Tetesi: Si shwari, rais Magufuli kutangaza mazito August 31 siku moja kabla ya UKUTA

Tetesi: Si shwari, rais Magufuli kutangaza mazito August 31 siku moja kabla ya UKUTA

Siasa uchwara za maji taka kamwe hazitaruhusiwa milele. Mikutano ya siasa safi inayofuata kanuni, taratibu na sheria za nchi hazijawahi kuzuiwa. Wewe ulishaona wapi siasa za kumwita rais aliyechaguliwa na majority, hao minority walioshindwa wanamuita uchwara na kuandamana nchi nzima wakimwita hivyo. Kama si upunguani ni nini? Lazima cha mtema kuni wakionje angalao kidogo ili waone kautamu kake.

Tarehe 1 Sep wanaotaka kuonja hako kautamu kake jitokezeni tu wala haina haja ya kuja kubwabwaya huku Jf sasa hivi. Tarehe 2 tunawasubiri mje mtusimulie hako ka utamu ka mtema kuni.
Baada ya kukaa na kutumia akili zote ukaleta utumbo huu dr akili
 
Hata kama wapinzani hawataandamana lakini wangalau taifa limetambua kwamba kuna mahali rais anaenda mrama. Na kwa kwa mtazamo mpana hata yeye itabidi aitii katiba kwani alidhani anaweza kuifuata kwa jinsi apendavyo. Pia hali hii itamfanya awe makini zaidi na kuhakikisha hayo maendeleo anayoyahubiri ni lazima ayatekeleze ili kuwanyamazisha wapinzani wake maana kinyume na hapo ajue atapingwa mpaka achanganyikiwe. Ajue kama aliahidi viwanda bila kuwa na mkakati basi aandae jeshi la kutosha kwani upinzani atakaokutana nao hatokaa asahau maishani mwake.
 
The greatest fear is when you fear the unknown.
Akihutubia hiyo tarehe 31 basi ujue anawaogopa ye awaache tu aone kama wataandamana.
Ila pia polisi wamechoka mwezi mzima mazoezi ya kumkabili usiemjua inasikitisha sana!!!
Kama mkuu wa nchi kutoa angalizo kwa unaowaongoza ni jambo jema
 
Nguvu kubwa ya nini sasa? Kwani anapambana na jeshi la nchi nyingine?mbona muheshimiwa anafanya kaz nyepesi iwe ngumu? Unapambana na waandamanaji wasio na siraha sasa nguvu kubwa ya nini?
Kwani akiwaruhusu waandamane kama taifa tutapata madhara gani? Haya mambo ni yakawaida sana lakini naona mfumo wa kiutawala una complicate mambo tu.
 
Atangaze kuachana na udikteta uchwara na kuanza kuiheshimu katiba ya nchi atangaze Wabunge wote wa upinzani waliofukuzwa bungeni sasa wana haki ya kuruhusiwa kuingia Bungeni atangaze kuacha kuingilia na kuvuruga vikao vya Bunge ili kuwadhibiti wapinzani au mpaka kieleweke asidhani yeye yuko juu ya katiba na hivyo kuweza kufanya lolote huku akiendelea kuidharau katiba ya nchi na kuwanyima haki waliyopewa wapinzani ndani ya katiba.
Very simple kuandika humu ukijishashadua kuwa utaandamana nenda ujipime na nguvu ya dola
 
Atangaze kuachana na udikteta uchwara na kuanza kuiheshimu katiba ya nchi atangaze Wabunge wote wa upinzani waliofukuzwa bungeni sasa wana haki ya kuruhusiwa kuingia Bungeni atangaze kuacha kuingilia na kuvuruga vikao vya Bunge ili kuwadhibiti wapinzani au mpaka kieleweke asidhani yeye yuko juu ya katiba na hivyo kuweza kufanya lolote huku akiendelea kuidharau katiba ya nchi na kuwanyima haki waliyopewa wapinzani ndani ya katiba.
Naamini vibweka hivi tarehe 01/9 ndo final, Kati ya ukiwa na Magufuli Nani ataibuka kidedea, tusubiri.
 
Yet another package of EMPTY THREATS, as usual?

Certainly, the police force will have at least conducted enough drills to keep or bring its officers in shape!
 
Tayari kuna mpango wa kuwakamata viongozi wa Chadema tarehe 27 mwezi huu lakini walishatonywa kwa hiyo wamejiandaa.
 
Habari nilizopata kutoka jikoni zinasema kuwa siku ya August 31 mwaka huu, siku moja kabla ya UKUTA rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kutangaza mambo mazito kwa watanzania.

Inasemekana kuwa rais anatarajiwa kuliweka jeshi la polisi katika tahadhari kubwa huku kukiwa na mazuio kadhaa yatakayo ambatana na tahadhari hiyo kwa jeshi la polisi.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi kunatarajiwa kuwa na operesheni nzito ya jeshi la polisi na huenda kukatumika nguvu kubwa zaidi katika kukabiliana na Chadema nchi nzima.

Aidha nimedokezwa kuwa ofisi zote za Chadema nchini zinatarajiwa kuzingirwa na jeshi la polisi siku hiyo ya september moja.

#UKUTA for Democracy!

UKUTA` DUMEZIMA UNANG'ANG'ANIA WA NINI?????
 
Tayari kuna mpango wa kuwakamata viongozi wa Chadema tarehe 27 mwezi huu lakini walishatonywa kwa hiyo wamejiandaa.
Ha ha haa!..hawa jamaa wa Chadema hua wanapatia wapi Intelegensia yao?hua nawakubali sana.kweli hichi ndio chama cha upinzani tz
 
AC
Atangaze kuachana na udikteta uchwara na kuanza kuiheshimu katiba ya nchi atangaze Wabunge wote wa upinzani waliofukuzwa bungeni sasa wana haki ya kuruhusiwa kuingia Bungeni atangaze kuacha kuingilia na kuvuruga vikao vya Bunge ili kuwadhibiti wapinzani au mpaka kieleweke asidhani yeye yuko juu ya katiba na hivyo kuweza kufanya lolote huku akiendelea kuidharau katiba ya nchi na kuwanyima haki waliyopewa wapinzani ndani ya katiba.
HA KUWATISHA WATU WEWE BAK! Huna lolote zaidi ya kunyea ndoo...baada ya maneno yako machafu kumtukana Mheshimiwa Rais...
 
Back
Top Bottom