Mjuni Lwambo
JF-Expert Member
- Apr 25, 2012
- 11,133
- 12,361
SIRI+NYEPESI, ila sina uhakika kama hatuzijui, ninajua wengi tunazijua ila hatuzifuati.Point yangu sio kwamba utajiri ni siri,bali point yangu ni kuwa utajiri ni siri nyepesi ambazo hatuzijui.
Siri+nyepesi.
Utajiri ni rahisi sana, ni rahisi sana kiasi kwamba tunashindwa kuufikia.
Tatizo moja la kitu kirahisi ni kwamba kinaboa, ndio maana wengi hawakifanyi. "Naomba uniruhusu niwe nachanganya na kizungu ili kufafanua vizuri" It is simple, but not easy.
Kutajirika inatakiwa ufanye kitu rahisi kila siku lakini kwa muda mrefu kiasi, tuseme miaka kumi, unafanya kitu kilekile, hapa ndipo inapoboa. Utajiri hauhitaji uwe na mbwembwe, haihitaji mizuka wala ngedembwe.
Mfano; kama wewe umeajiriwa, labda unalipwa laki tano, kila ukipokea mshahara, unaweka laki mbili pembeni, laki tatu ndio unatumia na familia yako, kila mwezi. Baada ya mwaka mmoja utafikisha milioni moja na laki mbili, unanunua bodaboda, kisha unaendelea na zoezi lile lile la kuweka laki mbili kila mwezi...
Halafu kila mwaka unanunua bodaboda, kama ukiendwlea hivyo kwa miaka kumi, hata kama hujawa tajiri lakini utakuwa umepiga hatua kubwa. Simple but not easy, not easy because it a simple and mechanical way of doing things, haikupi mwanya wa kuandaa birthyfay parties kwa sababu utaingilia ratiba ya kuweka laki mbili....
Not easy kwa sababu ni aina ya maisha inayokosa msisimko, na binadamu tunataka msisimko, leo umeenda club, kesho umenunua dela jipya, unachukua mkopo benki unanunua vitz, hivyo vyote ni msisimko wa maisha... Kwa hiyo unachokisema ni siri, kimekaa kwenye kitu kinaitwa DELAYED GRATIFICATION, japo kuna mengine pia ya kuambatisha hapo.
Nimejaribu kufafanua kwa ufupi.