadi na Uenezi wa CCM Paul Makonda akitoa maagizo kwa Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa na kumapa miezi sita kuyatekeleza. Makonda alitoa maagizo hayo aliyoyasema kuwa ni ya chama (CCM) huko Dodoma.
Hili silioni kama jambo geni. Nani asiyemjua Paul! Hakuanza kutoa maagizo leo. Ni Paul huyu aliyelitukana 'Bunge' , Waziri mkuu akiwemo. Nini kilifanyika? Ni impunity. Si huyu paul alikuwa anatoa maagizo kila siku wakati wa JPM, wote wakiwemo PM walikuwa kimya. Jambo zuri la Paul ni kuwa consistent na utendaji wake, habadiliki.
Waziri Mkuu, kichama, ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM; Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM. Kwa nafasi yake, ni sehemu ya ndani kabisa ya chama. Waziri Mkuu, kiserikali, ni mtendaji mkuu wa serikali na mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni. Hushauriana na Rais hata kwenye teuzi mbalimbali, zikiwamo za Mawaziri.
Kwahiyo Waziri mkuu ni sehemu ya watu waliokubali uteuzi wa Paul. Si kukubali gizani, bali walikubali wakimjua.
Hapa kuna tatizo la ''ego' . Viongozi wanaogopa nafasi zao binafsi na si heshima na hadhi za nafasi zao.
Usingeweza kumtweza Kawawa, Malecela, Salim , Warioba, Msuya kireja reja namna hiyo. Ni hawa wasakatonge
Kulingana na nafasi ya Waziri Mkuu ndani ya CCM na Serikali, si sawa wala busara kumuagiza hadharani kufanya hili au lile. Pamoja na kuwa mwanachama wa CCM katika nafasi nilizozitaja, ni kiongozi wetu kitaifa. Tunamheshimu na anapaswa kulindiwa heshima yake. Kumuagiza kwa kumtaja hadharani kunaweza kutafsirika kama kumtweza na kumbagaza.
Kwanza, anapaswa alinde heshima yake halafu tutmheshimu. Mzee Warioba aliwahi kwenda kwa Nyerere na kumwambia kama abcd inafanyika mimi najiuzulu.. Tena hiyo ilikuwa siri ya serikali lakini hakujali nafasi yake, alijali heshima ya nafasi na heshima yake. Mzee Warioba yupo anadunda heshima zinamfuata!
Waziri Mkuu ana majukumu makubwa na mengi. Anafanya kazi kubwa na nyingi. Anafanya kazi za chama chake-CCM na Serikali yetu. Tumheshimu Waziri Mkuu wetu....asitwezwe kwa mgongo wa chama na maagizo ya chama.
Narudia tena, lazima kwanza aheshimu nafasi yake halafu sisi tutamheshimu. Juzi alikuwa na chaguo, kumkaripia Paul au kumwambia Mwenyekiti kama humkemei hadharani naachia ngazi, hakufanya anaogopa asijekatwa jina wakati wa kinyang'anyiro cha Urais.
Ukimsikiliza Paul, kuna kauli anayotumia '' anamshukuru Rais SSH kwa kubeba jina lake hadi Kamati kuu''
Hii ni kuwaambia watu uwepo wake si wa kubahatisha, yeye ni mteule wa Mwenyekiti wa CCM na Rais kama wao
Juzi kasema ni maagizo ya chama, sasa unajiuliza Waziri mkuu hakuwepo kwenye vikao vya chama!
Paul atawasumbua sana kwasababu hawana mtima, wanaogopa vyeo na wanavizia teuzi. Huko ndiko uwanja wa 'nyumbani' wa Paul.