Si sahihi kumpa maagizo Waziri Mkuu hadharani, si kila kiongozi anaweza kupewa maagizo hadharani

Hata hapo Malawi ilifanyika hivyo !
Rais alianzisha Chama chake akiwa Ikulu !
kwa hapa nchini wanasema sekretarieti ya chama cha mapinduzi ina nguvu kubwa kuliko kiongozi yeyote wa serikali isipokuwa rais. Wanahalisha katibu wa uenezi wake ana mamlaka ya kum command kiongozi yeyote wa serikali isipokuwa rais. Tuseme tu huo ni mfumo wa chama chao kutawala, haiwezekani katibu wa itikadi na uenezi kumsulubu waziri mkuu au makamu wa rais huo ni utovu wa nidhamu na ni utawala mbovu (regime)
 
Jidanganye....siku anaacha uanachama..na urais unasepa hapohapo
 
Kweli watu Wanasemaga SiHasa ni uongo uongo tu unaokubalika !
Ngoja tuone !!
 
Mwamba alisemaga Mtanikumbuka !
Umagufulication katika kuongoza Nchi hakukwepeki !
Ndio maana Makonda alipokelewa pale Lumumba kwa kibwagizo cha -
Magufuli Magufuli Magufuli !! Everything was planned !

β€œMtanikumbuka kwa yale mazuri sio kwa yale mabaya β€œ By Mwamba !
 
Maagizo yakitolewa ndan mnakimbilia space mnasema watu dhaifu,wengine lugha za kejeli "hili nalo mkalitizame" au hii sio kejel huko twita au mnafikiri hatuoni? Maagizo yanatolewa live live bila chenga napo mmekuja kuanza kulia sasa wakil msom mbona space kule tunakuaga wote hamuelewek.au ndio nasikia mnatumia kero za wananch kama kete.zikishughulikiwa tutakosa ajenda
 
Jidanganye....siku anaacha uanachama..na urais unasepa hapohapo
Rais wa Nchi ni mkubwa sana kuliko chochote kile katika Nchi !!
Na wengine wakaongeza na cheo cha Mwenyekiti wa Chama ambaye pia kwa kanuni zilizopo Chamani Mwenyekiti hawezi kutikiswa na yeyote pale Chamani πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ™πŸ™πŸ™ !
 
Anayetoa maagizo anatumwa na mwenyekiti ambaye ndiye boss wa huyo waziri mkuu. Samia ni rais mpole na pia hana uwezo wa kurumbana hadharani na wasaidizi wake ambao wote ni wanaume waliomzunguka.

Ujumbe anaoutoa Makonda moja kwa moja una akisi kile ambacho boss anafikiria muda huo huo. Huyo ni mjumbe tu hauawi hata siku moja.

SSH anachukuliwa kama Mama na ni hulka inayompa aina fulani ya udogo mbele ya wasaidizi wake tofauti na JPM aliyewavaa uso kwa uso wote waliomkera na kumkwaza katika kufanikisha mipango ya kimaendeleo.

Kawapelekea Makonda waumane wao kwa wao, huo ndio ujumbe wa Samia ndani ya CCM na ndani ya serikali kuu.
 
Ni nyakatib hizi tu za Paul Makonda ambazo waziri mkuu anapewa maelekezo hadharani na kiongozi wa chama chake
 
Nilifikiri mada imeambatana na vifungu vya sheria kumbe hisia tu.

Hili agizo lingetolewa na mtu mwingine si ajabu isingekuwa topic!

Ndiyo maana mmeletewa Makonda wanajua kila atakachoongea ni mjadala.
 
Ila PM naye ana moyo! Ingekuwa Mimi ningekuwa nikishaniuzuru siku nyingi sana. Sio kwa movie hizi
 
😁😁😁
Your browser is not able to display this video.
 
sasa nimeelewa kwann aliteuliwa makamo waziri mkuu
 
Wameshawekana sawa ili lionekane si tatizo
Your browser is not able to display this video.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapi na nani kasema kashindwa kazi? PM atakuwepo Kila Kona ya Tzn? Kwa hiyo Wananchi wakiibua shida asielekezwe au? Acha ujinga
Najaribu kutafuta mjinga ni nani nashindwa.
Yaani PM kapelekewa Dotto ambaye ana ulinzi/sauti kuliko manaibu wote hujiulizi!??
Haya PM anaagizwa agizwa tu kama mtendaji wa kitongoji bado tu hushtuki!!?
Ngoja niwaachie ulimwengu watajibu.
 
Acha wavuane nguo tu maana sisi wananchi wenye njaa na maisha magumu hayatuhusu
 
Acha wavuane nguo tu maana sisi wananchi wenye njaa na maisha magumu hayatuhusu
Usiseme hivi... Nchi inaenda inavoenda kwa sababu washajua wananchi wengi hawana interest na siasa za nchi!
Hivyo viongozi wanaiba tu na kuwasababishia ugumu wa maisha
 
Ndo yametokea tufanyeje Sasa ?Yesu macho na masikio!
 
Hili silioni kama jambo geni. Nani asiyemjua Paul! Hakuanza kutoa maagizo leo. Ni Paul huyu aliyelitukana 'Bunge' , Waziri mkuu akiwemo. Nini kilifanyika? Ni impunity. Si huyu paul alikuwa anatoa maagizo kila siku wakati wa JPM, wote wakiwemo PM walikuwa kimya. Jambo zuri la Paul ni kuwa consistent na utendaji wake, habadiliki.
Kwahiyo Waziri mkuu ni sehemu ya watu waliokubali uteuzi wa Paul. Si kukubali gizani, bali walikubali wakimjua.
Hapa kuna tatizo la ''ego' . Viongozi wanaogopa nafasi zao binafsi na si heshima na hadhi za nafasi zao.
Usingeweza kumtweza Kawawa, Malecela, Salim , Warioba, Msuya kireja reja namna hiyo. Ni hawa wasakatonge
Kwanza, anapaswa alinde heshima yake halafu tutmheshimu. Mzee Warioba aliwahi kwenda kwa Nyerere na kumwambia kama abcd inafanyika mimi najiuzulu.. Tena hiyo ilikuwa siri ya serikali lakini hakujali nafasi yake, alijali heshima ya nafasi na heshima yake. Mzee Warioba yupo anadunda heshima zinamfuata!
Waziri Mkuu ana majukumu makubwa na mengi. Anafanya kazi kubwa na nyingi. Anafanya kazi za chama chake-CCM na Serikali yetu. Tumheshimu Waziri Mkuu wetu....asitwezwe kwa mgongo wa chama na maagizo ya chama.
Narudia tena, lazima kwanza aheshimu nafasi yake halafu sisi tutamheshimu. Juzi alikuwa na chaguo, kumkaripia Paul au kumwambia Mwenyekiti kama humkemei hadharani naachia ngazi, hakufanya anaogopa asijekatwa jina wakati wa kinyang'anyiro cha Urais.

Ukimsikiliza Paul, kuna kauli anayotumia '' anamshukuru Rais SSH kwa kubeba jina lake hadi Kamati kuu''
Hii ni kuwaambia watu uwepo wake si wa kubahatisha, yeye ni mteule wa Mwenyekiti wa CCM na Rais kama wao

Juzi kasema ni maagizo ya chama, sasa unajiuliza Waziri mkuu hakuwepo kwenye vikao vya chama!

Paul atawasumbua sana kwasababu hawana mtima, wanaogopa vyeo na wanavizia teuzi. Huko ndiko uwanja wa 'nyumbani' wa Paul.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…