acha kujitetea ujinga. ulipaswa kuleta habari yako ikiwa kamili.
JF inatoa fursa pana kwa author kuandika habari yake kwa undani zaidi ili kutomuacha msomaji njia panda. link inakuwa ni ziada tu ya ku support kile ulichoandika.
hata hivyo link sio kitu salama sana na ndio maana wataalamu wa mifumo ya ulinzi wa kimtandao, siku zote wanashauri kutokukimbilia kufungua link ambayo huielewi.
hii inatokana na baadhi ya wahalifu wa kimtandao(hackers), kutumia link kama portal ya kukusanya taarifa mbalimbali za watu wengine kwa malengo ya kutenda uhalifu.