Si wote ndani ya Serikali wanafurahia kunangwa Hayati

Si wote ndani ya Serikali wanafurahia kunangwa Hayati

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
Huo ndiwo ukweli.

Wengi wao wapo hapo kwa namna moja ama nyingine kwa msaada wa Hayati hususani wana siasa.

Pamoja na kwamba baadhi ya wateule walitenguliwa lakini ni imani yangu waliobaki wapo wasiofurahishwa na kunangwa kwa boss wao wa awali!
 
Wananchi hawapendezwi na hili jambo kabisa.

Wanaona kiongozi wao yuko mbali nao.

Anawakumbatia wafanyabiashara na matajiri.

Hasikii vilio vyao. Inasikitisha mno .
 
Sio kunangwa,watu wanafunguka Ili kuponya mioyo yao.
 
CCM kumejaa wanafiki sana sikutegemea kuona post za Le mutuz kumchana vipande bosi wake aliyekuwa akimuita Le fieldmarshal Paul Makonda waliyekuwa wanakula nae bata live.

Watu wa ccm siku mama anastaafu watamnanga balaa lakini sasa hivi wanafurahia tuu posho wanazolipwa maana inaonekana mama si mbanaji wa posho sababu hana roho mbaya.
 
Tutegemee Magufuli kunangwa zaidi ya hapa kwa sababu hii ni strategy ambayo rais Samia ameamua kuitumia ili kupunguza umaarufu wa JPM huku mtaani kwa lengo la kuinua profile yake. Lakini kwa jinsi mambo yanavyokwenda sioni kama hii itafanikiwa. Kama upepo hautabadilika na kufanya hali ya maisha kuwa nafuu kwa watu wenye kipato cha chini, Samia atakuwa kwenye hali ngumu sana. Time will tell.
 
Mwaka mmoja akiwa madarakani Magufuli alikuwa amefanya kazi kubwa sana na ilikuwa inaonekana.

Kuanzia kwenye sera na sheria hadi huduma na uwajibikaji. Alikuwa ameshaiweka nchi kwenye msitari na alikuwa very popular.

Mama yenu ana zaidi ya mwaka na mwezi mmoja na bado ni unpopular kuliko hata Kikwete, kwahiyo anaumia. Anatapatapa.

Pole zake. Na asipokuwa makini 2025 itafika hajafanya chochote cha maana.
 
Wananchi hawapendezwi na hili jambo kabisa.

Wanaona kiongozi wao yuko mbali nao.

Anawakumbatia wafanyabiashara na matajiri.

Hasikii vilio vyao. Inasikitisha mno .

Wananchi gani, hao mliopora uchaguzi mkawawekea majizi ya ccm? Mngekuwa mnajali wananchi mngeheshimu box la kura. Mnajificha kwa wananchi dhalimu akipewa ukweli wake.
 
Back
Top Bottom