GE2025 Siasa za Bukoba Mjini Kati ya Lwakatare na Kagasheki ilikuwa hatari sana ile ligi!

GE2025 Siasa za Bukoba Mjini Kati ya Lwakatare na Kagasheki ilikuwa hatari sana ile ligi!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mkuu hata mimi kwa kumbukumbu zangu hao jamaa walikua na battle kubwa unaweza ukadhani hawatoki chama kimoja.... unaambiwa hao jamaa walikua ni full kutafutana kuuana jimbo halitulii..
Kipind hicho siasa ilikua tamu sana kufatilia alaaniwe vibaya aliyetuharibia mfumo wetu wa siasa safi na kutufikisha hapa tulipo
 
Lwakatare alikuwa CHADEMA kama nakumbuka vizuri? Halafu akaja kuhama? Kweli umekumbusha mbali. Ni moja kati ya majimbo yaliyokuwa yanatia msisimko. Ule CCM ya wakati ule ilikuwa na watu weledi. Walikuwa hawana ujinga wa kukata majina ya wapinzani au kuingiza kura vituoni... na kama ilifanyika basi ilikuwa kwa kiwango kidogo. Wapinzani walikuwa mpaka wanashinda kesi mahakamani na matokeo yanatenguliwa.
Kabisa hapo napendekeza kikwete akumbuka,kwakuifanya ccm isisinzie kama sasa inakoelekea, maana CCM ni kama ilisaulika bukoba mjini,waliogopa hata kukatiza mitaani na uniform zao,ilikuwa raha sana,lkn sasa mmmh!! ,tusitarajie hivi vyama sijui vya ubwabwa na wenzake,hawataambulia chochote safari hii,ngoja muone.😭😭
 
Hawa ilika mahala bukoba iligawanyika pande mbili. Pale manisapaa baraza la madiwani liligawanyika timu meya timu mbunge. Ukienda vijiwe vya gahawa sokoni, stand kuna vijiwe timu meya, timu mbunge na timu pinzani ukijichanganya kwenda kwa wapinzani utarudi meno huna. Uhasama wao ulikua mkubwa sana hawa mabwana miradi mingi tu ya kimaendeleo ilishindwa kufanyika bukoba sababu ilikua inakwamishwa kimaamuzi ktk vikao vya madiwani. Ikihisiwa huu mradi kuna nguvu ya mbunge basi timu meya wataenda kuukwamisha kwenye baraza la madini la maamuzi,ivyo ivyo mradi ukionekana kuna mkono wa meya utamishwa na timu mbunge. Pm wakati ule Mzee Pinda aliwapatanisha bila mafanikio.
Mkurugenzi na watendaji wake walikuwa vyambo.
 
Mimi mchuani mkali ninao ukumbuka ulikuwa kati ya Dr Masha na Dr Shija kule Sengerema.
 
Kipind hicho siasa ilikua tamu sana kufatilia alaaniwe vibaya aliyetuharibia mfumo wetu wa siasa safi na kutufikisha hapa tulipo

Magufuli katuharibia siasa halafu akafa. Yule jamaa wa hivyo, Leo ubunge ni kwaajili ya CCM
 
Lwakatare alikuwa CHADEMA kama nakumbuka vizuri? Halafu akaja kuhama? Kweli umekumbusha mbali. Ni moja kati ya majimbo yaliyokuwa yanatia msisimko. Ule CCM ya wakati ule ilikuwa na watu weledi. Walikuwa hawana ujinga wa kukata majina ya wapinzani au kuingiza kura vituoni... na kama ilifanyika basi ilikuwa kwa kiwango kidogo. Wapinzani walikuwa mpaka wanashinda kesi mahakamani na matokeo yanatenguliwa.
Awali alikuwa CUF baadae akahamia Chadema
 
Hao Kamani na Chegeni wana uhusiano wa karibu sana kama sikosei ni mtu na mjomba wake, hakika uchu wa madaraka ni hatari sana
 
Back
Top Bottom