Siamini nilichokishuhudia: daladala level seat, hakuna foleni, hakuna kelele, abiria hawasukumani, makonda hawatukani, unafika haraka unakoenda

Siamini nilichokishuhudia: daladala level seat, hakuna foleni, hakuna kelele, abiria hawasukumani, makonda hawatukani, unafika haraka unakoenda

Kila kitu kinawezekana,vituo vya Daladala vikiboreshwa watu wawe wanapanda kwa kanuni na usimamizi ukiwepo (kila kulipo na check point) tutaweza.
Huu ugonjwa ni kipimo kizuri cha akili na ustaarab.
 
Kilicho sababisha gari nyingi kuwa level seat sio tu kwa sababu ya tamko la mamlaka, ila msingi mkuu wa kupungua kwa foleni mjini na kutojaza abiria. Ni kwa kuwa ofisi nyingi Sana zimefungwa kutokana na hili janga la Corona. Mfano mi nilko maeneo ya chole road masaki hapa Kuna baadi ya ofisi kadhaa zimefungwa. Kwa hiyo hata hawa akina mamantile pia wamefunga baadhii ya sehemu zao, kwahiyo automatic akina mamantile lie hawapandi tena daladala kadhalika sie vinyozi wa michongoma hatuendi vibaruani pia Kuna hawa madada wa maofisini hawaendi tena na vipasso vyao maofisi. Kwa hiyo vipasso viko home na vx pia za maboss zako home pia. lazima foleni zipungue barabarani na abiria pia niwachache kwasababu hizo hizo. Nadhani nimeeleweka hata bar tupo wachache meza kibao nyeupe kwakuwe wengine anapoingia job ndio anapata issue za kupata japo hela ya bia. Si unajua zile zetu mara boss chlorine ya swimming imeisha Mara ooh boss bomba limepasu naomba pesa ya connect na tap, Mara mafuta Katika jenereta imeisha. Dili zote hizi zinafanyika tukiwa kwa ofisi. Sasa hivi mwendo wa kuokoka tu kwa razima. Ukiulizwa vp honey uku wapi nasingizia Corona kumbe dili zimekata. Kwa kherini naona dada anakuja na bili mkononi nimlipe hivi visafari vi2 nikalale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Hii Hesabu Yako Ndugu---

Toa Pesa Ya Boss 100,000/=,
Toa Pesa Ya Mafuta Kwa Kesho Yake,
Toa Pesa Ya Service Ya Iyo Gari Kwa Mwezi,
Toa Pesa Ya Kula Konda Na Dereva,
Toa Sio Pesa Bali Ela Ya Wapiga Debe Kwa Vituoni,
Toa Pesa Ya Konda/Dereva Kupeleka Nyumbani....

Tupe Hesabu Yake Sasa

Hata hivyo watapata tu hela tena bila shida. Assume daladala itaenda mjini safari tano kwa siku. Kwa hiyo kwenda na kurudi ni trip 10. Kila daladala inabeba abiria 31. Kama kila abiria atatoa TZS 400, maana yake kwa siku konda atakusanya 10 x 31 x 400 = TZS 124,000. Hapo hatuhesabii anayepanda na kushuka njiani na mwingine kupanda.

Pia magari yatakuwa kwenye hali nzuri kwa sababu hawatayaoverload, hivyo kupungua kwa gharama ya service.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Unajuwa hawa wamiliki wa daladala,hawajui kama gari inapotengenezwa kutoka kiwandani,imeshapangiwa mahesabu ya kubeba abiria au uzito kiasi fulani,unapozidisha uzito,ni kuwa unaharibu machine,body ya gari,chassis,mipira,na vipuli kadhaa vya gari.Ndio pale mmiiliki wa gari anapopata hasara,ya kila mara kutengeneza gari.Kubadilisha mipira ya gari kwa mda mfupi.Gari inachakaa kwa mda mfupi,kabla hata kurudisha hela ya manunuzi ya gari.Kwa tamaa ya kujaza abiria(uzito mkubwa),kuliko uwezo wa gari.
Hata hivyo watapata tu hela tena bila shida. Assume daladala itaenda mjini safari tano kwa siku. Kwa hiyo kwenda na kurudi ni trip 10. Kila daladala inabeba abiria 31. Kama kila abiria atatoa TZS 400, maana yake kwa siku konda atakusanya 10 x 31 x 400 = TZS 124,000. Hapo hatuhesabii anayepanda na kushuka njiani na mwingine kupanda.

Pia magari yatakuwa kwenye hali nzuri kwa sababu hawatayaoverload, hivyo kupungua kwa gharama ya service.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magari ya Mlandizi na Kibaha to Mbezi nimeona yamesimamisha watu na Traffic wapo kibao muda wa around saa 12 jion , rushwa noma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom