Siamini kama utajiri unapatikana kwa njia ngumu zenye mateso

Tokea zamani nimekuwa siamini msemo unaosema kwamba utajiri unahitaji uvumilivu,subira,kupitia magumu nakadhaalika.

ninachoamini ni kwamba utajiri sio mgumu kupatikana ni rahisi lakini huwenda njia zake hizo watu hawazijui(zina siri)

Tukumbuke kuwa kitu kuwa rahisi haina maana kwamba watu watakijua kitu hiko,kinaweza kuwa ni rahisi na bado ikawa ni siri pia.

Mimi naamini utajiri una formula zake nyepesi nyepesi za siri ambazo wachache wanazifahamu.

KAMA utajiri ni kupitia magumu mbona leo tuna idadi kubwa ya watanzania wanaofanya kazi ngumu za kilimo na ujenzi na bado hawawi matajiri ?

KAMA utajiri unahitaji muda ukiwa katika kazi ngumu mbona kuna watu wanazeekea na kufia katika kazi za ujenzi miaka na miaka bila kuwa matajiri ?

Kama utajiri ni kupitia magumu na mateso basi leo watanzania wengi sana wangekuwa matajiri kwa sababu idadi kubwa ya watanzania wanafanya kazi ngumu.

Bakhresa wanasema alitoka kwenye kazi ya kushona viatu,mbona kuna wanaozeekea katika kazi hiyo hawawi kama bakhresa ?

Utajiri naamini ni siri,tena siri ni nyepesi mno lakini nadhani huwenda wengi wetu tunaamini kwamba lazima tuteseke kwanza na kuumia ndipo tupate utajiri.

Nakataa kujifariji kwamba mateso ninayopitia ni ishara ya kutoboa mbeleni kwa sababu wapo wanaozaliwa kwenye mateso na kufia kwenye mateso bila kuuona utajiri.
Kunatofauti kubwa kati kufanya kazi kwa bidii.. na kufanya kazi kwa akili

"Work smart.. not hard"

Sent from my SAMSUNG-SM-J327A using JamiiForums mobile app
 
Mungu sio mbinafsi hivyo "eti humpa yeyote amtakae" kwahiyo Mungu anachagua nani awe tajiri na nani awe maskini..!!!

Mungu sio mbinafsi kiasi hicho aisee.

#YNWA
Tushirikiane bas ili tuwe matajiri au mwenzangu ushatoboa?
 
Hayo uliyoainisha ndo msingi wa utajiri wa Mungu ulipo tatizo tumegoma kabisa kuukubali ukweli, hebu angalia binadamu alitokana Adam na Adam akaambiwa utakula kwa jasho maana yake apambane kulisha familia yake na kuipa urithi na bado Mungu akatoa agizo kwa wanaume wote kwamba watawapa Mali watoto wao alisema Mali na urithi mtu atapewa na babaye hivyo baba aliyepambana kiasi cha kuwa na Mali za kuwapa uzao wake wapate pa kuanzia ndo anaweza kutengeneza matajiri wenye mlengo wa Mungu ila Sasa hayo tumewaachia watu waupe wafanye kwa kuzaa watoto na kuwapa muelekeo na sisi ni kuzaa tu bila kujua nini tunawapa watoto wetu, zaidi sana hata viongozi wa Dini hawatoi msisitizo hapo, Kila baba anawajibu wakutoa Mali kwa watoto aliowazaa na kuwaweka kwenye maadili ya kuzalisha hizo Mali Ili ziwafikie wajukuu na vitukuu ila Sasa tunaenda kinyume kabisa na maandiko yaani wajukuu ndo watafute Mali Ili watoe ulirithi na Mali kwa mababu zao na hata wazazi hii ikikomeshwa tutaona Kila mtu anatumia muda na nguvu zake vizuri.
Somo kubwa sana umenipatia ndugu.
 
Mungu sio mbinafsi hivyo "eti humpa yeyote amtakae" kwahiyo Mungu anachagua nani awe tajiri na nani awe maskini..!!!

Mungu sio mbinafsi kiasi hicho aisee.

#YNWA
Kuna luck na risk

Soma.

Ecclesiastes 9:11
[11]I returned, and saw under the sun, that the race is not to the swift, nor the battle to the strong, neither yet bread to the wise, nor yet riches to men of understanding, nor yet favour to men of skill; but time and chance happeneth to them all.

Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
 
Utajiri naamini ni siri,tena siri ni nyepesi mno lakini nadhani huwenda wengi wetu tunaamini
Nilipoanza mwenyewe kuisoma Biblia Takatifu na kuielewa ndiposa nikajua siri zote za utajiri zimejificha humo na matajiri wakubwa wanapitia vitabu vitakatifu kupata itajiri toka kwa Mungu.

Naendelea kujifunza kwa vitendo. Omba Roho wa Mungu akufunulie kidogo tu siri za utajiri utashangaa
 
Ahare na sisi baadhi ya siri kama hutojali
 
SIRI+NYEPESI, ila sina uhakika kama hatuzijui, ninajua wengi tunazijua ila hatuzifuati.

Utajiri ni rahisi sana, ni rahisi sana kiasi kwamba tunashindwa kuufikia.

Tatizo moja la kitu kirahisi ni kwamba kinaboa, ndio maana wengi hawakifanyi. "Naomba uniruhusu niwe nachanganya na kizungu ili kufafanua vizuri" It is simple, but not easy.
Kutajirika inatakiwa ufanye kitu rahisi kila siku lakini kwa muda mrefu kiasi, tuseme miaka kumi, unafanya kitu kilekile, hapa ndipo inapoboa. Utajiri hauhitaji uwe na mbwembwe, haihitaji mizuka wala ngedembwe.

Mfano; kama wewe umeajiriwa, labda unalipwa laki tano, kila ukipokea mshahara, unaweka laki mbili pembeni, laki tatu ndio unatumia na familia yako, kila mwezi. Baada ya mwaka mmoja utafikisha milioni moja na laki mbili, unanunua bodaboda, kisha unaendelea na zoezi lile lile la kuweka laki mbili kila mwezi...

Halafu kila mwaka unanunua bodaboda, kama ukiendwlea hivyo kwa miaka kumi, hata kama hujawa tajiri lakini utakuwa umepiga hatua kubwa. Simple but not easy, not easy because it a simple and mechanical way of doing things, haikupi mwanya wa kuandaa birthyfay parties kwa sababu utaingilia ratiba ya kuweka laki mbili....

Not easy kwa sababu ni aina ya maisha inayokosa msisimko, na binadamu tunataka msisimko, leo umeenda club, kesho umenunua dela jipya, unachukua mkopo benki unanunua vitz, hivyo vyote ni msisimko wa maisha... Kwa hiyo unachokisema ni siri, kimekaa kwenye kitu kinaitwa DELAYED GRATIFICATION, japo kuna mengine pia ya kuambatisha hapo.

Nimejaribu kufafanua kwa ufupi.
Asante kiongozi
 
safuher mfano mmojawapo ni hayo hapo. Ni mengi kinahotakiwa ni uamuzi thabiti bila kujali mtu atakufa au la kwa wewe kuchukua na kutekeleza uamuzi wako.

Zingatia

Ikiwa degree (shahada) yako ya uchumi huu usioweza kukufanya uione milango ya uchumi unasomea miaka mitatu. Vivyo hivyo tambua hauwezi kujifunza nidhamu na siri za utajiri kwenye post au jibu moja kama hivi. Ni jambo unatakiwa uingie kujifunza kwelikweli. Na kwa wakristo Yesu ni mfano (mentor/great teacher) wa wewe kufikia mafanikio yako ya juu kabisa na Biblia ina kila mwongozo unaoutaka katika uchumi. Nilipolijua hili nilishangaa sana na hii ni mojawapo ya siri kuu hatuambiwi.

Anza sasa kuzisaka siri, ni kazi ngumu kwa asiependa lakini nyepesi ukiamua.
 
Tokea zamani nimekuwa siamini msemo unaosema kwamba utajiri unahitaji uvumilivu,subira,kupitia magumu nakadhaalika.

ninachoamini ni kwamba utajiri sio mgumu kupatikana ni rahisi lakini huwenda njia zake hizo watu hawazijui(zina siri)

Tukumbuke kuwa kitu kuwa rahisi haina maana kwamba watu watakijua kitu hiko,kinaweza kuwa ni rahisi na bado ikawa ni siri pia.

Mimi naamini utajiri una formula zake nyepesi nyepesi za siri ambazo wachache wanazifahamu.

KAMA utajiri ni kupitia magumu mbona leo tuna idadi kubwa ya watanzania wanaofanya kazi ngumu za kilimo na ujenzi na bado hawawi matajiri ?

KAMA utajiri unahitaji muda ukiwa katika kazi ngumu mbona kuna watu wanazeekea na kufia katika kazi za ujenzi miaka na miaka bila kuwa matajiri ?

Kama utajiri ni kupitia magumu na mateso basi leo watanzania wengi sana wangekuwa matajiri kwa sababu idadi kubwa ya watanzania wanafanya kazi ngumu.

Bakhresa wanasema alitoka kwenye kazi ya kushona viatu,mbona kuna wanaozeekea katika kazi hiyo hawawi kama bakhresa ?

Utajiri naamini ni siri,tena siri ni nyepesi mno lakini nadhani huwenda wengi wetu tunaamini kwamba lazima tuteseke kwanza na kuumia ndipo tupate utajiri.

Nakataa kujifariji kwamba mateso ninayopitia ni ishara ya kutoboa mbeleni kwa sababu wapo wanaozaliwa kwenye mateso na kufia kwenye mateso bila kuuona utajiri.
Utajiri ni Mungu akiamua kuweka neema zake kwako. Unaweza ukawa na bidii ya kujenga ukuta kwa mate but kama Mungu hajakubariki hupati kitu bro
 
Usile mchana.

Manake tengeneza pesa..save pesa..investment pesa ilete pesa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Utajiri unatokana na fursa zilizopo. Na anaeytengeneza fursa hizo(mazingira ya kuwa tajiri) ni serikali.
Sikubaliani na wewe kwa mazingira mengi tu.

Kwa sababu serikali inayomuongoza bakhresa ndio hiyo hiyo inayomuongoza babu yangu kijijini.

So ingelikuwa swrikali ndio sababu basi tungekuwa na bakhresa wengi.

Nina hakika kuna something behind
 
Back
Top Bottom