Si upungufu wa nguvu za kiume tu umekuwa tatizo hata uwezo wa wanaume kuzalisha unapungua

Si upungufu wa nguvu za kiume tu umekuwa tatizo hata uwezo wa wanaume kuzalisha unapungua

Sijaelewa na nahisi siwezi kuelewa......

Hivi ni wanaume ndio wanakuwaga na tatizo la nguvu za kiume na kushindwa kuwatosheleza wake zao?


Ombi kwetu mabaharia.... Ukiona mchumba wako,mkeo anakuambia huna lolote na hujafanya lolote jua huyo siyo size yako tokea na umuache utakuja kunishukuru
Ahsante sana kwa ushauri wako na nikuahidi kwamba naufanyia kazi ushauri wako. Ubarikiwe sana
 
Ni kweli kwamba tatizo hili linakuw kwa kasi ya ajabu hapa nchini (pengine na sehemu nyingine pia) kwanza tatizo halisi lenyewe linasababishwa na aina ya maisha na malezi ambayo tunalea watoto wetu na vijana wetu wa leo. Mama ametumia madawa ya uzazi wa mpango kwa miaka 10, (hatujui madhara yake kwake na kiumbe kinachofuata), anahangaika anapata ujauzito anajifungua mtoto wa kiume maskini ya Mungu mtoto anaanza kuvalishwa diapers toka siku ya kwanza (nani ajuaye madhara ya zile kemikali kwenye mfumo mzima wa uzazi?) , Mtoto analishwa vyakula synthesized toka madukani (vingine vimepita na muda), anakua anafikia kula vyakula vingine, chakula kikuu ni chips na mayai na coka au fanta baridi kwa miaka mingi.

Upande mwingine wa shilingi watu wazima wanaishi maisha ambayo ni too relaxed hasa sehemu za mijini, vijana wanakunywa pombe kupita kiasi vyakula wanavyokula sio nutritive kiasi cha kutosha hawafanyi mazoezi muda mwingi wamekaa makazini wakitoka hapo wanakaa baa hadi saa sita za usiku wanarudi nyumbani kulala.. mwili unakuwa goi goi na minyama uzembe hapo ni lazima tu utapata moja kati ya matatizo tajwa (upungufu wa nguvu za kiume au low sperm count)

Kundi la mwisho ambalo ndio kubwa zaidi ni kundi ambalo kimsingi hawana tatizo ila wanaaminishwa kwamba wana tatizo na wao wameamini kwamba wana tatizo kutokana na aina ya wanawake wanokuwa na mahusiano nao. By the way tatizo la ukosefu wa nguvu za kike ni kubwa kuliko la ukosefu wa nguvu za kiume, wanawake wengi hawafiki kileleni sababu wamekosa nguvu za kike kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kuanza kujihusisha na mapenzi katika umri mdogo, lakini atasema hafiki kwa sababu mwanaume anayempa huduma hiyo hana nguvu za kiume, mwanaume ataamini hivyo na kuanza kutafuta madawa ambayo yanamuongezea tatizo ambalo kimsingi hakuwa nalo kabla.
 
Itabidi nianzishe biashara za kuwatia vibendi wenye uhitaji..

Mimba ya pili nitafanya kwa discount ya 25%, ya 3 kwa 35% ya 4,5 kwa 50%

Wenye uhitaji karibuni sana[emoji23]
 
Tunakwama wapi jamani........life style wengi wanadhani ni kuvaa pekee,,,, chakula ni habari ya mjini kusababishs yote haya,,, vyakula vya asili vipo shida ni kuiga na kujijaza ujinga kwa kufuata mifumo ya maisha ya wakoloni.
 
Usisahau pia kuna jitihada za makusudi za mabeberu ku control population ya dunia. Sisi tukiwa kama wapokeaji wa kila aina ya madawa, bidhaa za vyakula, vinywaji nk kutoka nje, hatuwezi kujua ni kwa kiasi gani vitu hivi vinaweza kua vimefanyiwa editing ili visaidie ku control population in the long run. Sisi tunachekelea tu kugonga hennesy na jack daniel , kwa wenye pharmas wanakuambia dawa inayoongoza kuuza ni p2, hatujui madhara ya mbeleni.....
 
Usisahau pia kuna jitihada za makusudi za mabeberu ku control population ya dunia. Sisi tukiwa kama wapokeaji wa kila aina ya madawa, bidhaa za vyakula, vinywaji nk kutoka nje, hatuwezi kujua ni kwa kiasi gani vitu hivi vinaweza kua vimefanyiwa editing ili visaidie ku control population in the long run. Sisi tunachekelea tu kugonga hennesy na jack daniel , kwa wenye pharmas wanakuambia dawa inayoongoza kuuza ni p2, hatujui madhara ya mbeleni.....
Rafiki yangu mmoja mtoto wake pekee wa kiume ana tatizo hili. Ameoa mwaka wa tatu huu mke hajakamata ujauzito, baada ya kutembelea hospitali kadhaa imefahamika tatizo ni la mwanaume.

Shost amekumbuka kuwa kijana alipokua na miaka mitano alipata cancer, walihangaika na mionzi na aliweza kupona kumbe madhara ya tiba ile imeondoa uwezo wa uzazi.

Wameamua kutafuta watoto wadogo waasili.
 
Back
Top Bottom